Hivi ni kweli hizi ni shule za vipaji maalum?

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
614
1,000
Hali zenu wanajamvi hasa great thinkers!!

Nawaomba mnisaidie kuwaza:
1. Je hizi shule zetu za vipaji maalum zinakuza vipaji gani?
2. Je ni njia gani zinatumika kukuza vipaji husika?
3. Je walimu wa hizi shule wana vipaji pia?
4. Hivi kuna "vipaji maalum" ambavyo hufundiswa/hukuzwa kwenye shule zetu za vipaji maalum kweli?
5. Je vigezo gani wanatumia kujua vipaji vya watoto kabla ya kuchaguliwa?
6. Je kujua KKK ni kuwa na kipaji?
7. Baada ya kumaliza hizi shule vipaji vyao huendelezwa wapi?

====
Kama hakuna hivyo vipaji maalum

(1) Kuna haja gani ya kuwa na shule chache ambazo zinapewa huduma bora kisha tukazipima sawa na shule zenye mazingira magumu?

(2) Je, inawezekana kwamba zilianzishwa kwa ajili ya watoto wa kinafulani tu? ila wanajifanya kupeleka wengine kuficha ukweli?

(3) Wale wanaopelekwa technical school huishia kwenye vyuo vya ufundi kama Dar tech, Mbeya tech nakadhalika, hawa wenye vipaji mwisho wao wapi? kama haupo why ziendelee kuwepo?

(4) Wizara husika inasera na dira gani kuhusu vipaji? kwao vipaji ni nini?


Nangu Mandokwa.
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,047
2,000
Iyunga Boyz Enzi hizo kwa kweli tulkua vipaji maalumu


Mtu unafundishwa lecture mbili za mechanical engineering na bado unapata A ...

Alooo ... Ma mechanical draft


Kama uwezo wako ni wa kawaida ule mziki hautoboi


Engineering science form three najifunza mambo ya advance

Kumbe mwamba ulikua jirani? Ifunda The Glorious Technical School live long Forever.
Unapiga Unga (Masomo ya Ufundi matatu) Civics, Kiswahili na English kama kutimiza wajibu tu. Zilisababisha penalty sana.
 

Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,465
2,000
Hizo shule za "vipaji maalum" ninadhani wanaongoza kwa maisha magumu shuleni na walimu wachache, hasa wa Sayansi (My experience from Tabora School).

Ila kutokana na vipaji vyao katika Elimu, ndio maana wanaongoza (kwa miaka karibu yote) kwa kufaulu vizuri.

It takes "kipaji maalum" kufaulu vizuri katika mazingira ambayo ordinary people would fail vibaya.

Pale kigezo cha kuingia ni ufaulu wako - haijalishi ni mtoto wa kigogo au kabwela.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom