Hivi ni kwanini ttcl wako so conservative and old fashioned? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kwanini ttcl wako so conservative and old fashioned?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by tototundu, Sep 9, 2010.

 1. tototundu

  tototundu Senior Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilisoma comment ya mdau mmoja humu forum akielezea uzuri wa TTCL.

  Mimi nina maoni tofauti, ambayo huwa yananipa mawazo sana.

  Kwanini nasema hivi, Kwannza hawako business oriented, kuna vitu vingine makampuni yaliyozaliwa juzi yameshafanya automation long ago. Eti mtu ukitaka kuhama bundle let say 500Mb kwenda 2GB lazima uandike barua! Barua? Karne ya 22!
  Licha ya kuandika barua huo uhamisho lazima fundi afanye manually ofisini, tena mpaka aombwe na customer care, TTCL, are you serious?

  Hilo la kwanza, la pili ni ile kutowajali na kutowachangamkia wateja wadogo. Ni TTCL tu ndio ambao hawana small bundles kama 15Mb, 20 MB etc hata kama ni per day plan, hivi TTCl hakuna department ya marketing ama research?

  Mimi naamini TTCL ndio watu wenye best platform ya communication hapa TZ especially Internet, lakini watu waliopo pengine hawana vision, au wamepitwa na wakati, au pengine TTCL bado inaendeshwa kiserikali serikali....
   
 2. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Sikujua kama mbaka uandike barua hapo ni usumbufu usio wa lazima , nilitaka kuhama ya TTCL ambayo ni unlimites niende ya bundle ya 8GB ,wanada ina speed nzuri zaidi ya hizi za unlimited , ila nimeamua kurudi Sasatel, niliweka hiyo ya 120,000 unlimited ya TTCL , bado speed siwezi kuangalia videoz kwa speed nzuri.Sasatel wana Unlimited connection ila iko bei juu Sh 240,000. speed yano ni kubwa.
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Niliwai pia kuandika thread moja nikijiuliza hivi TTC Inahujumiwa na watu maksudi ili makampuni binafsi yapate wateja au TTCL inakosa watendaji wanaojuakuendesha mambo kitaalamu.

  Kweli TTCL wana infastructure amabzo wao ndo wanatakiwa kuwa ISP provider mkubwa tena wa broadbad, bora na nafuu. lakini duh labda ndio mashirika ya Umma mpaka aje TX.
   
 4. tototundu

  tototundu Senior Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  TTCL walianza na package nzuri sana mwanzo, ile ya sh 40 per mb, nikasikia makampuni mengine wakiongozwa na vodacom yalilalamika kwa TCRA TTCL wanauwa biashara yao ya internet (wakati huo voda, tigo, zain ilikuwa about sh 300 per mb) ikabidi TTCL wapandishe bei kwa nguvu ingawa bei ya awali haikuwa na hasara kwao.

  Vodacom sasa hivi wana package mpaka ya 15MB kwa shilingi 500, almost the same as bei ile ya mwanzo ya TTCL ya Sh 40 kwa MB.
  Nahisi hapa kuna hujuma pia, au TTCL bado wamelala.
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Mkubwa, kwa ujumla tanzania bado tuko nyuma na tunanyonywa sana katika mawasiliano ya data.
  Lakini hata hvo, kwa fixed line bado nitaprifaa TTCL! Sijajua wewe unazungumzia ttcl mobile au fixed, fixed is cheper and faster: Tsh15/mb@8mbps!! and less kwa matumizi makubwa!
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  TTCL ni kampuni ya umma (ikisimamiwa na serikali) hii hii tunayoifahamu. Muswada wa marekebisho yoyote ya operations za ttcl ni mambo ya sera ya nchi. Ikitaka kufanya mageuzi yoyote makubwa lazima approval ifanyike serikalini, wakati fulani kuna maamuzi kuhusu ttcl yalitakiwa yawe approved na bunge spika wa bunge wakati huo alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya vodacom tz aka (wivu wa kike) kwa maelezo haya utakuwa umepata majibu kwamba who is who in this country.
   
 7. r

  rizikicr Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  TTCL wanatoa huduma zilizo cheap, kwa mfano ttclbb standard ni tsh 30,000/= for 2Gb per month. Lakini hakuna advertisement yoyote wanayofanya, hata kuwapigia simu wateja wao wa kawaida kuwapa taarifa za mabadiliko ya bei imewashinda. miye naona kuna kuvivu fulani, au wanajihujumu wenyewe.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Vote for changes! CHADEMA
   
 9. tototundu

  tototundu Senior Member

  #9
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo ndipo ninapopataka. Tshs 15/mb.(ingawa sina uhakika kama ni kweli) Ukitaka hii bundle inaanzia Tshs 45,000 kwa 1 GB kwenda juu. Kama kungekuwa na bundle lets say ya Shilling 1000 (1000/15 = 66.7MB), bundle ya ya Shilling 2000 (2000/15 = 133MB) etc. Huku kwenye bundle ndogo ndogo ndio kuna wateja wengi sana, na watu wengi wataconnect na fixed wire services kwa incentives kama hizi, sijui huko TTCl hakuna mwenye mawazo mapya au hawaoni kampuni nyingine zinafanyaje.....
   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Da!, mkuu, 30,000=2gb mbona reasonable sana, hzo za elfu mbili utatumia muda gani mkuu? TTCL nadhani hawana vocha za jerojero! Lakini nadhani itafika muda watalazimika kufanya hivyo kama wataona soko linaelekea huko!
   
 11. tototundu

  tototundu Senior Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni marketing strategies tu, ZANTEL wana offer ya 2GB kwa shillingi 10,000 (kwa wiki) na 2GB kwa shilling 35,000 (kwa mwezi). On top of that wana 250MB kwa shilling 10,000 kwa mwezi na 250MB kwa shilling 6000 kwa siku. Nina mtu ndani ya Zantel ananiambia idadi yao ya wateja imeongezeka wenyewe wanashangaa.
   
 12. tototundu

  tototundu Senior Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwenye vocha za shilling elfu mbili mbili ndiko kuna wateja wengi. Vodacom wana mpaka shillingi 300. TTCL wana fixed na wireless, halafu bao wamelala
   
Loading...