Hivi ni kwanini wacheza kareti wengi Bongo wako rafu, wanavuta bhangi, hawana maisha, ni vijana ambao wapo wapo tu?

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,630
5,135
Nimecheza michezo ya martial arts shorinji karate kuanzia nipo High school Kibaha sec. Hapa nilikuwa nakutana na vijana wengi walio hatua mbalimbali umahili wa michezo ya karate ila wengi wao ni jobless na wanavuta sana bhangi.

Nikiwa likizo nyumbani bado nilitembelea dojo mbali mbali na kukutana na vijana wengi wajuzi wa huu mchezo. Ila wengi wao vile vile hawana future kimaisha .

Wengi walikuwa wenyeji wazuri wa mahabusu za polis na kupiga mizinga wakiona mtu wanayefahamiana.

Nimecheza martial art hadi chuo kikuu ambapo baadaye nilipunguza kasi nasasa nimeacha kabisa. Nikiwa university Moro hapa kuna kijana alikua mahili sana wa goju ryu karate akiitwa Badu. Tatizo lake lilikua bhangi na alikua jobless na sasa amekua chizi.

Kuna mifano mingine mingi ya aina hiyo..hivi nikwanini hasa ? Huu mchezo wa karate una laana gani. DSM, arusha na mikoa mingine yenye uharifu sana wacheza karate wengi ni vibaka pia na wanapiga ngumi usisubiri.
 
Nina miaka 30 vp naweza kujiunga angalau kupata ujuzi kidogo wa kujihami nikivamiwa kizembe??
 
Wameanza kubadilika siku hizi.Walikuwa wakiona filamu za Kichina na Wachina walivyoishi miaka ya 60-80 mwanzoni wakadhani ndiyo hivyo.Ugumu-ugumu.Snake in the eagles shadow!😝😝😝😝😝
 
Nina miaka 30 vp naweza kujiunga angalau kupata ujuzi kidogo wa kujihami nikivamiwa kizembe??
Boss huu mchezo unahita hobby . kama unaupenda toka moyoni utauweza maana mazoezi yake ni magumu sana.
 
Hawa ndio waleee waliokuwa wanahisi hip pop ni ugomvi akina sister p, na z b , wakawa wanaiga maisha ya akina 2pak mwishowe wakapotea
 
Ni kweli wengi huwa wanasahau kuwa Kuna kutafta maisha..unaowasemea wew ni wale waliotaka kubobea haswa kwenye hio michezo uku wakisahau uchumi..Ila tuliocheza kipindi tuko skuli na vyuo Haina athari sana kiuchumi
 
Si hata ushukuru wameamua kujishughulisha na kitu kiliko kukaa kijiweni na kukaba watu ? Hii nchi haina programu yoyote kwa vijana wake, ndo maana boda boda au bongo flava au kukaba.
 
Back
Top Bottom