Hivi ni kwanini Watanzania ni waoga kufanya manunuzi Mtandaoni?

8ATP

Senior Member
Jul 27, 2017
167
217
Japo kuwa tupo katika 'information age' lakini naona kuna muamuko mdogo sana, hasa wa sisi watanzania kufanya manunuzi mtandaoni. Mimi binafsi nishafanya mara moja kununua bidhaa mtandaoni. Japo kuwa bidhaa ilifika lakini kipindi naisubiri nilipitiwa na mawazo mengi, ikiwemo hofu ya kutapeliwa au kufikishiwa mzigo sio.

Je kwa upande wako ambae umewahi au hujawahi ni nini hofu yako uliyonayo kukufanya usiendelee au usijaribu kununua bidhaa "online".

Karibu kwa mchango wako. Pia wazoefu mnakaribishwa.
 
Kwa kesi ya manunuzi mtandaoni hapo kuna makundi mawili mkuu kundi lakwanza niwauzaji wandani ya nchi wanaopost bidhaa zao ktk mitandao mbali mbali yakijamii ktk hili nami nimeshawahi kufanya manunuzi simara moja wala mbili sasa kuna hili kundi lapili wale akina ebay,Amazon,Aliexpress n.k Kwakweli hawa mimi sijawahi kuagiza japo one day nitajilipua kila nikickia kua mzigo ukifika Tz TRA wanataka cjui % ngap yathamani namzigo hapo ndo najiuliza sasa apa nitakua nimesev kias gani..je ww ulivyoagiza iyo bidhaa kama uliagiza toka nje kwa akina Amazon uliokoa pesa kias gani tofauti nakama ungenunulia tu hapa hapa nchini?
 
Japo kuwa tupo katika 'information age' lakini naona kuna muamuko mdogo sana, hasa wa sisi watanzania kufanya manunuzi mtandaoni. Mimi binafsi nishafanya mara moja kununua bidhaa mtandaoni. Japo kuwa bidhaa ilifika lakini kipindi naisubiri nilipitiwa na mawazo mengi, ikiwemo hofu ya kutapeliwa au kufikishiwa mzigo sio.

Je kwa upande wako ambae umewahi au hujawahi ni nini hofu yako uliyonayo kukufanya usiendelee au usijaribu kununua bidhaa "online".

Karibu kwa mchango wako. Pia wazoefu mnakaribishwa.
Mimi natamani niagizie simu mtandaoni nasikia bei rahisi inaweza kuwa tofauti hata kwa laki 2 na bei ya hapa, sijui kweli ama vipi..

Hofu yangu bhana sijui naanzia wapii tatizo,ila nins imani nikiwa ssiriaz nitajiua pakuanzia..
 
Pakuanzi ni uwe na sanduku la posta au la ofisi unayo fanyia kazi. Pili unakua na app ya mtandao unapenda kununulia bidhaa mf. Aliexpress, kisha unajaza details zako km po box jina sahihi post code, tatu card ya kukuwezesha kufanya manunuzi online km mastercard nk wengi tunatumia mastercard mpesa hapo mpesa watakupa card utakapo hitaji kuitumia utaweka pesa kwenye mpesa kisha utahamisha kutoka mpesa yako kwenda mastercard yako hapo utaweza kuagiza chochote mtandaoni, mf vitu ambavyo Bongo havipo kabisa au pesa ni nyingi basi online ni rahisi mf niulizia kariakoo display ya xiaom redmi 4x nikaambiwa 130k lakini niliagiza kwa 40k tu hapo utajua nili save kiasi gani, bidhaa uhakika ni mkubwa au kuchelewa lakini kufika ni lazima
 
Japo kuwa tupo katika 'information age' lakini naona kuna muamuko mdogo sana, hasa wa sisi watanzania kufanya manunuzi mtandaoni. Mimi binafsi nishafanya mara moja kununua bidhaa mtandaoni. Japo kuwa bidhaa ilifika lakini kipindi naisubiri nilipitiwa na mawazo mengi, ikiwemo hofu ya kutapeliwa au kufikishiwa mzigo sio.

Je kwa upande wako ambae umewahi au hujawahi ni nini hofu yako uliyonayo kukufanya usiendelee au usijaribu kununua bidhaa "online".

