Hivi ni kweli CCM inataka kubaki yenyewe kweli?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Hivi ni kweli CCM inataka kubaki yenyewe kweli?

Inamaana CCM hawaoni faida ya upinzani kabisa?

Mfano upinzani umepunguza hata baadhi ya manyanyaso ya ndani ya CCM yenyewe, kwa kuhofia kuwa ukimnyanyasa mwana CCM atahamia upinzani.

Pili faida nyingine ni ule udhubutu wa wanachama wa upinzani kuikosoa serikali kwa yale mambo ambayo mwanachama wa CCM hawezi kuyasema wakiwa CCM, hivi ni kweli CCM hawajui faida ya upinzanai, wana CCM hawajui faida ya simba kwa yanga?
 
Katika dunia ya leo ushindani katika siasa hauzuiliki hivyo kutengeneza njama za kuua upinzani ni sawa na kuziba tundu la panya kwa mkate kwenye sofa tena sebuleni
 
ccm ndio nini? Mbona alikufa nayo Mwl. Nyerere. Hapa nawaona waigizaji tu ambao wanalindwa na Basata.
 
Mfano mzuri ni leo,yanga imecheza tp mazembe washabili wa simba wamewapa pole wenzao wa yanga kufungwa,hivi ndivyo ccm na vyama vya upinzania uwe
 
Huyo mwenyewe anayejiita rais wa masikini bila nguvu ya upinzani urais angeusikilizia chato anachunga ng'ombe hofu ya upinzani iliwafanya ccm wamteue yeye ili kupunguza nguvu yao, leo kajifanya amesahau.
 
Hilo ndilo kosa la kwanza na kubwa walilo lifanya ccm.
Lakini mm nipo hapa naendelea kuangalia mchezo unaendeje na mwisho wake utakuwa nini.
 
Kwa kweli kaburi la demokrasia linazidi kuchimbwa. Wenye mawazo mgando wanafikri wapinzani wanakwamisha maendeleo, na kudhani kuwa maendeleo yataletwa na ile dhana ya kusifiwa sana, kushaniliwa na kukubaliwa kwa kila hoja wanazoleta kwa asilimia mia moja. Pasi upinzani, na wanajinasibu kwamba hawaoni upungufu wowote kwani akidi inatimia na miswada na bajeti vinajadiliwa na kupitishwa. Mi naamini kuwa mawazo mbadala kutoka upande mwingine so tu yana saidia kufanya marekebisho, Bali pia kuweka hali ya tahadhali na kutenda kwa umakini katika jambo ambalo hapo awali uliona ni thabiti na kamilifu.
 
Back
Top Bottom