Hivi ni kweli hizi ni shule za vipaji maalum?

founder wa Facebook alienda shule za vipaji maalumu..!? Maana mfano wako ni unrelated kbs na kitu nilichozngumza....
I knew that you gonna say something worst but not that one.......unajua found wa facebook? yule ndo mwenye kipaji sasa....mwenye kipaji atafanya kila njia na kutumia hivyo visivyochangia kufanya maajabu..kufanya maajabu.. au alienda huko kukariri tu...
 
Hali zenu wanajamvi hasa great thinkers!!

Nawaomba mnisaidie kuwaza:
1. Je hizi shule zetu za vipaji maalum zinakuza vipaji gani?
2. Je ni njia gani zinatumika kukuza vipaji husika?
3. Je walimu wa hizi shule wana vipaji pia?
4. Hivi kuna "vipaji maalum" ambavyo hufundiswa/hukuzwa kwenye shule zetu za vipaji maalum kweli?
5. Je vigezo gani wanatumia kujua vipaji vya watoto kabla ya kuchaguliwa?
6. Je kujua KKK ni kuwa na kipaji?
7. Baada ya kumaliza hizi shule vipaji vyao huendelezwa wapi?

====
Kama hakuna hivyo vipaji maalum

(1) Kuna haja gani ya kuwa na shule chache ambazo zinapewa huduma bora kisha tukazipima sawa na shule zenye mazingira magumu?

(2) Je, inawezekana kwamba zilianzishwa kwa ajili ya watoto wa kinafulani tu? ila wanajifanya kupeleka wengine kuficha ukweli?

(3) Wale wanaopelekwa technical school huishia kwenye vyuo vya ufundi kama Dar tech, Mbeya tech nakadhalika, hawa wenye vipaji mwisho wao wapi? kama haupo why ziendelee kuwepo?

(4) Wizara husika inasera na dira gani kuhusu vipaji? kwao vipaji ni nini?

Nangu Mandokwa.
Ule ulikuwa uongo mtakatifu,hakukuwa na shule za vipaji maalum,
Serikali ilikuwa Haina rasilimali za kutosha,ikachagua shule chache na kuziendeleza kwa kuzipatia Miundombinu ya kutosha,Waalimu,vitabu,madarasa,hostel,na ikawa inachukua wanafunzi wachache waliofaulu kwa alama za juu zaidi ndio wanaenda hizi shule,kipindi hicho Kumbuka shule za binafsi zilikuwa chache sana.
Miaka ya 90,kulikuwa hakuna kufaulu darasa la saba,ilikuwa ni kuchaguliwa,unaweza ukafaulu lakini usipate nafasi ya kuchaguliwa Kwenda shule za serikali(na kipindi hicho usipoenda shule za serikali unaonekana ulikuwa kilaza darasani)
Cha ajabu nilikutana na wale wa "vipaji maalum"chuoni,niliwakimbiza balaa,Richa ya kusoma private school Tena kijijini.sikuona tofauti yao waliosoma Tabora boys,Kilakala,Tambaza,Moshi tech nk,
Mie na PCM yangu ya sekondari nilikimbiza sana.
Shule yoyote inaweza kuwa ya "vipaji maalum"kama ikiwa na Miundombinu yote muhimu,Waalimu wa kutosha,vyumba vya madarasa,vitabu,library,maji,umeme,nk
 
Umebaki kuvalishwa dera tu.
Una wivu wa KIKE almanusura uwe mshikishwa ukuta.
Kama hukubahatika kusoma Special School (Tabora Boys, Mzumbe, Kibaha na Ilboru) pole sana.
 
Umebaki kuvalishwa dera tu.
Una wivu wa KIKE almanusura uwe mshikishwa ukuta.
Kama hukubahatika kusoma Special School (Tabora Boys, Mzumbe, Kibaha na Ilboru) pole sana.
Mbona umekazana kushadadia wanaume wenzio tu? We uliesomea hizo shule unanini cha ziada zaidi ya hao unaowananga? We ndo una wivu! Punguza shobo.
 
Wengi humu waliosoma hizo shule na pengine chuo hawajui kutofautisha" Gifted and talented"
Wengi wenu humu ni gifted sio talented.
Gifted anafaulu darasani lakini talented uwanjani.
Wachache sana wanakuwa both.
Ronaldo na Mess ni talented sio gifted kwa sababu darasani hawakuomyesha uwezo wa juu.
Hakuna shule za talented ila zipo za gifted.
Kuna vyuo vinachukua talented navyo ni Bagamoyo na butimba.
Naweza sema kwa mbali football academia zinakuza vipaji.
Neno vipaji halikidhi maana kama kingereza, kingereza kimetofautisha uwezo wa darasani na nje ya darasa.
Kuna makosa ya kimaana katika neno vipaji.
 
Back
Top Bottom