Karibu kwa mchango wako. Pia wazoefu mnakaribishwa.
Nadhani kwa sasa bado mfumo wa mtandao hauna security ya kutosha juu ya muamala na
Bado hakuna the right to claim
 
Sawa mkuu, ntaanza na kuagiza kitu kidogo ambacho hata nikitapeliwa nitakuwa na uwezo wa kuwa kawaida pasi na kutembea kichaa na kuomgea mwenyewe njiani
Pakuanzi ni uwe na sanduku la posta au la ofisi unayo fanyia kazi. Pili unakua na app ya mtandao unapenda kununulia bidhaa mf. Aliexpress, kisha unajaza details zako km po box jina sahihi post code, tatu card ya kukuwezesha kufanya manunuzi online km mastercard nk wengi tunatumia mastercard mpesa hapo mpesa watakupa card utakapo hitaji kuitumia utaweka pesa kwenye mpesa kisha utahamisha kutoka mpesa yako kwenda mastercard yako hapo utaweza kuagiza chochote mtandaoni, mf vitu ambavyo Bongo havipo kabisa au pesa ni nyingi basi online ni rahisi mf niulizia kariakoo display ya xiaom redmi 4x nikaambiwa 130k lakini niliagiza kwa 40k tu hapo utajua nili save kiasi gani, bidhaa uhakika ni mkubwa au kuchelewa lakini kufika ni lazima
 
Tatizo ni dhana fulani tumejijengea kwamba online bei ni rahisi, mbongo ukimwambia rahisi basi hapo anajua kwa laki 2 au 3 atapata flagship smartphone, kwa laki 4 au 5 atapata TV inch 42 tena smart toka kwa top brands😂😂😂😂😂.

Akija kwenye hualisia mambo ni tofauti jamani, hata milioni 2 na 3 ni rahisi pia inategemea na bidhaa na price range za bidhaa husika.
 
Japo kuwa tupo katika 'information age' lakini naona kuna muamuko mdogo sana, hasa wa sisi watanzania kufanya manunuzi mtandaoni. Mimi binafsi nishafanya mara moja kununua bidhaa mtandaoni. Japo kuwa bidhaa ilifika lakini kipindi naisubiri nilipitiwa na mawazo mengi, ikiwemo hofu ya kutapeliwa au kufikishiwa mzigo sio.

Je kwa upande wako ambae umewahi au hujawahi ni nini hofu yako uliyonayo kukufanya usiendelee au usijaribu kununua bidhaa "online".

Karibu kwa mchango wako. Pia wazoefu mnakaribishwa.
Mimi kwa Mara ya kwanza kununua bidhaa nilianzia humu jamii forums kutoka kwa member mmoja anaitwa Stable George yeye tuliingia mkataba wa kuniuzia vitabu ambapo aliniuzia vitabu Vingi kwa softcopy na alinitumia kwa email yangu Ila kwa nje ya nchi bado sijawahi kununua na hasa shida IPO kwenye hii kitu credit card/debit visa yaani hapa huwa nahisi nikijaribu tu hackers wanaweza kuchukua mpunga wote .Pia usalama wa mzigo ninaonunua upo wapi maana mikataba tunayiingia ndani ya nchi tu changamoto kibao hutokea sijui hii ya nje hali ikitokea mzigo hujafika itakuaje. Kwa yeyote ambaye amewahi Fanya manunuzi makubwa na madogo labda kununua software au bidhaa kama kwenye maduka ya Amazon nk. naomba utupatie udhohefu wako na utufundishe namna SALAMA ya kufanya manunuzi na ikitokea changamoto ya mzigo kutofika naanzia wapi ili kupata haki yangu.
 
Japo kuwa tupo katika 'information age' lakini naona kuna muamuko mdogo sana, hasa wa sisi watanzania kufanya manunuzi mtandaoni. Mimi binafsi nishafanya mara moja kununua bidhaa mtandaoni. Japo kuwa bidhaa ilifika lakini kipindi naisubiri nilipitiwa na mawazo mengi, ikiwemo hofu ya kutapeliwa au kufikishiwa mzigo sio.

Je kwa upande wako ambae umewahi au hujawahi ni nini hofu yako uliyonayo kukufanya usiendelee au usijaribu kununua bidhaa "online".

Karibu kwa mchango wako. Pia wazoefu mnakaribishwa.
Nishamefanya ununuzi wa bidhaa mbali mbali kutoka kwenye mtandao lakini nikiwa nchi tofauti na Tanzania. Nimewahi kununua vioo vya simu kwa ajili ya simu zilizovunjika, covers za simu, miwani, nguo, vifaa vidogo vidogo vya electronics nk. Mitandao nayotumia zaidi ni eBay na Facebook. Facebook ya Tanzania bado hawana section ya kuuza na kununua vitu ila nchi nyingine eg Ulaya wana section ya namna hiyo na watu huuza na kununua vitu vingi mno. Nikiwa nje ya nchi huwa napenda kuitumia Facebook kwani mara nyingi ukiona bidhaa mnakubaliana na mnunuzi kukutana ana kwa ana na kuuziana. eBay unaagiza kitu kutokana na picha yake ila vilevile wauzaji wengi wanaaminika. Changamoto kubwa ya kununua vitu kwenye mitandao kwangu mimi ni kuwa unanunua kitu kutokana na picha na maelezo unayoona hivyo kuna changamoto kubwa kwenye kununua bidhaa nyingi i.e. hujui exactly kikoje na quality yake ikoje.
 
