Hivi ni kweli hatuna haja ya KATIBA MPYA? Uko wapi UZALENDO wa viongozi wtu?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,145
2,000
Hey guys, hivi ni wapi tunataka kilipeleka taifa hili? Ni kweli jamani imefikia mahali tunasema hadharanu kabisa kua hatuna haja ya kua na katiba mpya kipindi hiki ambacho kweli tunalia na mifumo mibovu inayozuia taifa letu kupiga hatua? Heo hii panga pangua ya viongozi kwenye mamlaka za serikali ni kwa sababu ya mifumo mibovu ya kikatiba bado tunasema katiba haihitajiki? Serious?

Kiongozi wetu anasama kua hatuna haja ya katiba mpya na kuna watu wanafurahi na kupiga makofi?Watanzani kuna mahali tunakosea sana, vyeo vyetu tunaviona kua na umuhimu zaidi kuliko mifumo itakayoweza kubadili taifa letu hasa kwa vizazi vijavyo.

Sioni uzalendo wa kiongozi yeyote katika taifa letu, kama tunashindwa kusimamia rasilimali zitakazotumika kwenye maandalizi ya katiba tunasingizia kua ni anasa, huu sio uzalendo hata kidogo. Hatuwezi kufika kwa hali hii hata malaika aje wa aina gani, yaani pesa za kodi ya wananchi kutimika kwenye katiba ni anasa?Tunashindwaje kizisimamia zisitumike kama anasa?Mungu atusaidie sana maana hatujui kama tunakosea.

Tuna katiba mbovu yenye mifumo ya kikoloni karne hii ya 21 ambayo tunataka tutoke hapa tulipo lakini tunasema hatuoni umuhimu wake? 2020 ikifika ndio tutajua kua kuna umuhimu wa hili, hakuna kiongozi atakayeweza kulizuia hili maana litakuja lenyewe automatically kulingana na matukio tutakayokumbana nayo.

CCM mmewadanganyia watanzania katiba mpya na leo mnarudi kusema hamuitaki hadharani ili muendelee kuwapoteza? Hakika mtalipa katika hili, tangulize uzalendo na tumieni fursa yenu kama chama tawala kulisaudia taifa.
 
Kajolijo

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,380

wewe katika pita pita zako zote uliwahi kusikia akinadi katiba mpya wakati wa kampeni,.. kama hamna kwanini ulimpgia kura. kama unaitaka subiri 2020 muiweke kama ajenda katika kampeni zenu
 
koyola

JF-Expert Member
May 20, 2015
2,483
2,000
Marekebisho ya ukakasi yanayolalamikiwa kwenye katiba iliyopo ni kufanyia marekebisho na kuondoa vipengele ukakasi vilivyopo na kuweka ambavyo vinakubalika na wengi kama kuchukua yaliyopo kwenye tume wa warioba na kufauta taratibu za kibunge kuyaweka Mwisho tutajikuta na katiba iliyo bora
 
godfrey wilson

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
447
500
wewe katika pita pita zako zote uliwahi kusikia akinadi katiba mpya wakati wa kampeni,.. kama hamna kwanini ulimpgia kura. kama unaitaka subiri 2020 muiweke kama ajenda katika kampeni zenu
kwani hiyo katiba mnataka ifanye jambo gani ufurahie wewe au kutaka nn ama wana siasa na polojo zao. mulizeni Odinga na katiba alitaka sana nia aingie madarakani haikuweza kumwingiza sasa anataka ibadilishwe tena akifikiri katiba ndio inapiga kura
 
jumamwaki

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
239
250
Shida ni kuwa katiba mpya inawezekana kupatikana kabisa kwa asilimia kubwa ...isipokuwa wenye uwezo wa kuitaka hawana nguvu ya kufanya hivyo... Na wenye uwezo au maamuzi yenye nguvu kwa nchi yetu ni wale ambao hawana nia ya dhati ya kufanya mabadiliko kwani wakifanya hivyo hawatapata mwanya wa kuwadhibiti watu wenye mitazamo tofauti...... Mkumnbuke kuwa katika nchi yetu wenye mamlaka hawataki kusumbuliwa sana na maoni tofauti wanataka kuamini kuwa wao ndiyo wanaopaswa kupanga mambo na wewe mwananchi ni kutekeleza tu ndio wao wanafurahi kwa sababu wanapata mwanya wa kuendelea kuwepo madarakani..... kwa sababu kama wana nchi wanahitaji katiba mpya iweje wewe mwingine useme mimi sihitaji kuandaa pesa kwa ajili ya kuiendeleza mchakato wa katiba mpya ilhali wananchi hawa ndio wanaotoa pesa zao kwa ajili ya kila kitu kwa ajili ya kupata kile wanachohitaji ..... wanalipa kodi wakihitaji, balabala, maji, maendeleo yote, lakini kikubwa kingine wanachohitaji ni katiba na kinachodhibitisha ni kuwa mchakato ulishaanza mapema , na ulitengewa hela hizo hizo za kodi za wananchi, /.....................................Hekima inahitajika sana katika uongozi kuliko kitu kingine chochote kile ,uongozi hauhitaji, Phd, hauhitaji silaha , hauhitaji ubabe, , Ukitumia mbinu tofauti na Hekima Ni vigumu sana kufanya Maamuzi mazuli, Silaha na ubabe ni mbinu ambayo haiwezi kudumu ila Hekima ni silaha yenye kudumu.......... MUNGU IBALIKI TANZANIA , BALIKI VIONGOZI WETU watumie HEKIMA badala ya PHD na Ubabe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom