Hivi ni kwanini wanaowaambia wenzao wajiajiri wao wameajiriwa?

huu ni uwendawazimu wa kifikra...wanadhania kujiajiri ni kazi ndogo halafu sijui wanaposema ujiajiri sijui katika kitu gani labda ndio tatizo lao lipo hapo...maana any ajira binafsi inataka capital ya kuanzisha sasa mtu katoka chuo iyo ela ya capital atapata wapi sasa...tuangalie cha kupost au kureply sio unaongea tuu jiajiri wakati hata kwako hauna fridge la kuuza ice cream...

mtaji mkubwa nadhani unapaswa kuwa fikira madhubuti na uweza wa kuchukua maamuzi magumu. Naamini ukiwa na fikra na mipango sahihi na uwezo wa kudhubutu-mtaji kwa maana ya pesa si tatizo.
 
We hujawahi kuona mzinzi namba moja anafundisha kwenye semina ya ukimwi jinsi ya kuacha kabisa ngono kama njia ya kuepuka maambukizi?Au mzazi anamwonya mwanae wa kiume eti ajizuie kufanya ngono hadi siku atakapooa?!kitu ambacho hakiwezekani kabisa!!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
jamani inafurahisha sana mjadala huu,kiukweli lawama kwa serikali hazikwepeki,inahitaji kulaumiwa sana tena mno,kwani wao ndio wamlipewa dhamana ya kuwatafutia maisha bora watanzania,badala yake wao wanafanya yakwao,hawaumizi vichwa juu ya jinsi gani kuongeza ufanisi na kupanua sekta ya viwanda na kilimo na nyingine kama hizo,wamepauka mawazo,wanatakiwa warudi darasani, nchi hii kila kitu siasa,siasa,siasa......... acheni ujanja ujanja jamani...kujiajiri sawa lakini kuna msingi wa kujiajiri ulio live? hatuna institutions imara za kufundisha watu misingi hiyo,watu wanapenda kulukia juu juu sana, nani kakwambia kuwa elimu ya Tanzania inawatengeneza watu kuwa wajasiriamali? elimu yetu inatuandaa kufanya kazi maofisini,mpaka kesho,hivi siasa ilianzisha mabilioni ya JK? mnayakumbuka? hivi yako wapi na nani amefaidi? tunahitaji elimu ya ujasiriamali sasa kuanzia sec to university lakini tuache siasa za kudanganya watu,siasa inataka ujiajili wakati hakuna mazingira hayo,unahitaji kujiandaa kisaikolojia vinginevyo itakuwa kama mabilioni ya JK.............SIPENDI UNAFIKI KWENYE UKWELI.
 
Hili swali nilishawahi kujiuliza sana kabla. Wanasiasa ndiyo watu wakwanza kusisitiza watu wajiajiri wakati yeye anazeekea kwenye ajira. Ni wanafiki wakubwa
 
Inategemea unamwongelea mtu wa level gani ya elimu. Tatitizo la ajira maana yake nini? Mtu wa chuo akitaka kujiajiri lazima mtaji uwe mkubwa kidogo ukilinganisha na darasa la saba hata kama wote wanamawazo sawa ya fursa. Kazi zingne za kujiajiri ni za kipuzi sana tusishushe sana elimu ya kibongo hata kama haiwafanye vijana kujiajiri.
Hawa ndio dizaini ya watu ambao mtoa mada anajaribu kuwatetea.
wanafunzi wa vyuo wa siku hizi mnajidanganya sana.
 
Nayachukia sana majitu yanayoleta mada za kujiajiri humu ndani.

Mungu hapendi kuwachukia wenzako. kumbuka wengine wamejaliwa kuhamasisha watu na pia kujiajiri ni kuzuri kama utakuwa serious na huo mchakato kwani kuajiriwa mara nyingi ni kutimiza ndoto za bossi wako wakati huohuo za kwako hazitimii kwa zaidi ya asilimia 75. Wangu mtizamo
 
TUTAACHA LINI HUU UNAFIKI WATANZANIA! Inasikitisha sana hapa tz kwetu, wanaotoa elimu ya ujasiria mali yeye mwenyewe kaajiriwa na ni mwoga hata kusikia neno JIAJIRI, AU HAKUNA AJIRA WAKATI YEYE ANAYO!

Tukubali kitu kimoja ni kwamba sisi watanzania ni wanafiki sana na utakuta jitu linazungumzia kujiajiri wakati lenyewe hata watoto wake anawatafutia ajira.
TUTAACHA LINI HUU UNAFIKI WATANZANIA?!!

Uko sawa boss na mara nyingi kwa maisha yetu ya kiafrika lazima uajiliwe kwanza ili utafute mtaji ndo baadae ujiajir waache unafik wa kudanganya watu
 
Tumesha kuwa jamii ya kulalama tu kulalama tu. Mtu badala ya kukuna kichwa kutafuta solutions ana kazania kulalamika tu kuhusu tatizo kana kwamba kulalamika ndio kutatatua tatizo. Sisi sio nchi masikini na changa ya kwanza. Hata hao walioendelea walisha pitia hatua kama hizi sema waka tafuta suluhisho.

Ushauri wangu kwa watu. Ukipenda kulalamika sana huta kuja kuendelea. Utailalamikia serikali, utaya lalamikia mazingira na mwisho wa siku unaweza jikuta una lalamikia wazazi wako au ndugu zako wenye maendeleo. Life is not fair. Kubali hali halisi na tafuta jinsi ya kujikomboa iwe kwa kuajiriwa au kwa kujiajiri.

Wengi tunacho jidanganya ni kwamba kuanzisha biashara ni mpaka uwe na mtaji mkubwa. Tatizo la graduates wengi wanakua wanadharau baadhi ya kazi au biashara. Wanajiona kwa vile wamesoma basi lazima waazie level fulani ya juu. Acha kujisikia. Kama huja toka kwenye familia yenye uwezo wa kukupa mtaji mkubwa au unaoweza kukutafutia kazi kirahisi jua huna tofauti na huyo asie na elimu unaemdharau. Kama kweli elimu yako si ya kuungaunga na kukaririsha unaweza ukatumia elimu yako kutoka.

Mwisho wa siku kama hautaki basi endelea kulalamika Yesu ataja rudi na kujibu maombi yenu. Ila mkubali kuwa angalia wenzenu walio anza kidogo kidogo wakiendelea mwaka hadi mwaka. Sasa wewe unae tafuta kazi miaka miwili na mwenzio ambae kaanza kimradi kidogo na sasa kabiashara kake kana miaka miwili sijui nani nafuu.
 
Uko sawa boss na mara nyingi kwa maisha yetu ya kiafrika lazima uajiliwe kwanza ili utafute mtaji ndo baadae ujiajir waache unafik wa kudanganya watu

Kuna njia nyingi za kupata mtaji wa kujiajiri. Ungekua mtu wa kukuna kichwa na kufikiria ungezijua hizo fursa.
 
Hatuta fikia hitimisho kwenye hili...ila niseme ivi..ujinga kukataa ushauri wa kujiajiri kisa alioutoa ni mhajiriwa.

Kweli mkuu. Tatizo Watanzania tumezoea ulalamishi. Siku zote kwetu sisi mbaya ni mtu mwingine au anaesababisha umasikini wangu ni mtu mwingine. Ndio maana nchi hii hamna linalo tatuliwa kwa sababu kila mtu ni kulalama tu na kulialia.
 
Acha ujinga wewe yani mtu kamaliza degree aende kuuza mitumba,alafu hao utakaowakuta wanasoma hiyo degree unawapa ujumbe gani,kabla hujawambia wenzako hebu kuwa na experience na ukisemacho wewe umewai kuuza mitumba? Tatizo nchi hii imejaa ubinafsi viongozi wao ni kuongea tu hawaweki mifumo mizuri kuwapatia vijana ajira au kujiajiri na ukumbuke sio kila mtu ana kipaji cha kujiajiri,bora hata hizo field za wanafunzi zingekuwa zinapatikana na kuwafundisha wanafunzi kiuhakika labda ingesaidia watu kujiaji,kama mtu wa degree hata diploma aende akauze mitumba basi hakuna haja ya kuweka vyuo,watu wanasoma ili wakauze mitumba au kuuza genge kweli unaweza kutoa ushahuri huo,acha siasa za kijinga bana@ MwanaFalsafa
 
Hivi kuna mahali nimesema aende akauze mitumba? Mtu ukijisifia na elimu unashindwa kuwa mbunifu? Umesha wahi sikia miradi ya kuku? Mboga mboga je? Tatizo hamjifikirishii ndio maana ukakimbilia kutaja kuuza mitumba wakati sina nilipo sema wasomi wakauze mitumba.
 
kweli mkuu. Tatizo watanzania tumezoea ulalamishi. Siku zote kwetu sisi mbaya ni mtu mwingine au anaesababisha umasikini wangu ni mtu mwingine. Ndio maana nchi hii hamna linalo tatuliwa kwa sababu kila mtu ni kulalama tu na kulialia.

walioshiba hao bwana
 
Acha ujinga wewe yani mtu kamaliza degree aende kuuza mitumba,alafu hao utakaowakuta wanasoma hiyo degree unawapa ujumbe gani,kabla hujawambia wenzako hebu kuwa na experience na ukisemacho wewe umewai kuuza mitumba? Tatizo nchi hii imejaa ubinafsi viongozi wao ni kuongea tu hawaweki mifumo mizuri kuwapatia vijana ajira au kujiajiri na ukumbuke sio kila mtu ana kipaji cha kujiajiri,bora hata hizo field za wanafunzi zingekuwa zinapatikana na kuwafundisha wanafunzi kiuhakika labda ingesaidia watu kujiaji,kama mtu wa degree hata diploma aende akauze mitumba basi hakuna haja ya kuweka vyuo,watu wanasoma ili wakauze mitumba au kuuza genge kweli unaweza kutoa ushahuri huo,acha siasa za kijinga bana@ MwanaFalsafa
Wewe kama umesoma, bado haujaelimika. go back to school.
 
Huu ni uwendawazimu wa kifikra...wanadhania kujiajiri ni kazi ndogo halafu sijui wanaposema ujiajiri sijui katika kitu gani labda ndio tatizo lao lipo hapo...maana any ajira binafsi inataka Capital ya kuanzisha sasa mtu katoka chuo iyo ela ya Capital atapata wapi sasa...tuangalie cha kupost au kureply sio unaongea tuu jiajiri wakati hata kwako hauna fridge la kuuza Ice cream...

Kilimo kwanza ndio mkombozi wa vijana wasio na kazi
 
Kujiajiri muhimu maaana kazi kupata yaweza kukuchukua miaka mingi hivyo unajituma tu mtaji utapata au mnaunda kikundi na kwenda kukopa hela kama kikundi na kujiendeleza
 
Hivi kuna mahali nimesema aende akauze mitumba? Mtu ukijisifia na elimu unashindwa kuwa mbunifu? Umesha wahi sikia miradi ya kuku? Mboga mboga je? Tatizo hamjifikirishii ndio maana ukakimbilia kutaja kuuza mitumba wakati sina nilipo sema wasomi wakauze mitumba.

Hukusema sawa,ila hicho ndicho unacho maanisha...graduate fresh from college hana experience na hivyo viujasiriamali vyako vya kufuga kuku leo avamie tu kazi za watu..think twice!
 
Hukusema sawa,ila hicho ndicho unacho maanisha...graduate fresh from college hana experience na hivyo viujasiriamali vyako vya kufuga kuku leo avamie tu kazi za watu..think twice!

Acha kuwa mbishi. Sicho nilicho maanisha. Hata huko kazini unapo kwenda huna experience napo seti? Si unaenda kufundishwa seti? Sasa nikupe mfano.

Pia huko kudharau na kudai "viujasiriamali vya kuuza kuku" kwa taarifa yako biashara ya kuku ndio one of the most profitable. Kifaranga kimoja ni shilingi elfu moja. Hiko kifaranga kikija kukua na kuwa kuku kamili anakua na thamani ya shilingi elfu 20 mpaka elfu 25. Waulize wenzako wanaofuga kuku sio kudharau na kusema "viujasiriamali vya kuku" wakati kuna watu wana fuga kuku na wanaingiza pesa kuliko huyo wa ofisini. Tatizo lenu watu kama nyie ni dharau.

Cha pili. Kama umefuatilia mjadala na post zangu tokea mwanzo nilisha sema sina pingamizi na mtu kuajiriwa. Kuajiriwa na kujiajiri zote ni njia za kujipatia kipato. Nikasema mtu ambae ana taka kazi lakini ana kaa miaka kadhaa hapati kazi si vibaya kufikiria kujiajiri. Ila kama wewe unamshauri mtu akae miaka miwili mitatu ana ngojea kuajiriwa tu sawa.
 
Back
Top Bottom