Hivi ni kweli hii sababu inatosha kuvunja uchumba ama nimeingizwa cha kike?

mps

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
387
527
Ni hivi kuna binti nimekuwa nae kwenye uchumba kwa miaka miwili sasa yeye ni muislam na mimi mkristo, tumebahatika kupata mtt japo hatukuwahi kuishi pamoja kama mme na mke ila tulishakubaliana awali kwambani yeye atabadili dini na ndoa tutafunga kanisani na wazazi wake aliwaambia mama akakubali baba akawa anasitasita.

Cha ajabu kipindi akiwa mjamzito alitamkia kuwa hawezi olewa na mkristo nikajua anatania ila mpaka sasa kasimamia msimamo huo. Daa! kiukweli namhurumia mtoto wangu kukosa malezi ya baba na mama kwa sababu zisizoeleweka nimeamua kumpa go ahead na mtoto kalazimisha kumpa jina la kiislam.

Naombeni ushauri kwa wenye uzoefu na haya mambo
 
Mshukuru Mungu kwa kila jambo maana hujui kakuepushia nn. Ila issue ni kwa mtoto jinsi ya kumweka upande wako hasa ktk imani
 
Imani hufunzwa na ukifuzu imani hulindwa...sioni haja ya kulazimisha kisicho lazimishika mwache aiishi imani yake. Mungu ni mwema ukimtumaini utampata wa maisha yako na waimani yako.
 
Thanks kwa michango yenu coz hata mm sijataka kutumia nguvu nyingi kumshawishi kumuoa yote namwachia Mungu ila kibaya zaidi ni kwamba kipato chake sio cha uhakika kujisimamia hivyo anasema akipata wa dini yake ataolewa.My kid is too young ningemchukua kwakweli
 
Mie sizan kama waislam Mungu wao n tofaut na wakristo.. sasa cjui hiz sababu za din zinatoka wap ikiwa kila pande inamwabudu Mungu mmoja, Acha kuleta udin iwe sababu ya mtoto kukusa malezi yako hata huyo Mungu mnae mgawa kwa mafungu ahafiki ilo swala
 
Nadhani chamsingi nikupatia mahitaji na malezi bora mtoto, dini hata umlee dini gani lakini mwisho wa siku anaweza badili akiamua,as long as wewe ni Baba timiza majukumu yako mengine muachie mwenyezi mungu......
 
Huwa nawaambiaga watu, mahusiano kati ya watu wenye dini tofauti huwa ni shida ila they brand me a 'hater'. Its not easy, ndio nyie wawili mnakubaliana lakini once kila mtu akarudi makwao, aisee the pressure is not light, kuna watu hawawezi kuhandle extreme pressure ndio kama huyo dada. Its not easy for a person to change her/his religious beliefs, yani mtambo wake aureconstruct, for you..heee..alafu baadae uanze kumnyanyasa, kweli atakuua.

Watu wanakurupuka to get married hvyo hivyo ndoa ya kiserikali, sawa, ila umefikiria mbele? what about the children? watalelewa katika dini gani? kuna watu wengne wanasema kabisa eti tutaachia mtoto achague, mxa! the child is 5yrs old and doesnt knw a mosque nor church, lets say mtoto msichana, baba mkristo mama Islam, baba kanisani anaenda mara 2 kwa mwaka alafu mnasema awe mkristo, nani atampeleka? kama sio kuchangany watoto tu, psychological torture, sijui ndio tutatoa vizazi wapagani tunakoenda?!...SIO RAHISI KAMA WATU WANAVYOFIKIRIA

In the end tunaacha familia inasambaratika..baba kule, mtoto mmoja huku mwngne kule...na wale wanaochepuka na wanapata watoto juu,khaaa baba kule, mtoto kule (watoto wanaathirika sana, ukiwaona wale ambao wamepitia this and could not withstand the pain, aisee,inauma sana, kuna wale they just end up growing up not caring, generation zijazo zitakuwa na psychological issues nyingi)
 
Umekosea uliposhurutisha abadili dini, oaneni bomani kila mtu abaki na dini yake. Ndo hivyo you are free to choose but not free from consequences of your choices.

mps
 
Last edited by a moderator:
mie sizan kama waislam Mungu wao n tofaut na wakristo.. sasa cjui hiz sababu za din zinatoka wap ikiwa kila pande inamwabudu Mungu mmoja, Acha kuleta udin iwe sababu ya mtoto kukusa malezi yako hata huyo Mungu mnae mgawa kwa mafungu ahafiki ilo swala
Mkuu, natofautiana na wewe; Mungu 1 hawezi kuwaambia Wakristo "usiue" halafu huyo huyo awaambie waislamu "ueni ------". Mungu 1 hawezi kuwaambia wengine sameheeni wanaowaudhi halafu huyo huyo awaambie wengine lipizeni kisasi! Siamini na sita amini kama mungu wa waislam ndio Mungu wa Wakristo.
 
Back
Top Bottom