Hivi ni kwanini kuna watu kila jambo la maendeleo linalofanywa na Serikali wanachukia?

Ni kweli lakini hawa wenzetu humu mitandaoni wamekuwa watu wa kupiga sana kelele kuponda kila kitu yani me naumia sana ki ukweli.
Hutakiwi kuumia , Kama alivyoshauri baba mzazi wa HAJI MANARA.

Dawa ya mwanaye kumzuia asiongee nj KUMFUNGA.

Hivyo dawa ya kuwafanya wapinzani wakose cha kuongea ni kuweka Maendeleo na utawala Bora.

Kumbuka hata ustawi wa upinzani ni jukumu la chama tawala.
 
Ni kweli lakini hawa wenzetu humu mitandaoni wamekuwa watu wa kupiga sana kelele kuponda kila kitu yani me naumia sana ki ukweli.

Mkuu kama ni kuumia utaumia sana, huku hamna mbuzi wa kusifia kila kitu. Ww nenda huko vijijini ndio kuna watu wanashangilia chochote. Kama serikali inaendesha udhalimu usipoteze muda wako kusubiri kama utasikia sifa zozote.
 
Hao wanaopinga ni mapandikizi ya mabeberu na sio wengi kiivyo ila wako wamepandikizwa na mabeberu kila mmoja unakuta ana majina tofautitofauti kama 20 au 30 na wanalipwa kwa kupinga juhudi za Rais za miradi ya maendeleo

Nani ana muda wa kumiliki id zaidi ya moja? Hapa unapewa ukweli wako, sifa kasubirieni kwa wasiojitambua na wasaka maslahi binafsi.
 
Wakuu nashindwa kujua shida ni nini.Maana Mh Rais alisema maendeleo hayana vyama sasa kulikoni kila jambo la maendeleo ambalo Serikali inafanya kuna baadhi ya watu wanakasirika na kuombea kabisa hayo mambo yasifanikiwe.

Inajengwa reli ya kisasa ya SGR kuna kuna watu wanaomba mradi usiishe mapema,mradi wa kisasa wa umeme na mengine mengi tu.

Hivi juzi juzi pia serikali imetoa Ajira 1000 za madaktari na pia wameahidi kuajiri walimu lakini ukifatitilia kiundani kuna watu kama hawapendi au wanaumia kuona haya mambo mazuri yakifanyika.Shida ni nini Wakuu?

Ahadi ni Vitendo!

Awamu ya tano,Hapa kazi tu!
JPM kazini!
Nawasilisha!!!
Mpaka itupe majibu rasmi ya mauaji ya lisu yaliyofeli Azory gwanda Ben sanane nk
 
Hatua gani huyu kachukua kwa waliochota pesa za Escrow na mahaka ya ufisadi ilikuwepo?
Ukitaka kuonekana una uelewa, soma maelezo ya wenzako. Umesoma? Kuna watu wanalaumu eti kuna watu wamebabikizwa kesi za uhujumu, wewe tena unauliza mbona watu hawajakamatwa, ni wewe huyo huyo uliyesema watu wanaonewa. JF imekuwa kijiwe cha ubishi, eti! Ukiwa wa hivyo hutaweza kuongeza uelewa.
 
Wakuu nashindwa kujua shida ni nini.Maana Mh Rais alisema maendeleo hayana vyama sasa kulikoni kila jambo la maendeleo ambalo Serikali inafanya kuna baadhi ya watu wanakasirika na kuombea kabisa hayo mambo yasifanikiwe.

Inajengwa reli ya kisasa ya SGR kuna kuna watu wanaomba mradi usiishe mapema,mradi wa kisasa wa umeme na mengine mengi tu.

Hivi juzi juzi pia serikali imetoa Ajira 1000 za madaktari na pia wameahidi kuajiri walimu lakini ukifatitilia kiundani kuna watu kama hawapendi au wanaumia kuona haya mambo mazuri yakifanyika.Shida ni nini Wakuu?

Ahadi ni Vitendo!

