Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,483
- 30,155
Mahakama kuu imefanya uamuzi wa kihistoria, ambao umeungwa mkono na mamilioni ya wapenda demokrasia nchini ya kubatilisha wakurugenzi ambao pia ni.makada wa Chama cha Mapinduzi, kuwa wasimamizi wa uchaguzi nchini
Kilichonishangaza ni kusikia Mwanasheria Mkuu wa serikali, Dr Adeladus Kilangi, kuwa na nia ya kutaka kukata rufaa ya kupinga uamuzi huo wa mahakama kuu wa kutengua uamuzi wa wakurugenzi, kuendelea kuwa wasimamizi wa chaguzi hizo!
Sasa ninachojiuliza ni sababu zipi zinazomfanya Mwanasheria Mkuu wa serikali akate rufaa, wakati yeye kama Mwanasheria Mkuu, akitambua kuwa chombo cha mahakama ndicho chombo pekee nchini, chenye wajibu wa kuzitafsiri sheria na itakapoona baadhi ya sheria zinakiuka haki ya msingi ya kibinadamu au zinakiuka haki ya msingi ya sheria mama, ambayo ni Katiba ya nchi, chombo hicho kina wajibu wa kuzibatilisha??
Nadhani ni wakati muafaka kwa sasa kwa chombo hicho cha mahakama kuwa wakali zaidi kwa watawala wetu ambao wana kiburi cha hali ya juu na hawataki kutii maamuzi ya mahakama hiyo, ingawa maamuzi hayo yanakuwa yanafurahiwa na mamilioni ya wapenda demokrasia nchini na wanaharakati wa nchi hii