Hivi ni kwanini nchi za wazungu kila wanapotupa misaada tunawaita wahisani wetu wa maendeleo lakini pale wanapotukosoa tunawaita mabeberu?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,339
2,000
Kuna msamiati mpya umetungwa hususani na watawala wetu wa serikali ya awamu ya 5 kwa kuwaita nchi za wazingu kuwa ni mabeberu, pale wanapotoa "constructive criticism" yenye lengo la kututaka tujirekebishe ili nchi yetu ipate ufanisi wa hali ya juu.

Hata hivyo ajabu ni kuwa wazungu hao hao, wanapokaa kimya bila kusema lolote kutokana na maovu tunayoyafanya, tunawasifu sana na kuwaita kuwa ni wahisani wetu wa maendeleo.

Tunafahamu kuwa katika vitabu vyote vya dini vinatwambia kuwa mkamilifu ni mmoja pekee, ambaye ni Mungu aliyetuumba na sisi binadamu wengine wote, tuna mapungufu yetu, ambayo tunapaswa tuelezane ili tujirekebishe.

Sasa hili la watawala wetu kuchukua "capacity" ya Mungu wetu na kutotaka kabisa kukosolewa ni kujiletea laana, kwa kuwa watakuwa wanapingana na maandiko matakatifu ambayo yanampa Mungu pekee, ambaye hapaswi kukosolewa kwa lolote na sisi binadamu tunafahamu kuwa ni yeye pekee Mungu wetu, ambaye yuko "perfect by 100 percent"

Vile vile kuna kumezuka propaganda za kitoto sana za watawala wetu za kudai kuwa tupo kwenye vita ya kiuchumi na hao wazungu, ndiyo sababu ya hao wazungu aka mabeberu kutuonea wivu na kutupiga vita.

Hivi sisi kanchi tunaoagiza hata vijiti tu vya kuchokonoa "tooth picks" tunawezaje kupigwa vita na nchi kama Marekani, yenye uwezo wa kutengeneza kila kitu tunachotumia kuanzia magari ya kifahari tunayotembelea hadi hayo madege tunayoyaita "dreamliners" tunayotamba nayo kuwa tumeyanunua kwa fedha taslimu?

Vile vile hii nchi yetu tunapenda sana kujimwambafai kuwa eti nchi yetu tuna uwezo wa kuwa "donor country" kwa hizo nchi za mabeberu.

Sasa mbona serikali yetu imeanza kuhaha na kuweweseka sana, baada tu ya hizo nchi za mabeberu za EU, kuonyesha dalili za kutukatia misaada baada ya wao kubaini kuwa nchi yetu imeuvuruga mno mfumo wa kidemokrasia na uchaguzi mkuu uliopita na inakiuka mno haki za binadamu?

Tunapaswa tujisahihishe, wazungu wanapotukosoa tukae chini na kuangalia ni wapi tulipokosea na tujirekebishe, badala ya hii hali tunayoendelea nayo ya kujiona sisi tuko 100 percent perfect na kila wazungu wanapotukosoa tuwaite majina mabaya kuwa wao ni mabeberu, lakini wanapokaa kimya kama China, tunawasifu na kuwaita ni washirika na wahisani wetu wazuri wa maendeleo.
 
Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
8,642
2,000
Jana slowslow/polepole kasema anawapenda sana na kuwaheshimu sana baada ya wao kutaka waeleze walipeleka wapi hela waliyopewa ya kusuka wakati hawajasuka? 😊
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,339
2,000
Jana slowslow/polepole kasema anawapenda sana na kuwaheshimu sana baada ya wao kutaka waeleze walipeleka wapi hela waliyopewa ya kusuka wakati hawajasuka? 😊
Hapo wameingia 18 ya hao mabeberu wazungu.................

Hivi waliwezaje "kuzitafuna" pesa za msaada wa nchi za EU za corona, wakati nchi yetu imeutangazia ulimwengu kuwa haina hata mgonjwa mmoja wa corona?
 
Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
8,642
2,000
Hapo wameingia 18 ya hao mabeberu wazungu.................

Hivi waliwezaje "kuzitafuna" pesa za msaada wa nchi za EU za corona, wakati nchi yetu imeutangazia ulimwengu kuwa haina hata mgonjwa mmoja wa corona?
Tusubiri zile saa 48 walizopewa watakuwa wametoa majibu mkuu.