Awamu ya tano,Hapa kazi tu!
JPM kazini!
Nawasilisha!!!
Ugumu wa maisha unasababisha hasira zisizo na mpango
 
Ukitaka kuonekana una uelewa, soma maelezo ya wenzako. Umesoma? Kuna watu wanalaumu eti kuna watu wamebabikizwa kesi za uhujumu, wewe tena unauliza mbona watu hawajakamatwa, ni wewe huyo huyo uliyesema watu wanaonewa. JF imekuwa kijiwe cha ubishi, eti! Ukiwa wa hivyo hutaweza kuongeza uelewa.

Patriot hapa jukwaani sio kwenye chumba cha mtihani kwamba utasoma kila comment kwenye uzi fulani. Huwa tunachangia randomly na sio lazima kufanana mawazo na yoyote. Hata hivyo sihitaji kusoma comment za watu wote humu jukwaani ili kujua kuwa utawala huu wa Magufuli unaendesha nchi kwa uonevu wa wazi. Nitakupa mifano kadha kudhihirisha kuwa yoyote ambaye Magufuli anachuki naye binafsi ananyanyaswa, kama ifuatavyo hapo chini.
  1. Magufuli ana nongwa na chuki binafsi na cdm, hivyo anatumia madaraka yake kuwadhalilisha, kuwabambikia kesi cdm, kuwahujumu kwenye chaguzi kwa matumizi mabaya ya madaraka. Pia katika mazingira ambayo hayajathibitishwa hasa kutokana na yeye binafsi kuzuia uchunguzi, wafuasi na viongozi wa cdm wamekuwa wakishambuliwa na vyombo vya dola na watu wasiojulikana hadi kupata vilema vya kudumu na hata kuuwawa, bila yeye kuchukua hatua yoyote kuonyesha haridhishwi na hali hiyo.
  2. Rugemalira na Seth mpaka leo wako ndani, lakini ni dhahiri kabisa sakata lililowaweka ndani walishirikiana na viongozi waandamizi wa ccm na serikali kwenye awamu iliyopita. Mbona hao viongozi waandamizi hawako ndani na kina Seth? Hivi majuzi wakati wa kesi, Rugemalila alimtaka Gavana wa BoT awataje wote waliochota hela za Escrow, mbona kama kweli sio uonevu kwa baadhi ya watu hajawataja mpaka leo?
  3. Hivi majuzi tulisikia Takukuru ikiongea kwa mbwembwe kuwa uchunguzi wa sakata la kina Kange Lugora limefikia 99%, kama sio upendeleo wa wazi mbona hatuoni wakipelekwa mahakamani? Inawezekana vipi wapinzani ndio inatoka amri ya kufunguliwa mashtaka mara moja, hata kwa mambo yasiyo na tija? Kama sio chuki binafsi za rais kwa wapinzani hasa cdm ni nini?
Hivi unatoa wapi nguvu yanl kutetea utawala wenye chuki binafsi dhidi ya kundi fulani la wananchi? Je ninahitaji kupitia kila comment ya mchangiaji huku jukwaani ili kubaini huo ukatili wa wazi?
 
Wakuu nashindwa kujua shida ni nini.Maana Mh Rais alisema maendeleo hayana vyama sasa kulikoni kila jambo la maendeleo ambalo Serikali inafanya kuna baadhi ya watu wanakasirika na kuombea kabisa hayo mambo yasifanikiwe.

Inajengwa reli ya kisasa ya SGR kuna kuna watu wanaomba mradi usiishe mapema,mradi wa kisasa wa umeme na mengine mengi tu.

Hivi juzi juzi pia serikali imetoa Ajira 1000 za madaktari na pia wameahidi kuajiri walimu lakini ukifatitilia kiundani kuna watu kama hawapendi au wanaumia kuona haya mambo mazuri yakifanyika.Shida ni nini Wakuu?

Ahadi ni Vitendo!

Awamu ya tano,Hapa kazi tu!
JPM kazini!
Nawasilisha!!!
Hakuna maendeleo bila amani, uhuru wa mawazo. Hata ukigawa mapesa lkn bila amani, upendo ni bure. Magufuli anachukiwa na watanzania wengi kwasababu ya tabia yake ya kuminya demokrasia, kuua raia wasiyokuwa na hatia, kubambikia wananchi kesi na kuwaweka ndani na kuwafunga.
 
