Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,478
- 30,141
Tumesikia vituko na hila mbalimbali wanazofanyiwa wagombea wa upinzani, hususani wa chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema katika uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini, tarehe 24 mwezi Novemba, mwaka huu
Vituko kama vile wasimamizi wa uchaguzi "kuzikimbia" ofisi zao katika siku ambayo ndiyo iliyoelezwa kuwa rasmi ya kuchukua fomu za kugombea uongozi wa serikali za mitaa, ndiyo habari ya mjini hivi sasa
Wagombea wa upinzani kupewa fomu, na wasimsmizi wa uchaguzi, ambazo hazijapigwa mihuri, ndiyo habari nyingine inayo- trend sana hivi sasa
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, hivi hiki ninachokiona kwenye uchaguzi huu, ndicho kinachoshabiana na tambo zote za wanaccm kuwa upinzani nchini kwetu umejifia wenyewe, kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli za kujenga reli ya SGR, Bwawa la umeme kutoka mto Rufiji na kununua ma-dreamlimer ambapo watetezi hao wa utawala huu wa awamu ya tano, umekuwa ukidai kuwa maendeleo aliyoyafanya Mheshimiwa Rais Magufuli, katika kipindi hiki, hayakuwahi fanyika katika tawala zote za awamu zilizopita!
Ningependa kuwauliza hao watetezi wakubwa wa utawala wa awamu hii, hivi si mnaijua ile methali isemayo kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza??
Sasa ningependa kuwauliza hao wapambe, ni kitu gani mnachokihofia, wakati mnajua kuwa mazuri mnayoyafanya yanaonekana hadi na kipofu??
Hivi hii hali inayoendelea, tukiunganisha dots, tutakuwa tunakosea tukisema natokana na vitisho alivyovitoa Jiwe, alipowatamkia kuwa nyiye maDED ninawapa magari ya kifahari ya kutembelea, nyumba nzuri za kuishi na mishahara minono............
Halafu nisikie umemtangaza mpinzani kashinda katika eneo lako, utakuwa umejifukuzisha kazi wewe mwenyewe!
Nchi yetu kikatiba ni ya mfumo wa vyama vingi, na kwa maana hiyo kwa mwananchi kuchagua kiongozi wa upinzani siyo dhambi......
Kama nyiye watawala wetu mlikula kiapo cha kuitii Katiba hiyo, kwa hiyo ni vyema sisi wananchi tukaona KWELI Katiba hiyo inatekelezwa kwa vitendo