Hivi ni kweli eti zile shanga wamasai zinatoka baharini?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Sio mara ya kwanza au ya pili kusikia hii habari hata siku za nyuma niliwahi sikia kuwa eti zile punje wanazotengenezea shanga hawa wamasai huwa eti zinaokotwa baharini pale maji ya bahari yanapohama kwenye ule mchanga eti ukienda kupepeta ule mchanga unazikuta zile punje hivi kuna ukweli wowote au ni maneno tuu ya kijiweni,naomba mwenye kujua anitoe tongotongo.
 
Nilishadanganywaga hivyo zamani ila nimejiuliza sa hivi kuwa hivi hadi kale katobo kanakuwa kako tayar tena kwa muondo tofauti tofaut wenye kufanana ... Mengine nikujiongeza alafu waingia Google
 
Kwahiyo mpaka dodoma kuna bahari,
Maana wamasai hayo madude kwenye viatu wanayo!
Au ndiyo kusema huwa wanakuja dar wanakusanya kama ndoo,
And then wanaruka chap kusambaza mikoani.
 
Sio mara ya kwanza au ya pili kusikia hii habari hata siku za nyuma niliwahi sikia kuwa eti zile punje wanazotengenezea shanga hawa wamasai huwa eti zinaokotwa baharini pale maji ya bahari yanapohama kwenye ule mchanga eti ukienda kupepeta ule mchanga unazikuta zile punje hivi kuna ukweli wowote au ni maneno tuu ya kijiweni,naomba mwenye kujua anitoe tongotongo.
Masai na bahari wapi na wapi ?
 
  • Thanks
Reactions: Ctr
Mi mwenyewe nimejiuliza nikajaribu kuuliza wwngine wameenda mbali wanadai eti huwa zinakuwa zimetengenezwa na majini ndo maana zinakuwaga hata na rangi tofauti
Nilishadanganywaga hivyo zamani ila nimejiuliza sa hivi kuwa hivi hadi kale katobo kanakuwa kako tayar tena kwa muondo tofauti tofaut wenye kufanana ... Mengine nikujiongeza alafu waingia Google
 
Usiseme shanga za wamasai maana zinatengenezwa china. Hata yale manguo wanayojitanda hutengenezwa ughaibuni huko wanaletewa then tunawasifu kuwa wanadumisha mila.
 
Nimewakilisha ki hivyo ili nieleweke kiurahisi zaidi
Usiseme shanga za wamasai maana zinatengenezwa china. Hata yale manguo wanayojitanda hutengenezwa ughaibuni huko wanaletewa then tunawasifu kuwa wanadumisha mila.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom