Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Nimekua humu kwa kipindi kidogo lakini hili la kuitana mkuu limekuja tuu sjui kwa nini wakuu?

Hutegemea ;

1. Heshima: Watu hapa JF ni wa kila rika, na laiti ingekuwa tunaweka umri halisi ingekuwa shida sana katika kuchangia baadhi ya mada, mfano mtu mzima kuongea vitu vya kipuuzi na pengine mtoto/kijana kudharaulika hata kwa michango yake (kwa sababu tu ya Umri wake).Hivyo kwa kutumia neno "Mkuu" bado kunalinda heshima fulani.

2. Mazoea/Mtindo: Kama vile maneno 'mshkaji', 'mheshimiwa'
n.k yanavyopokelewa kwenye jamii, neno 'Mkuu' limepokelewa
hivyo hivyo hasa katika jamii ya JF.

Hivyo, kulinda heshima kunabaki sababu ya msingi, ingawaje kunaweza kuwa na sababu nyinginezo.
 
binafsi naitumia mkuu kuzuia offence kwa watu...kwa sababu hatujuani umri na jinsia naamua kulitumia mkuu kumtaja mtu..ndo hivo mkuu

Hata mimi ndiyo maana nalitumia, kwasababu linaweza kutumika kwa jinsia yoyote na umri wowote.
 
Ni heshima iliyojengeka hapa JF tokea ikiitwa Jambo.
Ni ishara ya heshima kwa kuwa wakati huo watu hawakuwa wakitukanana, bali nguvu ya hoja ndio ilitawala.
Ukiachana na hilo ili kuepisha mkanganyiko wa jinsia baina ya wanachama, neno mkuu limekua mbadala wa kaka, dada, baba, mama n.k.

Nimekua humu kwa kipindi kidogo lakini hili la kuitana mkuu limekuja tuu sjui kwa nini wakuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom