Hivi ni kwanini Rais Magufuli anafuatiliwa sana nchini Kenya?

Hili nalo lina kaukweli fulani, tangu mchome vifaranga na kukamata ng'ombe wetu, vilisababisha uhasama baina yetu kiasi hata Wakenya ambao hawakua wana issue na Tanzania wakajua kweli mumefikisha chuki zenu kwenye kiwango kipya.

Teh teh teh tihiii
siyo hilo bana.
kenya people tend to compare your crying baby with our bulldozer.
🤣🤣🤣😅😅😅
ahaaa haaa haaa
 
Hili nalo lina kaukweli fulani, tangu mchome vifaranga na kukamata ng'ombe wetu, vilisababisha uhasama baina yetu kiasi hata Wakenya ambao hawakua wana issue na Tanzania wakajua kweli mumefikisha chuki zenu kwenye kiwango kipya.

Labda pia inaweza kuwa ni sababu, who knows?
 
Nina rafiki huko wakati mwingine hunipa news za Raisi Magufuli ambazo mimi mwenyewe sijazisikia bado, sikumbuki ni lini Raisi wa JMTZ amekuwa gumzo kubwa hivi huko Kenya kama Raisi Magufuli, hivi ni
kwa nini?

Najua haya si unayotaka kuskia, lakini huu ndio ukweli.
Wakati ule tu Magufuli ana 'trend' Kenya ni anapofanya kitendo cha ujinga. Mfano kutuma majeshi forex, kupiga risasi wapinzani, kununa korosho kwa lazima ama kuchoma kuku za Kenya.

Unafaa utembee Kenya angalau siku kidogo. Vyombo vya habari hapa huenda hata mwaka mmoja bila kuleta habari yoyote ya Tanzania.
 
Juzi Walipokuwa wanazindua OSBP ya namanga wakenya walihudhuria kwa wingi kuliko watz, na kilichowaleta ni kumuona Magu maana Rais wa kwao wanamfahamu toka mda.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ili usikae mjinga, fungua Facebook ya Uhuru Kenyatta, uangalie wale watu yeye huvutia popote aendapo.
Namanga hata haikufika nusu ya umati ambao yeye hupata kila siku.
 
Kwanini basi ukasema wakenya walitokea Namanga kwa wingi kwa sababu ya Magu?
Ilhali Uhuru kila siku huvutia umati mkubwa kila aendapo?
Ulikuwepo lakini? Nisije nikawa nabisha na mtu ambae siku ta tukio alikuwa kajiado hapa.

Kama ulikuwepo utanielewa lkn kama ulikuwa kajiado huwezi kuelewa chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina rafiki huko wakati mwingine hunipa news za Raisi Magufuli ambazo mimi mwenyewe sijazisikia bado, sikumbuki ni lini Raisi wa JMTZ amekuwa gumzo kubwa hivi huko Kenya kama Raisi Magufuli, hivi ni
kwa nini?
Kenya ndiyo walikuwa wauzaji namba moja wa Tanzanite duniani. Baada ya JPM kuingia madarakani hawana kipande hata ki1 cha Tanzanite. Hii imewauma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua haya si unayotaka kuskia, lakini huu ndio ukweli.
Wakati ule tu Magufuli ana 'trend' Kenya ni anapofanya kitendo cha ujinga. Mfano kutuma majeshi forex, kupiga risasi wapinzani, kununa korosho kwa lazima ama kuchoma kuku za Kenya.

Unafaa utembee Kenya angalau siku kidogo. Vyombo vya habari hapa huenda hata mwaka mmoja bila kuleta habari yoyote ya Tanzania.

Siyo kweli huenda Kenya mara kwa mara na ndo maana nikauliza hilo swali, sijatoa hewani tu, hata Gavana wa Nairobi anamnukuu Magufuli kila mara.
 
Huyu mleta mada Barbarosa anafurahisha, anavosema kwamba huwa anaambiwa haya yote na 'mwenzake', eti hadi anatumiwa links. Kupata habari za Magufuli au Tz kwenye media za Kenya ni nadra sana. Tena sana. Sio kwenye magazeti, Tv wala kwenye radio. Labda wakati anapofanya vitu vya ajabu ajabu ndio utaona habari zinazomhusu, kwenye mitandao ya kijamii. Sanasana kwenye jukwaa hili.
 
Huwa natumiwa links mara kwa mara, kuhusu tv sijui ila Magazeti haipiti wiki wataandika chochote kuhusu Magufuli, nitakupa mfano juzi kati nilitumiwa kuambiwa Magufuli kamuombea mama yake mgonjwa hospitalini, Wakenya wanajua hilo nilishangaa.
 
Nimemskia tu Sonko akimnukuu Magufuli mara moja. Alimtumia Magufuli kama excuse ya kutoa matamshi ya kijinga, ama policy ya upuzi.
Sidhani uzi huu uliletwa hapa ili wakenya wajibu swali la mleta mada. Utakuwa ni uzi wa ligi za kisiasa, siasa za Tz. Mimi binafsi huwa nina upendo mkubwa wa kufatilia habari kama zinazochimbuka kila uchao Tz ila kwenye media za Kenya hazipatikani hata kidogo. Yaani kwenye magazeti hata wiki mbili zitapita bila kuona jina la Tz wala Magufuli. Kwenye Tv hawaleti habari kutoka Tz, mitandaoni, mara moja moja.
 
Nimemskia tu Sonko akimnukuu Magufuli mara moja. Alimtumia Magufuli kama excuse ya kutoa matamshi ya kijinga, ama policy ya upuzi.

Mfano juzi kati nimetumiwa link ktk Kenya kwamba Mama yake Raisi Magufuli ni mgonjwa na picha Raisi Magufuli akimtembelea Mama yake hospitalini, nilishangaa iweje Mkenya alijue hili?
 
Huwa natumiwa links mara kwa mara, kuhusu tv sijui ila Magazeti haipiti wiki wataandika chochote kuhusu Magufuli, nitakupa mfano juzi kati nilitumiwa kuambiwa Magufuli kamuombea mama yake mgonjwa hospitalini, Wakenya wanajua hilo nilishangaa.
Eti Magufuli alifanya nini? Hahaa! :D Hebu tupia hiyo link basi, ya habari hizo kama zilivoripotiwa kwenye media za Kenya. Na iwe media inayoheshimika tafadhali.
 
Back
Top Bottom