GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,544
- 108,869
Ni kwamba Ulaya na Marekani mipango mingi ya ' Kuwaangamiza ' wale ' Maadui ' tishio wa nchi zao wa ndani au wa nje hufanyika kwa ' Usiri ' mkubwa, uratibu wa Kitaalam zaidi na umakini wa hali ya juu kiasi kwamba hata Kitendo Kikifanyika kuja Kuamini kuwa kimefanya ' Kijasusi ' huwa ni ngumu tofauti na ambavyo kwa nchi za Kiafrika ( ukiziondoa tu Uganda, Rwanda na Tanzania ambazo hazina huu mchezo kwakuwa Wao ni Watu wa Mungu na wanamuogopa sana Mungu ) mipango yao hujulikana kiurahisi na hata Mtoto mdogo.
Hapa huwa kuna udhaifu gani kwa upande wa nchi nyingi za Kiafrika na unadhani ni wapi ambapo nchi nyingi za Ulaya kama Uingereza, Ufaransa na Urusi bila kuisahau na Marekani wanatushindia hasa katika masuala mazima ya Ujasusi / Unjagu hasa katika suala zima la ' Kuwaangamiza ' kama siyo ' Kuwapoteza ' kabisa wale ' Maadui ' wao wa ndani na wa nje?
Karibuni Wajuvi ( Pundits ) wa haya masuala ili kama kawaida Yetu Sisi wengine tuweze Kujifunza mawili matatu kutoka Kwenu.
Nawasilisha.