Hivi ni Kwanini? .........................sijui jibu

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,291
1,250
Hivi ni kwanini ina kuwa hivyo? Jiulize haya yanatutokea kila siku..

LAW OF QUEUE:

Ukibadilisha mstari unapopanga foleni bank, supermarket ama kwenye huduma ya foleni ule uliouacha unakwenda mbio zaidi.

LAW OF TELEPHONE:
Namba unayopiga kwa makosa daima haipo bize (busy) unayoitafuta haipatikani

LAW OF MECHANICAL REPAIR:

Mikono yako inapokuwa michafu pua inaanza kuwasha ili uikune

LAW OF THE ALIBI:

Ukimdanganya bosi kuwa umechelewa kwa sababu gari lako limepata pancha kesho yake utapata pancha kweli, hata ukisingizia ugonjwa basi utaumwa kweli

BATH THEOREM:

Ukishaanza kuoga tu simu itaanza kuita

LAW OF ENCOUNTERS:

Uwezekano wa kuonekana na watu unaongezeka unapokuwa na mtu unayetaka usionekane ukiwa nae

LAW OF THE RESULT:
Unapojaribu kumueleza mtu kwamba mashine yako imeharibika ukiwasha itafanya kazi

LAW OF BIOMECHANICS:
Sehemu inayowasha mwilini huwasha zaidi pale ambapo huwezi kujikuna, unaokuwa na watu basi utawashwa matakoni ama kwenye korodani ambako ni soo kujikuna.

THEATRE RULE:

Watu wanaokalia viti vizuri ndio wanaochelewa kufika

LAW OF COFFEE:

Ukikaa tu ofisini na kuanza kunywa kahawa ama chai yako basi bosi atakuita na kukuchelewesha mpaka kahawa/ chai yako ipoe.

Ama kweli NGOMBE WA MASKINI HAZAI

Je ni kweli jamani?????????

afrodenzi

Platinum Member
Nov 1, 2010
18,152
2,000
hahhahhahhah Rev leo umeniacha hoi..
Duhh hii ni kweli asilimia mia ya mia..
mmmhhh yaani hayo mambo yote yanatokeaga sana .mmmhh
 
Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,291
1,250
hahhahhahhah Rev leo umeniacha hoi..
Duhh hii ni kweli asilimia mia ya mia..
mmmhhh yaani hayo mambo yote yanatokeaga sana .mmmhh

Leo umenipa Thanks lazima nitaokota hela

The Following User Says Thank You to Rev Masanilo For This Useful Post:

afrodenzi (Today)​
 
Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,291
1,250
Leo asubuhi imenikuta hii

BATH THEOREM:
Ukishaanza kuoga tu simu itaanza kuita
 
Pelosi

Member
Jul 22, 2010
83
70
LAW OF QUEUE:
Ukibadilisha mstari unapopanga foleni bank, supermarket ama kwenye huduma ya foleni ule uliouacha unakwenda mbio zaidi.

LAW OF ENCOUNTERS:
Uwezekano wa kuonekana na watu unaongezeka unapokuwa na mtu unayetaka usionekane ukiwa nae

Hizi zimeshanitokea mara nyingi sana....
 
Eng. Smasher

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
745
0
Rev hizi hapa chini sio kweli esp inayonihusu LAW OF RESULTS labda mashine yako iwe haijaharibika mkuu!!
Hiyo ya cahi labda kwa wanaofanya kazi za u mesenja mkuu!!
Hiyo ya Simu kidogo huwa inatokea!

Hivi ni kwanini ina kuwa hivyo? Jiulize haya yanatutokea kila siku..

BATH THEOREM:

Ukishaanza kuoga tu simu itaanza kuita

LAW OF THE RESULT:
Unapojaribu kumueleza mtu kwamba mashine yako imeharibika ukiwasha itafanya kazi

LAW OF COFFEE:

Ukikaa tu ofisini na kuanza kunywa kahawa ama chai yako basi bosi atakuita na kukuchelewesha mpaka kahawa/ chai yako ipoe.

Ama kweli NGOMBE WA MASKINI HAZAI

Je ni kweli jamani?????????

myao wa tunduru

JF-Expert Member
Mar 9, 2010
615
250
hivi ni kweli pia kama una tumbo la kuendesha ukikaribia mlango wa msalani kasi ya usumbufu wa kubwa kutaka kutoka inazidi?
 
bacha

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
4,284
1,195
hivi ni kweli pia kama una tumbo la kuendesha ukikaribia mlango wa msalani kasi ya usumbufu wa kubwa kutaka kutoka inazidi?

ukiwa unaumwa una matatizo ya kikohozi, kinaweza kisikusumbue pindi unapokuwa peke yako lakini ukiwa kwenye mkusanyiko wa watu tu kinachachamaa balaa!
 
Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,291
1,250
ukiwa unaumwa una matatizo ya kikohozi, kinaweza kisikusumbue pindi unapokuwa peke yako lakini ukiwa kwenye mkusanyiko wa watu tu kinachachamaa balaa!

Unaweza kuwa na appointment na watu wakubwa sana kwako, na siku hiyo unataka uwaimpress, basi tumbo litaunguruma ile mbaya, hii itakukosesa hata amani! Ukimalizana nao tu tumbo haliungurumi tena. Kwanini jamani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom