Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Nimekua humu kwa kipindi kidogo lakini hili la kuitana mkuu limekuja tuu sjui kwa nini wakuu?

Mkuu pole sana kwa kuwa ndio mara yako ya kwanza kusikia hili neno '' MKUU'' ki ukweli mimi ni mmoja wapo wa watu wanaopenda kulitumia neno MKUU kwanza linarahisisha mawasiliano mathalani unaenda ofisi fulani afu hujui huyo mtu ana cheo gani....basi ili upate urahisi wa kuongea naye unatumia neno mkuu....'' mfano habari ya saahizi mkuu?'' naye atakujibu kwa uungwana salam ndugu yangu.....Kwa kifupi ndo mambo kama hayo mkuu.
 
Mkuu mdeki, hili neno mkuu umelikuta, hata mimi nimelikuta

Hebu pendekeza tutumie neno gani, mkuu!

Nimekua humu kwa kipindi kidogo lakini hili la kuitana mkuu limekuja tuu sjui kwa nini wakuu?
 
Nimekua humu kwa kipindi kidogo lakini hili la kuitana mkuu limekuja tuu sjui kwa nini wakuu?

Ni namna fulani ya kuonesha HESHIMA kwa mtu unayemjibu au kumrefer! Unaweza pia kusema "Sir"..lakini kwa kuwa sisi ni Watanzania na tunajivunia kiswahili, na kwa kuwa pia wengi hatufahamiani jinsia wala umri inatuwia rahisi kutumia jina "Mkuu". Umenielewa Mkuu?
Asante sana.
 
Mimi naona inatokana na MOTTO(SLOGAN) wa JF, "THE HOME OF GREAT THINKERS". Kwa hiyo ukishakuwa mwanachama wa JF Unastahili kuitwa ''MKUU" ili kuwekeana heshima. Ni mtazamo wangu tu 'Wakuu'.
 
Huku kwetu Arusha ukishakua na viJisenti tunaitana VIFARU au KIFARU!

. . . . . Mkuu Ndallo mimi ndiye muhanga wa jina hilo la KIFARU. Daily marafiki mananiita hivyo mpaka nachukia kuitwa jina la aina ya mnyama.
 
Last edited by a moderator:
Kwakuwa wanao takiwa kuwa wakuu magamba hawatendi kama wakuu bora sisi humu tuwe wakuu kwani tunaweza kuyafanya yaliyo washinda wakuu si ndio mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom