Hivi ni kwanini nchi za wazungu kila wanapotupa misaada tunawaita wahisani wetu wa maendeleo lakini pale wanapotukosoa tunawaita mabeberu?

msaada huwa hauna masharti(mhisani).

pesa yenye masharti sio msaada(beberu).

hii ni sawa na unakwenda kituo cha watoto yatima,unawapa hela wasimamizi wake kisha uwaambie hutaki wanunulie mchele hizo pesa.kama wana uhitaji na mchele kwa wakati huo wataichukia pesa yako.
 
Kuna msamiati mpya umetungwa hususani na watawala wetu wa serikali ya awamu ya 5 kwa kuwaita nchi za wazingu kuwa ni mabeberu, pale wanapotoa "constructive criticism" yenye lengo la kututaka tujirekebishe ili nchi yetu ipate ufanisi wa hali ya juu.

Hata hivyo ajabu ni kuwa wazungu hao hao, wanapokaa kimya bila kusema lolote kutokana na maovu tunayoyafanya, tunawasifu sana na kuwaita kuwa ni wahisani wetu wa maendeleo!

Tunafahamu kuwa katika vitabu vyote vya dini vinatwambia kuwa mkamilifu ni mmoja pekee, ambaye ni Mungu aliyetuumba na sisi binadamu wengine wote, tuna mapungufu yetu, ambayo tunapaswa tuelezane ili tujirekebishe.

Sasa hili la watawala wetu kuchukua "capacity" ya Mungu wetu na kutotaka kabisa kukosolewa ni kujiletea laana, kwa kuwa watakuwa wanapingana na maandiko matakatifu ambayo yanampa Mungu pekee, ambaye hapaswi kukosolewa kwa lolote na sisi binadamu tunafahamu kuwa ni yeye pekee Mungu wetu, ambaye yuko "perfect by 100 percent"

Vile vile kuna kumezuka propaganda za kitoto sana za watawala wetu za kudai kuwa tupo kwenye vita ya kiuchumi na hao wazungu, ndiyo sababu ya hao wazungu aka mabeberu kutuonea wivu na kutupiga vita!

Hivi sisi kanchi tunaoagiza hata vijiti tu vya kuchokonoa "tooth picks" tunawezaje kupigwa vita na nchi kama Marekani, yenye uwezo wa kutengeneza kila kitu tunachotumia kuanzia magari ya kifahari tunayotembelea hadi hayo madege tunayoyaita "dreamliners" tunayotamba nayo kuwa tumeyanunua kwa fedha taslimu?

Vile vile hii nchi yetu tunapenda sana kujimwambafai kuwa eti nchi yetu tuna uwezo wa kuwa "donor country" kwa hizo nchi za mabeberu!

Sasa mbona serikali yetu imeanza kuhaha na kuweweseka sana, baada tu ya hizo nchi za mabeberu za EU, kuonyesha dalili za kutukatia misaada baada ya wao kubaini kuwa nchi yetu imeuvuruga mno mfumo wa kidemokrasia na uchaguzi mkuu uliopita na inakiuka mno haki za binadamu?

Tunapaswa tujisahihishe, wazungu wanapotukosoa tukae chini na kuangalia ni wapi tulipokosea na tujirekebishe, badala ya hii hali tunayoendelea nayo ya kujiona sisi tuko 100 percent perfect na kila wazungu wanapotukosoa tuwaite majina mabaya kuwa wao ni mabeberu, lakini wanapokaa kimya kama China, tunawasifu na kuwaita ni washirika na wahisani wetu wazuri wa maendeleo!
Hiyo kawaida sana mbona binadamu akiwa hai uitwa mtu na akifa anaitwa marehemu mifano iko mwizi kila jina lina sababu zake watu ubadilishwa majina kutokana na matendo yao.
 
Twawaita wahisani kwa sababu tangu uhuru wamekuwa wakishirikiana na sisi kwenye kutusaidia kwenye miradi ya maendeleo.

Ndo maana tunao NIDA, SIDA, DANIDA , WFP na wengine tunao miaka na miaka.

Hawa wahisani hutupatia fedha za miradi ya maendeleo na huwa si mikopo.

Halafu kuna IMF na World Bank, hawa wapo kutusaidia mikopo na ushauri wa namna ya kuendesha uchumi, ila kwa masharti fulanifulani, kama kupunguza matumizi ya serikali na mengine.

