Hivi ni kweli elimu ya shule ya msingi Tanzania imeoza na kunuka kiasi hiki? Bofya hapa ujionee!!!

SENGANITU

Member
Sep 19, 2012
50
15
Baraza la mitihani la tanzania (necta) limeweka utaratibu wa kutoa mtihani wa kufanya mchujo kwa darasa la nne kila mwaka. cha ajabu ni kwamba baraza hilo linatoa copy mojamoja kila wilaya ili zitolewe copy zinazotosha kwa idadi ya watahiniwa wote ndani ya wilaya hizo,kibaya zaidi sana ni pale shule zinapoambiwa kuchangia RIM za karatasi kwa ajili ya photocopy hizo. nimejiuliza maswali machache hapa sijapata majibu yake,hebu nikushirikishe na wewe mwana JF utafakari kidogo!
1.Hivi hapo kuna usiri gani wa mtihani huo wa kitaifa?
2.Ni kweli baraza la mitihani bado lina hadhi kama hapo zamani?
3.Ni kweli nchi imefirisika mpaka inashindwa kutenga fedha kwa ajili ya mitihani hiyo?
4.Baraza linaepusha vipi udanganyifu katika mtihani huo?
Kama hii mitihani haina umuhimu kwanini inaendelea kuwepo?
NASIKITIKA SANA HII ELIMU TUPEWAYO WA TANZANIA!!!
 
Back
Top Bottom