Hivi ni kwanini maji ya mto Nile yanatoka ziwa Victoria(chini) na yanapandisha kwenda Egypt(juu)? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kwanini maji ya mto Nile yanatoka ziwa Victoria(chini) na yanapandisha kwenda Egypt(juu)?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mfukunyunzi, Apr 29, 2011.

 1. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani wataalamu wa Jiografia na maumbile ya dunia naomba mnisaidie kutatua hili suala:
  Ukitizama jinsi umbile la dunia (kama unaweza angalia hata kwenye lile umbile la dunia linalowekwa maofisini au majumbani) jinsi lilivyo inaonesha dhahiri kuwa eneo lilipo ziwa victoria lipo kwenye uwanda wa chini ukilinganisha na kule ilipo nchi ya Misri sasa chakushangaza ni kuwa maji ya mto Nile yanawezaje kumwagika kutoka ziwa Victoria na kuelekea kule Misri sehemu ambayo iko juu, na kwa uelewa wangu mimi ni kuwa maji huwa yanatiririka kutoka juu na kuelekea chini. Naomba wataalamu na magreat thinkers wenzangu mnisaidie kutatua/kunielewesha hili suala.

  nile river.jpg
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sasa wewe unadanganywa na ramani za ukutani? Chora ardhini ndo utapata picha
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mmmh! Ngoja tusubiri wataalamu!
   
 4. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,037
  Likes Received: 7,474
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika na kama Misri ipo juu au vipi...ila kitu ambacho nina uhakika ncho ni kuwa, ili kuufikia mto Nile popote ulipopita ni lazima ushuke, yaani umepita katika bonde, na kutoka na jiografia ya mahali ambapo mto huo unapopita ndiyo maana huwa linaitwa bonde la mto nile.
  Tusubiri wataalam zaidi waendelee kuchangia, labda wanaweza kutusaidia zaidi
   
 5. RR

  RR JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,718
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Mkuu unachangaya juu na kaskazini?....
   
 6. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapa suala sio ramani bali hoja ni jinsi umbile halisi la dunia jinsi lilivyo
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  As far as my my geography is......lake Victoria is situated where the imaginary line with 0 degree known as equator which divides the earth into two same hemispheres passes...! as you can see its like the childish riddle that asks....KAMA JOGOO AKITAGA YAI KATIKATI YA MLIMA KILIMANJARO YAI LITAANGUKIA UPANDE GANI?
  Hivyo basi, kutokana na kuwa katikati...maji huweza ku-flow katika pande hizo kuu mbili zilizogawanywa....!
  (wanajiografia wanikosoe)
   
 8. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo kidogo naanza kupata mwanga flani.
   
 9. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,406
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikupe jawabu. Unapotazama ramani kitabuni ama iliyobandikwa ukutani ukaona nchi ya Misri ipo juu kama unavyoita wewe (ingawa ukweli ni kuwa ipo Kaskazini wala sii juu) unaweza kujiuliza mara alfu lela ulela hilo swali. Ukweli ni kuwa haipo juu.
  Bara la Afrika, Wanajografia wanatuambia kuwa unapotokea Ethiopia kuelekea kusini unakuwa unaelekea uwanda wa juu. Ina maana kwamba maeneo mengi ya Kusini mwa Afrika yapo juu zaidi ya usawa wa bahari ukilinganisha na maeneo ya Kaskazini. Kwa mantiki hiyo, nchi za Sudani, Ethiopia na Misri zipo chini zaidi ukilinganisha na Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya ambako maji hayo ya mto Nile yanakotokea.

  Jambo kama hilo hilo huwa lina wachanganya watu wengi kuhusiana na mito miwili mkoani Mbeya. Mito hiyo ni Songwe na Kiwira ambayo yote hupeleka maji yake kwenye Ziwa Nyasa (wenyewe wanaliita Ziwa Malawi kwa kuwa ni mali yao) Watu hudhani maji ya mito hiyo hupandisha milima. Lakini ukitazama vema na kukokotoa kiwango cha maeneo hayo kutoka kwenye usawa wa bahari, utagundua hakuna mto unaopandisha mlima.

  Huo ndo mchango wangu.
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  soma google andika the source of river nile and how it flows to egypt utapata maelezo kibao.mm nipo north ya dunia naona kuna milima na mabonde pia ila jua ndio naliona linatoka south east linatua south west yaan kamma nusu duara kimzunguko kwa hivo saa 9 alfajiri limeshaanza kuonekana na kutua saa 3 usiku. sama to river nile limetoka uganda kule na kupita mabonde na sio kupanda milima.
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,988
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mimi sii mtaalam wa Jiografia,ila ninachofahamu ni kuwa bahari zote duniani ziko chini kwenye altitude moja,hivyo maeneo yote ya dunia(kwenye ardhi) ziko juu ya usawa wa bahari hivyo kupelekea maji toka pande tofauti kwenda baharini.
   
 12. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,037
  Likes Received: 7,474
  Trophy Points: 280
  Ninashwishika kusema jibu lako linaweza kuwa na hoja ya kuilinda, ila ngoja nijiridhishe kama hakuna mto unao flow toka kaskazini ya uganda kenya na kwingineko kuingia ziwa Victoria au kutoka kusini mwa Mwa ziwa victoria kuingia humo yaani toka Mwanza Shinyanga n.k
   
 13. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mkuu hapo kwenye red umechemka...ipo mito inayopandisha milima mfano mzuri ni mto Ruaha.
   
 14. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Sasa umemaanisha nini inamaana kama unafaatisha umbo la dunia basi maji yaliyopo ufaransa,canada,rusia kilasiku huku afrika tungekuwa wamafuriko!!
   
 15. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  hamna lolote zaidi ya uchawi wa kiarabu
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,312
  Likes Received: 19,459
  Trophy Points: 280
  shule za kata zina maajabu kweli kweli
   
 17. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Kunavitu haviitaji kuuliza lakini nikakumbuka msemo nikiwa primary eti akini ninywele kilamtu anazake!!
   
 18. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mto Ruaha hauwezi asilani kushindana na kanuni za asili kwa kupandisha milima.
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ukoje huo uchawi wa kiarabu?
   
 20. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Nasikia somo la Geography lilifutwa mashuleni tangia kipindi cha waziri Mungai, hivyo usishangae maswali kama haya. Enzi zetu swali hili angejibu kijana wa darasa la 5!
   
Loading...