Hivi ni kwanini Watanzania wanapenda sana kupiga?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,785
Je, sisi ni violent society? Watanzania wanapenda sana kutumia nguvu kutatua tatizo, kila kitu utasikia nitakutandika, hata JF utasikia mtu anakwambia ungekuwa karibu yangu ningekupiga ngumi, kidogo utasikia yule jamaa karibia nimzabe makofi, sasa ni kwa nini? Ni nani anakupa haki ya kumzaba makofi mwingine? Kwa nini hamuwezi kutatua matatizo bila ya kupiga?
Ukimpiga mtu unasikiaje?
 
Wanadamu wanatabia ya kuiga anayewaongoza.

Lkn pia thread hii imejaa tafiti wa uongo.

Kila mtu anapopinga Kuna Wengine wanaunga mkono na kusifia.

Akipinga chadema CCM wanasifia
Akipinga CCM chadema wanasifia
 
Mwingine alisema angepiga ma-shangazi wa wenzake wa huko Lindi.

Sijui haki hio alipewa na nani.

dodge
 
Nilitafsiri kupiga kwa maana ya kukosa uaminifu katika biashara na kupelekea kuiba fedha au mali au kutaka kupata zaidi ya anacholipwa.
Watanzania wengi ni wapigaji kwa defn zote😁😁😁
 
Kupigana ni nature ya viumbe hai sio mwafrika sio mzungu wote tuna tabia za kupigana. Kiasili mamalia wana tabia moja ambayo wanadamu wote pia tukiwa kama mamalia tunayo nayo ni ubabe (survivor of the fittest)
 
Kama hivyo ni kweli basi sisi bado ni animalistic, kwa maana Muzungu hapigani kwanza huwezi kukuta Muzungu wakipigana, watafyatuliana risasi lkn siyo ngumi au sijui kumsaba makofi aliekuudhi labda wale wa lower class kabisa.
 
Ni matokeo ya mifumo iliyokufa, watu hawaamini njia mbadala ya kupata suluhisho,hawaamini polisi wala mahakama ndio utaona kibaka anapigwa hadi kuuawa au polisi anawashambulia kwa risasi na kuwauwa majambazi, na pengine uwezo mdogo wa watu kujieleza na kueleweka na mwisho ukweli mchungu watu wengi hawana imani wamejivika dini wakati roho zao ni za kishetani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, sisi ni violent society? Watanzania wanapenda sana kutumia nguvu kutatua tatizo, kila kitu utasikia nitakutandika, hata JF utasikia mtu anakwambia ungekuwa karibu yangu ningekupiga ngumi, kidogo utasikia yule jamaa karibia nimzabe makofi, sasa ni kwa nini? Ni nani anakupa haki ya kumzaba makofi mwingine? Kwa nini hamuwezi kutatua matatizo bila ya kupiga?
Ukimpiga mtu unasikiaje?
Muulize mwenyekiti wa uvccm hawezii hitubia bila.kuwatisha wapinzani
 
Je, sisi ni violent society? Watanzania wanapenda sana kutumia nguvu kutatua tatizo, kila kitu utasikia nitakutandika, hata JF utasikia mtu anakwambia ungekuwa karibu yangu ningekupiga ngumi, kidogo utasikia yule jamaa karibia nimzabe makofi, sasa ni kwa nini? Ni nani anakupa haki ya kumzaba makofi mwingine? Kwa nini hamuwezi kutatua matatizo bila ya kupiga?
Ukimpiga mtu unasikiaje?
Kwa kufupisha watanzania tunapenda KUJIMWAMBAFAI
 
Mwaka wa kumi huu sijampiga mtu wala sijapigana, ila nafanya mazoezi ya kujilinda kama vile kesho nitapambana. Ikibidi kuzipiga hapo patachimbika.
 
Mama akikasirika ana kupiga na ndala, mfuniko wa ndoo, cha kusukumia chapati, stuli, kuni, mwiko, sufuria, ukija kukua ukawa mkubwa mwenzio akikukosea kidogo una mkunja shati umpe vitasa vyake vya kumtosha
 
Nilitafsiri kupiga kwa maana ya kukosa uaminifu katika biashara na kupelekea kuiba fedha au mali au kutaka kupata zaidi ya anacholipwa.
Watanzania wengi ni wapigaji kwa defn zote😁😁😁
Hahahaa uliwaza mbali mkuu. kweli kupiga ni nature yetu watz.
 
Back
Top Bottom