Nawachora ccm tu hapa
 
Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,487
2,000
Hata wachina wanatupa pesa mbona hatujawaita mabeberu? Kwa kuwa hawaingilii mambo yetu.
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
5,662
2,000
condom, vyandalua, vidonge vya kupunguza kuzaliana, uhuru wa mwanaume aliyeolewa na mwanume mwenzake kujitangaza nk ndiyo misaada yao hiyo mkuu!
Tukijenga mabwawa ya kufua umeme ili umeme ushuke bei au tukiendesha uchaguzi kwa fedha zetu wakakasirika! Jiulize KWANINI!
 
Sendoro Mbazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
1,453
2,000
Safi
condom, vyandalua, vidonge vya kupunguza kuzaliana, uhuru wa mwanaume aliyeolewa na mwanume mwenzake kujitangaza nk ndiyo misaada yao hiyo mkuu!
Tukijenga mabwawa ya kufua umeme ili umeme ushuke bei au tukiendesha uchaguzi kwa fedha zetu wakakasirika! Jiulize KWANINI!
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,755
2,000
Tutafakari pamoja.

Ukikopeshwa shilingi elfu moja riba ikawa elfu tatu hivyo mwishoni ukatakiwa kulipa elfu nne, na mkopeshaji huyo akitoa shilingi ishirini kwenye riba uliyompa ya elfu tatu na kusema amekupa msaada. Je. Utasema shilingi ishirini alizokupa na shilingi elfu moja alizokukopesha vyote ni msaada!?

Kama jibu lako ni ndiyo basi mkopeshaji asiitwe kupe wala beberu lakini kama jibu ni hapana lazima majina hayo yanamfaa mkopeshaji.
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
4,308
2,000
pale wanapotoa "constructive criticism" yenye lengo la kututaka tujirekebishe ili nchi yetu ipate u
Hiyo ☝🏿 ni kwa mtazamo wako, siyo kwa mtazamo wa serikali au viongozi wa nchi yetu. Kilicho 'constructive criticism' kwako siyo lazima kiwe hivyo kwa watu wote. Mtazamo wako siyo universal!
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,197
2,000
Tutafakari pamoja.

Ukikopeshwa shilingi elfu moja riba ikawa elfu tatu hivyo mwishoni ukatakiwa kulipa elfu nne, na mkopeshaji huyo akitoa shilingi ishirini kwenye riba uliyompa ya elfu tatu na kusema amekupa msaada. Je. Utasema shilingi ishirini alizokupa na shilingi elfu moja alizokukopesha vyote ni msaada!?

Kama jibu lako ni ndiyo basi mkopeshaji asiitwe kupe wala beberu lakini kama jibu ni hapana lazima majina hayo yanamfaa mkopeshaji.
Ni benki gani duniani inatoa mkopo kwa riba hiyo ya 300% au umeamua kuandika changamsha genge.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,755
2,000
EU hivi ni benki kumbe?
******
The EU provides funding in the form of loans and grants for a broad range of projects and programmes covering areas such as education, health, consumer protection, environmental protection and humanitarian aid. Funding is managed according to strict rules which help to ensure that there is tight control over how funds are used and that funds are spent in a transparent and accountable manner

===
Chunguza kwanza hoja kabla ya kumshambulia mleta hoja. Ona sasa ulivyojiabisha.
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,193
2,000
Kwa hiyo ukiwa na njaa kwako, jamaa akajitoeza kukuletea chakula, siku ya aje atake kumchukua mkeo, bado utaendelea kumwona ni mtu mzuri siyo?
 
Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,274
2,000
Mtu anayekupa msaada anaitwa Mhisani.
Mhisani anayetaka kukupangia utumieje misaada yako huyo ni beberu.

Kwa kifupi Mhisani anaweza pia kuwa beberu. Maana hizo ni sifa tu kama kuwa mrefu hakukuzuii kuwa mnene! Na kuwa mnene hakukuzuii kuwa mfupi.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,197
2,000
EU hivi ni benki kumbe?
******
The EU provides funding in the form of loans and grants for a broad range of projects and programmes covering areas such as education, health, consumer protection, environmental protection and humanitarian aid. Funding is managed according to strict rules which help to ensure that there is tight control over how funds are used and that funds are spent in a transparent and accountable manner

===
Chunguza kwanza hoja kabla ya kumshambulia mleta hoja. Ona sasa ulivyojiabisha.
Endelea kuvamia comments za wanaume rijali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom