Hivi ni kweli JamiiForums ina uhusiano na Wapinzani?

KiparaChaDamu

Member
Nov 27, 2018
12
18
Wanajamii forum naomba kuuliza.

Kuna tetesi kuwa Jamii Forum ina mahusiano ya karibu na WAPINZANI. Je, ni kweli?

Kwani kuna baadhi ya post zenye kuwagusa wapinzani huondolewa muda mfupi tu baada ya kupostiwa.

Nahitaji maoni yenu wadau. Tafadhali msiniondoe ni maoni tu.
 
Wanajamii forum naomba kuuliza.

Kuna tetesi kuwa Jamii Forum ina mahusiano ya karibu na WAPINZANI. Je, ni kweli?

Kwani kuna baadhi ya post zenye kuwagusa wapinzani huondolewa muda mfupi tu baada ya kupostiwa.

Nahitaji maoni yenu wadau. Tafadhali msiniondoe ni maoni tu.
Ndugu,

JamiiForums si dude linaloamua lijiendeshe vipi bali wanachama ndo huamua mwelekezo wa mijadala.

Aidha, JamiiForums ni zaidi ya Jukwaa la Siasa.

Sasa:

1) Tetesi hizo unazodai za JamiiForums eti kuwa na uhusiano na Upinzani ndo nazisikia sasa. Si ilikuwa ikidaiwa ni CHADEMA? Sasa wamekuwa wapinzani wote? Unajua kuwa hata hao wapinzani kuna wanaodai JF ni CCM?

2) Ili twende sawa, itaje mijadala ‘inayowasema’ wapinzani ambayo imeondolewa ili tuache kuishi kwa nadharia tu. Ni makosa tukijadili kitu kwa madai ambayo ni ‘baseless’ wakati ushahidi upo.

3) Tuzame katika miongozo:
Umesoma vema mwongozo wa ushiriki katika kutoa maoni? Soma hapa > JamiiForums' Community Engagement Guidelines - JamiiForums


Aidha, ulisoma ufafanuzi juu ya aina ya mada zinazoweza kuondolewa au zinazoweza pelekea ukafungiwa ndani ya JF? Soma hapa > Topic gani hufungwa au kufutwa kabisa JF? - JamiiForums

4) Basi tuseme (kwa nadharia tu) kuwa mabaya ya upinzani yakiwekwa yanafutwa... Je, Kuna mazuri kuhusu Chama Tawala au Serikali uliyaweka yakafutwa? Unaweza kukumbuka ni yepi (kwa mifano hai)? Kama yapo mazuri na hayaandikwi huku tukikazana (labda) kuandika mabaya ya wapinzani, unadhani hayo mazuri nani ataueleza umma usioyajua na wanaoyajua wameyakali wenyewe?

Mkuu wangu, ulimwengu huu wa mitandao unatoa upana wa kuhabarisha/toa taarifa kwa umma na tena kwa gharama nafuu au bure. Tumieni hii fursa kwa uzuri bila kutafuta mchawi! Ni rahisi, ukikwama wewe nitafute pembeni nikufafanulie kwa uzuri na bure tu!

Ni hayo kwa leo.
 
Mi kwa upande wangu naona ni kweli maana maada nyingi zinazodumu humu ni zile zenye mlengo wa kushoto kama wapo naomba kusikia kutoka kwao threads nying zimekuwa zikifutwa
 
Penye ukweli uwongo hujitenga..........

Kwa kuwa wapinzani wanausema ukweli mtupu na wanaCCM wanaongea propaganda tupu ili kuuimarisha utawala wao dhalimu na kwa kuwa penye UKWELI UWONGO hujitenga, ndipo hapo unapoweza"kuhisi" kuwa uongozi wa JF ni wa wapinzani!

Kwa kuwa posts za wanaccm zinapotea baada ya muda mfupi baada ya kuwekwa humu JF kwa kukosa wachangiaji
 
ni kweli, jamii forum haitakiwi kuwa na upendeleo, jana nilipost kuhusu wapinzani post yangu ikafutwa. lkn post zinahusu kuiponda CCM na serikali zinapewa kipaumbele
Wewe utapigwa leo hii...
Huwezi kuachwa uandike mada za uchochezi kama hizi
 
Kwa uzoefu wangu humu jf with more than 10 years, nijuavyo JF sio ya Wapinzani, ni ya wote, ndio maana CCM wapo, Wapinzani wapo, na sisi tusio na vyama tupo, ila imetokea mashabiki wa upinzani ndio wametamalaki humu zaidi hadi kuwafanya wana jf waandamizi wa CCM kama kina Nape, Mwigulu, Shonza, Makonda, Dr. Kigwangala etc kuingia mitini, na wengine kutumia majina ya bandia kufuatia kushambuliwa kama mpira wa kona.

Hilo la kufutwa threads, kila un appropriate threads zinapaswa kufutwa bila kujali ni za topic gani, hadi topics za sisi tusio na vyama zzitafutwa.

Kwa vile wafuasi wa uapinzani humu ni wengi, it's obvious threads zao pia zitakazo futwa ni nyingi, kama ulivyo uteuzi wa Kanda ya Ziwa, kufuatia wingi wao, kwenye kila kitu lazima wawe wengi ukiwemo uteuzi.

P
 
Wanajamii forum naomba kuuliza.

Kuna tetesi kuwa Jamii Forum ina mahusiano ya karibu na WAPINZANI. Je, ni kweli?

Kwani kuna baadhi ya post zenye kuwagusa wapinzani huondolewa muda mfupi tu baada ya kupostiwa.

Nahitaji maoni yenu wadau. Tafadhali msiniondoe ni maoni tu.
Hata macho huoni! Nadhani ni wakati wenu CCM kuanzisha jukwaa lenu
 
Back
Top Bottom