Una uhakika na hayo unayoyasema????
 
waonee huruma tu mkuu kwani hilo ni tatizo la kisaikolojia, wanahitaji tiba badala ya lawama.
 
Mmependekeza nini nyinyi wakati ninyi kila kitu mnapinga
Unaona, tayari automatically hukubaliani na mimi kwa kuwa unajua mie mpinzani. Mie siko huko nakukumbusha tu. Kwa mfano walipendekeza serikali isiingilie suala la ununuaji korosho.

Pia walipendekeza kwamba hatuwezi kutekeleza miradi mikubwa kama SGR na Stiegler kwa hela ya ndani peke yake, hata kama hawakuiunga mkono kwa 100%

Pia wamependekeza kwamba kabla ya kupiga kelele sana na kujikita kwenye uchumi viwanda tuweke mkazo kwenye uzalishaji malighafi ka ku-modernize kilimo

Pia walipendekeza kwamba mfumo wa elimu ufumuliwe na uundwe upya kwa kuwa ni wa kizamani sana na unalenga kufanya watu wasome wapate ajira, na hata hizo ajira hautuandai kuingia kwenye soko la ajira la kimataifa.

Bado unataka mifano?
 
Unaona, tayari automatically hukubaliani na mimi kwa kuwa unajua mie mpinzani. Mie siko huko nakukumbusha tu. Kwa mfano walipendekeza serikali isiingilie suala la ununuaji korosho.

Pia walipendekeza kwamba hatuwezi kutekeleza miradi mikubwa kama SGR na Stiegler kwa hela ya ndani peke yake, hata kama hawakuiunga mkono kwa 100%
Asa Mkuu kwanini miradi inaendelea lakini wao ukifatilia nyuzi zao nyingi humu ndani ni kuombea moradi isikamilike au ichelewe kukamilika wakati uhalisia miradi yottee inaendelea vizuri??? Si hivyo tu hata kwenye mambo mengi mazuri mengi lakini wao ni kutoa kashifa tu kwanini lakinii?
 
Tofautisha kati ya mashabiki wa vyama vya upinzani na wanasiasa wa vyama vya upinzani. Humu JF kuna mashabiki wa CCM na upinzani pia, wengi malofa hawajui hata wanalosema. Sasa ukitaka ku-judge busara za vyama vya upinzani kwa kauli za malofa mashabiki wa upinzani walioko JF una tatizo wewe. Na nashangaa kwa nini unaona kauli za kilofa za mashabiki wa upinzani humu JF lakini za malofa mashabiki wa CCM huzioni.

Na umeisoma signature yangu lakini?

Changamoto kubwa sana inayoyakabili mataifa masikini duniani na kufanya washindwe kuendelea ni nyingi ya akili ndogo kupewa mamlaka makubwa, kwa njia ya kura au kuteuliwa.
 
Achiaga ujinga weye
Wakuu nashindwa kujua shida ni nini.Maana Mh Rais alisema maendeleo hayana vyama sasa kulikoni kila jambo la maendeleo ambalo Serikali inafanya kuna baadhi ya watu wanakasirika na kuombea kabisa hayo mambo yasifanikiwe.

Inajengwa reli ya kisasa ya SGR kuna kuna watu wanaomba mradi usiishe mapema,mradi wa kisasa wa umeme na mengine mengi tu.

Hivi juzi juzi pia serikali imetoa Ajira 1000 za madaktari na pia wameahidi kuajiri walimu lakini ukifatitilia kiundani kuna watu kama hawapendi au wanaumia kuona haya mambo mazuri yakifanyika.Shida ni nini Wakuu?

Ahadi ni Vitendo!

Awamu ya tano,Hapa kazi tu!
JPM kazini!
Nawasilisha!!!

"My pain may be the reason for somebody's laugh,but my laugh must never be the reason for somebody's pain"

Charlie Chaplin
 
Back
Top Bottom