Japo kuwa tupo katika 'information age' lakini naona kuna muamuko mdogo sana, hasa wa sisi watanzania kufanya manunuzi mtandaoni. Mimi binafsi nishafanya mara moja kununua bidhaa mtandaoni. Japo kuwa bidhaa ilifika lakini kipindi naisubiri nilipitiwa na mawazo mengi, ikiwemo hofu ya kutapeliwa au kufikishiwa mzigo sio.

Je kwa upande wako ambae umewahi au hujawahi ni nini hofu yako uliyonayo kukufanya usiendelee au usijaribu kununua bidhaa "online".

Karibu kwa mchango wako. Pia wazoefu mnakaribishwa.
Bro Kodi..... idara ya makadirio TRA.... 😂
 
binafsi nafurahi sana mtu kuogopa kufanya manunuzi mtandaoni kwa sababu sitaki wenye vitu vizuri tuwe wengi town.

Kwa mara ya kwanza nilisoma humu Jf kuhusu kufanya manunuzi mtandaoni, nilisoma thread nyingi na tofauti tofauti ili nipate uelewa kwa kiasi kikubwa.

kwa mara ya kwanza niliagiza vitu aliexpress na vikafika bila shida japokuwa nilichelewa sana, nikarudi tena kusoma thread za JF nikagundua kuwa ni lazima kusoma feedback za wanunuzi wengine ili kujua kama bidhaa ni halisi na ina ubora gani.

Kuna ndugu yangu nilimsaidia kuagiza simu yake ya Samsung ambayo kwa hapa TZ mpya ni laki 7 na vijisent ila kwa nje nilipata kwa laki 2 na ushee buti ni used.

kabla ya mzigo kufika wafanyakazi wenzie walikuwa wanamponda sana kuwa hiyo laki mbili imeibiwa tayari, walimcheka sana kwa mujibu wake alivyoniambia ila baada ya 16 days mzigo ukafika aisee ilikuwa ni kama mpya kabisa + free orijino Chaja, sasa anasema kila mtu ana mtamani na anavyosema kuwa ukitoa yeye na mkurugenzi hakuna mwingine mwenye simu kali kama yake.

Wauzaji wengi wa nje sio waongo kama wa Kupatana.

Mtu nikimwambia kuwa hata ukiiba au mzigo kutofika unarudisha mtonyo wako na asipoamini naachana nae atakuwa anaona wenzie wasukuma tunamiliki vitu vya bei mbaya kumbe tumechukua nje kwa bei kama bure.

MBONA MKIAGIZA MAGARI HAMSEMI KAMA KUNA KUIBIWA?

mfanyabiashara wa Kariakoo anakuuzia simu laki 6 wakati ungezama aliepress, ebay au amazoni ungepata kwa laki 4.

Watanzania tuwe tunajaribu vitu sio kusema eti nitaibiwa na hujawahi hata kujaribu kununua hata mbegu za nyanya aliexpress za Tsh 600/-

WOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO.
 
Dah, yaani mimi mtandaoni ndo kama nyumbani. Vitu vingi nanunua na kuagiza mtandaoni.

Nimesha zoea na wala sina wasiwasi. Kikubwa ni kujua kanuni kuu za kununua mtandaoni. Kubwa kuliko yote, unanunua mtandao gani.

Mitandao kama ebay na amazon wanatumia mfumo unaitwa Escrow. Sawa na mtandao kama wa www.ajiras.com wa bongo unaotumia.

Kwa kifupi, hela yako inakuwa secured mpaka upokee mzigo wako. Bila hivyo, muuzaji atatuma tena au utarudishiwa hela yako.
 
Pakuanzi ni uwe na sanduku la posta au la ofisi unayo fanyia kazi. Pili unakua na app ya mtandao unapenda kununulia bidhaa mf. Aliexpress, kisha unajaza details zako km po box jina sahihi post code, tatu card ya kukuwezesha kufanya manunuzi online km mastercard nk wengi tunatumia mastercard mpesa hapo mpesa watakupa card utakapo hitaji kuitumia utaweka pesa kwenye mpesa kisha utahamisha kutoka mpesa yako kwenda mastercard yako hapo utaweza kuagiza chochote mtandaoni, mf vitu ambavyo Bongo havipo kabisa au pesa ni nyingi basi online ni rahisi mf niulizia kariakoo display ya xiaom redmi 4x nikaambiwa 130k lakini niliagiza kwa 40k tu hapo utajua nili save kiasi gani, bidhaa uhakika ni mkubwa au kuchelewa lakini kufika ni lazima
Mpesa gharama ni bei wanacharge. Mfano, Equity bank wanacharge kama 8% hivi. Yaani bei halisi ya bidhaa + 8%, sijui bank zingine wanafanyaje na kama wasiochaji nitafurahi kuwafahamu
 
Back
Top Bottom