safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,161
- 15,839
Mkuu naomba tuwasilianee unifahamishe zaidi tafadhali mkuu.
Naweza kuja pm mana nna shida ya kuagiza kitu flani hivi na sijawahi kufanya chochote kile mtandaoni..
Naweza kuja pm mana nna shida ya kuagiza kitu flani hivi na sijawahi kufanya chochote kile mtandaoni..
binafsi nafurahi sana mtu kuogopa kufanya manunuzi mtandaoni kwa sababu sitaki wenye vitu vizuri tuwe wengi town.
Kwa mara ya kwanza nilisoma humu Jf kuhusu kufanya manunuzi mtandaoni, nilisoma thread nyingi na tofauti tofauti ili nipate uelewa kwa kiasi kikubwa.
kwa mara ya kwanza niliagiza vitu aliexpress na vikafika bila shida japokuwa nilichelewa sana, nikarudi tena kusoma thread za JF nikagundua kuwa ni lazima kusoma feedback za wanunuzi wengine ili kujua kama bidhaa ni halisi na ina ubora gani.
Kuna ndugu yangu nilimsaidia kuagiza simu yake ya Samsung ambayo kwa hapa TZ mpya ni laki 7 na vijisent ila kwa nje nilipata kwa laki 2 na ushee buti ni used.
kabla ya mzigo kufika wafanyakazi wenzie walikuwa wanamponda sana kuwa hiyo laki mbili imeibiwa tayari, walimcheka sana kwa mujibu wake alivyoniambia ila baada ya 16 days mzigo ukafika aisee ilikuwa ni kama mpya kabisa + free orijino Chaja, sasa anasema kila mtu ana mtamani na anavyosema kuwa ukitoa yeye na mkurugenzi hakuna mwingine mwenye simu kali kama yake.
Wauzaji wengi wa nje sio waongo kama wa Kupatana.
Mtu nikimwambia kuwa hata ukiiba au mzigo kutofika unarudisha mtonyo wako na asipoamini naachana nae atakuwa anaona wenzie wasukuma tunamiliki vitu vya bei mbaya kumbe tumechukua nje kwa bei kama bure.
MBONA MKIAGIZA MAGARI HAMSEMI KAMA KUNA KUIBIWA?
mfanyabiashara wa Kariakoo anakuuzia simu laki 6 wakati ungezama aliepress, ebay au amazoni ungepata kwa laki 4.
Watanzania tuwe tunajaribu vitu sio kusema eti nitaibiwa na hujawahi hata kujaribu kununua hata mbegu za nyanya aliexpress za Tsh 600/-
WOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO.