Hivi ni kwanini watoto wanapenda kuwa Doctor, Engineer, Pilot, Askari

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,998
5,150
Habari zenu Wakuu!!!!

Niiingie moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu,
Kama umeshawai kuchunguza kwa watoto wanaosoma, ( either ni secondary or primary) ukiwauliza moja baada ya mwingne kuwa, mbele unataka kuja kuwa nan? Wengi majibu yao yanafanana, asilimia kubwa watajib napenda kuwa doctor, engineer, pilot, askar n. k mbali na hapo ni wachache watakaojibu aina nyingine ya kaz wanayotaka kuja kufanya, Hivi ni kwann iko ivo,

NAWASILISHA WAKUU!!!!
 
Mtoto naye anayo akili. Kama wewe ni mhasibu ama mwanasheria lakini kila anapougua unampeleka kwa daktari, na hata gari/Umeme unapokorofisha unaita injinia kwanini asione kuwa wa muhimu ni hao tu!? It is all about security hata kupenda jeshi imo humohumo. Watoto wa kizungu nao wako hivyo lakini wanabadilishwawanabadilishwa na mazingira
 
Siku zote akili ina kawaida ya kuhifadhi kitu unachokisikia ama kukiona mara kwa mara!

Hizo fani zimekuwa zikitajwa sana na kujulikana katika mazingira yetu ya kila siku na watu huambiwa kuwa ni fani zenye fursa kubwa za ajira endapo utazisoma!

Moja ya faida ya mtoto kuzijua fani kama hizi mapema ni kumuongezea jitihada na uwelewa mzuri katika masomo yake hasa hasa yanayoendana na hizo fani!

Lakini pia kuna tatizo linalokuja kutokea katikati ya maisha yao ambapo huwapoteza na kupoteza kabisa muelekeo wa maisha yao kutokana na kushindwa kuyakabili hayo masomo kwa sababu mbalimbali ambazo zinasemwa kila siku!

Ushauri wangu ni kwamba tuwajuze vijana kwamba kuna fani zingine ambazo wanaweza somea ukiachilia hizo!!

Vijana wengi wamekuwa wakipoteza mwelekeo kutokana na kufaham fani chache za kusoma ama kukosa taarifa sahihi ya kipi cha kusoma na kwa matokeo gani na alama zipi!?

Gud day!
 
Mm mwanzo nilipanga nije kuwa doctor ila form four nikazungusha especially science subjects sikukata tamaa nikapenda nije kuwa pastor ila mtaan paliniarb sikufanikiwa nikaona sio ishu ,nikachukua journalism
Duuh wewe hatari uchungaji wito bhna labda ufuate sadala
 
Mmi ni mwalimu vijijini watoto ukiwauliza huku wanakwambi tunataka kuwa walimu huwa nacheka sana nawaambia kazaneni na ufaulu uwepanda kwenye hii fani. Mazingira huchangia sana kufanya utamani au usikitamani kitu.
Nilipokuwa form one kuna jamaa alikuja pale shule madaftar yoke yote yaliandikwa PCM.

Kimbembe kikaanza form two ilimbidi akubaliane na ule mstari wa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ilivyo shida akaenda arts. Wastani form three kwenda form four uliloga aka-robe vipi sijui akaingia form four mock alipata four ya 31 akiwa na D kwenye kiswahili civics somo la dini sijui lile na history mtihani wa taifa alipata division ya vijana.
Kwahiyo maneno si vitendo na si kila ushuzi unaashiria kuwa unataka kukata gogo.

Nawaambiga wanafunzi wangu maisha si mchezo huu ni umande katikati ya baridi kali la asubuhi!!!
 
Hahahaha mkuu we endelea kubak mashamban nitakufikiria uwe mwalimu mkuu
 
Hizo ndiyo kazi wanazoaminishwa kuwa ni bora kuliko zote tokea wapo wadogo...
 
Back
Top Bottom