Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005, ibara ya 3(1) inaanisha kuwa nchi yetu itakuwa ya kidemokrasia yenye mfumo wa vyama vingi
Ingawa Katiba yetu inabainisha hivyo, kiutendaji ni kama nchi yetu ipo kwenye mfumo wa chama kimoja
Nitaorodhesha hapa sababu zangu zenye ushahidi wa mazingira kuoyesha uhalisia wa hoja yangu
1. Kwenye chaguzi ndogo zilizopita chama cha CCM kiliibuka na ushindi wa asilimia 100, tena kwenye kata 30 kati ya kata 77 walizogombea madiwani, CCM walitangazwa washindi bila kupingwa kwa sababu ambazo nyingine hazina mashiko kuwa eti miongoni ya wagombea wa upinzani walibainika kuwa siyo raia halali wa nchi hii!
2. Mkuu wa nchi kuwatangazia wateule wake kuwa hakuna kuwa "nyutro" katika Utendaji wao kwa kuwa wanalazimika kutekeleza ilani za Chama cha Mapinduzi!
3. Tulimsikia pia Jiwe akiwaagiza wateule wake maDED katika moja ya hotuba zake akiwaambia kuwa "Nimekuteua wewe ninakupa gari nzuri ya kutembelea na mshahara mnono na marupurupu na nyumba nzuri ya kuishi, halafu nisikie umemtangaza mgombea wa upinzani kuwa ameshinda..........." Mwisho wa kunukuu
4. Pale yanapotangazwa matokeo ya chaguzi hizo huwa tunaona maaskari wengi tu wa Jeshi la Polisi wenye silaha za moto. Hivi kwenye chaguzi huru na haki, kuna haja gani ya kutangaza matokeo huku kuna magari mengi ya washawasha??
5 Tulimsikia aliyekuwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, akiutangazia Umma wa watanzania kuwa ataomba msamaha kwa Mkuu wa nchi eti kwa sababu kwenye kata yake moja kushinda mgombea wa chama cha upinzani!
Anawezaje kuomba msamaha kwa Rais kwa kushindwa uchaguzi kwenye nchi inayoendeshwa kwenye mfumo wa vyama vingi??
Je kosa lake hapo ni lipi kama siyo Rais huyo "kuwaagiza" wakuu hao wa mikoa kuwa ni lazima CCM ishinde kwa asilimia 100??
Mkuu huyo wa Mkoa hata hivyo katika mabadikiko yaliyotokea hivi karibuni ameondolewa kwenye Mkoa huo!
Huo ni ushahidi wa mazingira kuwa nchi yetu ingawa kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, lakini kiuhalisiia ni kama inaendeshwa kwa mfumo wa chama kimoja