Hivi ni kwanini Ofisi nyingi za matawi ya Chadema zinahali mbaya sana.

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,912
Tofauti na CCM, ofisi za Chadema za vitongoji, kata, wilaya na mikoa ni dhoofu mno, kiasi ambacho hazina hata hadhi ya kuitwa ofisi.

Utakuta ofisi nyingi za huko mikoani, ni chumba kimoja kilichochoka, either kinakua karibu na gereji au sokoni.

Utakuta hapo nje ya ofisi, kuna jiwe kuubwa na bendera iliyochanika chanika, au kuchakaa.

Nashindwa kuelewa hawa watani zangu , wanamaanisha nini, maana hadhi ya ofisi haiendani kabisa na status ya chama, kama wengi wetu tunavyofahamu.

Sijui kama kweli wanamalengo ya kua chama cha muda mrefu au wamejikita zaidi katika kuboresha makao makuu.

Lakini la ajabu zaidi, hata makao makuu yenyewe hayaendani na hadhi ya chama chao.

Kuna nini huko chadema.
 
Ni Upumbavu kudhani uimara na ustawi wa chama ni majengo.Chama lazima kiwe na watu wanaokiunga mkono.Rasilimali fedha ya chama lazima ipewe kipaumbele cha kwanza ktk kutafuta wanachama na kueneza Itikadi.Hayo ndo yanayoweza kukufikisha malengo ya kisiasa.Majengo ni suala la ziada ikiwa fedha zitabaki.Hapa kuna sababu nyingi.Hata hivo Rejea Ujenzi wa Chama cha Tanu.Hadi tunapata Uhuru hakikuwa kimejielekeza Katika majengo ila kutafuta uungaji mkono wa watu.Ndo mana Miaka kadhaa ilopita Cdm walijielekeza zaidi Katika operation mbalimbali za uenezi na mafunzo kwa wanachama na viongozi wake.Hilo limewafikisha walipo kama Chama.wangechagua kutumia vimilioni sitini walivokuwa wakipata miaka ya 2005-2010,au vimilioni Mia mbili na nusu walivokuwa wakivipata 2010-2015 kujengea majengo makubwa ya kifahari yanayofikia gharama za mabilioni,Wangekuwa ni chama kidogo sana Leo kuliko Hali ilivo sasa.Mwisho tambua kwamba hata CCM wenyewe mpaka leo hii hawajawahi kujenga ofisi wala miradi wanayodai kuwa nayo.Wanachomiliki ni matokeo ya uporaji walioufanya wakati wa chama kimoja kwa kisingizio cha chama kushika hatamu.Mashule yanayotwa ya CCM yalijengwa kwa Michango ya lazima tena kwa wananchi wote au yalitaifishwa kikakabidhiwa chama,Viwanja vya michezo na vibanda vya masoko sehemu nyingi nchini vimejengwa na wananchi wote kwa mtindo uleule wa kusimamiwa na nguvu ya serikali,Ofisi za CCM zimejengwa kama ofisi za Serikali kwa Michango ya lazima,Ndo mana vijijini kwa Ofisi za CCM zina selo maarufu kama lokapu,chama kisingejenga selo isipokuwa Serikali.Ni ujinga kutumia Ruzuku kujenga maofisi badala ya kueneza chama na Itikadi yake ili kufikia malengo ktk Chaguzi
 
Tofauti na CCM, ofisi za Chadema za vitongoji, kata, wilaya na mikoa ni dhoofu mno, kiasi ambacho hazina hata hadhi ya kuitwa ofisi.

Utakuta ofisi nyingi za huko mikoani, ni chumba kimoja kilichochoka, either kinakua karibu na gereji au sokoni.

Utakuta hapo nje ya ofisi, kuna jiwe kuubwa na bendera iliyochanika chanika, au kuchakaa.

Nashindwa kuelewa hawa watani zangu , wanamaanisha nini, maana hadhi ya ofisi haiendani kabisa na status ya chama, kama wengi wetu tunavyofahamu.

Sijui kama kweli wanamalengo ya kua chama cha muda mrefu au wamejikita zaidi katika kuboresha makao makuu.

Lakini la ajabu zaidi, hata makao makuu yenyewe hayaendani na hadhi ya chama chao.

Kuna nini huko chadema.
Good observation.
 
Back
Top Bottom