Hivi ni kwanini tukio la KPG halijaandikwa kwenye vitabu vitakatifu?!

kwa kifupi:
yote ni sahihi yalitukia.
Kila moja lilitukia kwa wakati wake.
Binadamu wale wa olduvai,mungu aliamua kuwafutilia mbali... Pamoja na mijusi mikubwa ''dinno'' na viumbe wengine wa ajabu.
Ndipo akaipanga dunia upya na kumuweka adam na ubavu wake kama ''mfano'' wa bin adamu wengine sehemu mbalimbali za dunia.

kwa ushahidi upi?
 
Takriban miaka million 55 iliyopita kulitokea tukio la kimaafa linalojulikana Kama KPG impact ambapo jiwe kubwa lenye upana Wa mamia ya maili lilianguka na kuleta madhara sawa na mabomu laki moja ya nuclear ambapo asilimia 99 ya viumbe vote duniani vilitoweka.

Tukio hili limekuwa proven beyond doubt. Je biblia haikuona umuhimu Wa kubainisha hili kinagaubaga?!

Kwa maelezo zaidi Cretaceous–Paleogene extinction event - Wikipedia, the free encyclopedia

Hii miaka wameipataje ??
kwa nini uiamini ??
kwa nini uamini KPG ilitokea ??
na kwa nini unataka iandikwe kwenye biblia ??
 
kwani kwenye quruan ipo ? na kwa nn wale nyani - watu hawakuandikwa ktk vitabu vya dini ?
inategemea mawazo yko yalipo
 
Hii miaka wameipataje ??
kwa nini uiamini ??
kwa nini uamini KPG ilitokea ??
na kwa nini unataka iandikwe kwenye biblia ??
Nenda kasome methods of scientific dating. Hayo maswali mengine jijibu mwenyewe!
 
Takriban miaka million 55 iliyopita kulitokea tukio la kimaafa linalojulikana Kama KPG impact ambapo jiwe kubwa lenye upana Wa mamia ya maili lilianguka na kuleta madhara sawa na mabomu laki moja ya nuclear ambapo asilimia 99 ya viumbe vote duniani vilitoweka.

Tukio hili limekuwa proven beyond doubt. Je biblia haikuona umuhimu Wa kubainisha hili kinagaubaga?!

Kwa maelezo zaidi Cretaceous–Paleogene extinction event - Wikipedia, the free encyclopedia

We jamaa swala la uwepo wa mungu bado linakusumbua tu hadi leo?
 
Me nachojua dunia ina miaka 2014 soon baada ya siku kadhaa itakuwa na miaka 2015. Hayo mengine ya Carbon 15 hata siyajui
 
hii kitu haipo wikipedia as an authority..,bali ipo pale kusambaza knowledge. hii imekuwa recorded kwenye papers na journals za kila aina. legeza ubongo.

Brother acha ushamba, vitu vingine uwe unafikiria kabla hujaleta humu. Sio lazima uweke bandiko kama huna cha kubandika.
 
Ndugu.., nani kakwambia dunia ina miaka million 55, our Eath is about 4 billion years old!

Naona unanichanganya tu, kwenye bandiko unasema kuna tukio lilitokea miaka million 55 iliyopita, hili tukio la KPG lilitokea wapi kama hapa unasema dunia yetu ina umri wa million 4!!!!!? Sasa kama unaamini dunia yetu ina umri wa miaka million 4 kwa nini uamini tena kuna tukio KPG lilitokea miaka million 55 iliyopita, je tukio hili lilitokea kwenye dunia hii hii au unamaanisha dunia nyingine
 
Brother acha ushamba, vitu vingine uwe unafikiria kabla hujaleta humu. Sio lazima uweke bandiko kama huna cha kubandika.
Mi hata namshangaa jinsi anavyojichanganya sijui kakurupukia wapi, analeta vitu visivyokuwa na fact yoyote humu
 
Naona unanichanganya tu, kwenye bandiko unasema kuna tukio lilitokea miaka million 55 iliyopita, hili tukio la KPG lilitokea wapi kama hapa unasema dunia yetu ina umri wa million 4!!!!!? Sasa kama unaamini dunia yetu ina umri wa miaka million 4 kwa nini uamini tena kuna tukio KPG lilitokea miaka million 55 iliyopita, je tukio hili lilitokea kwenye dunia hii hii au unamaanisha dunia nyingine
Acha kujibu kwa kukurupuka unajiaibisha bure.., soma vizuri.., nimesema 4 BILLION NA SIO MILLION!
 
Back
Top Bottom