GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nimekuwa nikifuatilia mno mienendo ya Walinzi ( Bodyguards ) wa Viongozi Wakuu ( Marais ) wa nchi mbalimbali duniani ( ila kwa wa Tanzania sijawahi ) na kugundua kuwa wengi wao hupenda sana kuwaangalia Watu machoni na siyo mahala pengine.
Kwa mfano unaweza kukuta Kiongozi / Rais anasalimiana na Watu lakini badala ya wale Walinzi kuangalia kile Kitendo cha kupeana mikono au hata kukabidhiana kitu fulani wao ( Bodyguards / Walinzi ) macho yao huwa ' Kodo ' tu kuwaangalia wale Watu machoni tena huku wakiyakaza na kuwakazia kabisa.
Najua humu JF ni Kisima cha Maarifa na wapo Watu ambao wamebobea kabisa katika haya masuala mazima ya Ulinzi wa Viongozi hivyo kama hamtojali naomba mje na mnisaidie ili kuweza kulijua hili kwani huwa napenda mno kupata ' Maarifa ' mbalimbali ya mambo ya duniani.
Nawasilisha.