Mabeberu (imperialists) ni makampuni makubwa na taasisi za kimataifa ambayo yapo kwenye nchi hizo na yana uwezo wa kulobby kwenye hizi taasisi na kupenyeza ajenda zao.

Wakifanya hivyo, wote waunganishwa na kuitwa mabeberu.

Mfano ni chama cha CDU ambacho mbunge wake ni mmoja wa wale wanamakati watano walojadili kuhusu fedha za COVID-19.

CDU ni chama kinachorikiana na Chadema.

Hivyo mabeberu yapo kutaka rasilimali, malighafi na vyanzo vingine kutoka Afrika lakini si kwa nia njema bali kwa kupora na kutumia vibaraka wao ambao huziweka rasilimali hizo rehani.

Kwahiyo, Tanzania haina ugomvi na Denmark, wala Sweden, wala Norway, Ujerumani, Uingereza na Marekani.

Ila inaweza kuendeelea kujibu hoja kadha wa kadha zinazotoka kwa wawakilishi wa mabeberu.

Kumbuka nchi wahisani hazijijajibu wala kuongea chochote hadi sasa na hiyo ni kwasababu wote wameonekena mambo waloyafanya baada ya uchaguzi wa mwaka huu.

Hivyo kuna tofauti ya wahisani (mashirika ya maendeleo) na mabeberu (makampuni ya kibepari).
 
Kuna msamiati mpya umetungwa hususani na watawala wetu wa serikali ya awamu ya 5 kwa kuwaita nchi za wazingu kuwa ni mabeberu, pale wanapotoa "constructive criticism" yenye lengo la kututaka tujirekebishe ili nchi yetu ipate ufanisi wa hali ya juu.

Hata hivyo ajabu ni kuwa wazungu hao hao, wanapokaa kimya bila kusema lolote kutokana na maovu tunayoyafanya, tunawasifu sana na kuwaita kuwa ni wahisani wetu wa maendeleo!

Tunafahamu kuwa katika vitabu vyote vya dini vinatwambia kuwa mkamilifu ni mmoja pekee, ambaye ni Mungu aliyetuumba na sisi binadamu wengine wote, tuna mapungufu yetu, ambayo tunapaswa tuelezane ili tujirekebishe.

Sasa hili la watawala wetu kuchukua "capacity" ya Mungu wetu na kutotaka kabisa kukosolewa ni kujiletea laana, kwa kuwa watakuwa wanapingana na maandiko matakatifu ambayo yanampa Mungu pekee, ambaye hapaswi kukosolewa kwa lolote na sisi binadamu tunafahamu kuwa ni yeye pekee Mungu wetu, ambaye yuko "perfect by 100 percent"

Vile vile kuna kumezuka propaganda za kitoto sana za watawala wetu za kudai kuwa tupo kwenye vita ya kiuchumi na hao wazungu, ndiyo sababu ya hao wazungu aka mabeberu kutuonea wivu na kutupiga vita!

Hivi sisi kanchi tunaoagiza hata vijiti tu vya kuchokonoa "tooth picks" tunawezaje kupigwa vita na nchi kama Marekani, yenye uwezo wa kutengeneza kila kitu tunachotumia kuanzia magari ya kifahari tunayotembelea hadi hayo madege tunayoyaita "dreamliners" tunayotamba nayo kuwa tumeyanunua kwa fedha taslimu?

Vile vile hii nchi yetu tunapenda sana kujimwambafai kuwa eti nchi yetu tuna uwezo wa kuwa "donor country" kwa hizo nchi za mabeberu!

Sasa mbona serikali yetu imeanza kuhaha na kuweweseka sana, baada tu ya hizo nchi za mabeberu za EU, kuonyesha dalili za kutukatia misaada baada ya wao kubaini kuwa nchi yetu imeuvuruga mno mfumo wa kidemokrasia na uchaguzi mkuu uliopita na inakiuka mno haki za binadamu?

Tunapaswa tujisahihishe, wazungu wanapotukosoa tukae chini na kuangalia ni wapi tulipokosea na tujirekebishe, badala ya hii hali tunayoendelea nayo ya kujiona sisi tuko 100 percent perfect na kila wazungu wanapotukosoa tuwaite majina mabaya kuwa wao ni mabeberu, lakini wanapokaa kimya kama China, tunawasifu na kuwaita ni washirika na wahisani wetu wazuri wa maendeleo!
ULIONA WAPI HUYOMZUNGU ANATOA MSAADA WA BUREE?? MZUNGU HAJAWAHI TOA MSADAA NA HATO TOA MSAADA.
 
Back
Top Bottom