Hivi ni kwanini Jeshi la Polisi halimkamati Mkurugenzi wa wilaya ya Kinondoni kuhusiana na mauaji ya mwanafunzi Akwilina?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Nimejiuliza swali hili kwa muda mrefu kwa kuwa naamini ni lazima Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wake kwa weledi mkubwa ili kubaini chimbuko la tatizo ni nini

Tarehe 16/02/2018 wanachama wa Chadema walifanya maandamano(ambayo kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu ni halali) kwenda kwa Mkurugenzi wa wilaya ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli ili kwenda shinikiza atoe viapo vya mawakala wao, ambavyo kutokana na ukada wake kwa CCM alifanya hila za kutokuwapa hao Chadema, wakati alishawapa wenzao wa CCM

Kama tunavyokumbuka kuwa maandamano hayo yalizimwa kuendelea pale Kinondoni Mkwajuni na Polisi watuliza ghasia kwa mmoja wa askari hao kufyatua "kizembe" bunduki yake, ambapo risasi zake zilimpiga na kumwua mwanafunzi Akwilina Akwiline, ambaye wala hakuwa na hatia ambaye alikuwa kwenye daladala!

Baada ya tukio lile tulimsikia kamanda wa kipolisi wa kanda maalum ya Dar, Athumani Mambosasa, akikiri kuwa wanawashikilka askari wao 6 kuhusiana na mauaji hayo ya "kizembe" yaliyofanywa na mmoja wa askari wake

Cha kushangaza ni kuwa baada ya siku chache tulisikia taarifa nyingine kutoka kwa DPP, Buswalo Mganga, kuwa ameifuta kesi hiyo kwa kile alichokiita kuwa askari "wake" hawakuhusika na mauaji hayo na badala yake wakatuhumiwa viongozi wakuu wa Chadema walioandaa maandamano hayo kuwa ndiyo wanahusika na kifo cha mwanafunzi huyo!

Nilishangazwa sana na taarifa hiyo ya DPP ambayo inapingana na taarifa iliyotolewa awali na Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar kuwa wanawashikilia askari wake 6 kutokana na mauaji hayo

Matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona sasa kwa kiongozi Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini, Freeman Mbowe na mbunge mwenzie wa Chadema, Esther Matiko kuendelea "kuozea" jela kwa kile kilichoitwa .na mahakama ya Kisutu kuwa viongozi hao 2 wameidharau mahakama hiyo!

Tukumbuke kuwa hiyo kesi ambayo Jeshi la Polisi linawatuhumu viongozi wa Chadema ni ya kughushi, kwa kuwa maandamano ya amani kuonyesha hisia zako, yemeruhusiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa Tanzania, ibara ya 20(1) ambayo inasema hivi nikiinukuu "kila mtu anastahili kuwa huru, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine kutoa mawazo yake hadharani" mwisho wa kunukuu

Hivi kwa mujibu wa Katiba yetu ya nchi, Jeshi la Polisi linaweza kueleza Umma wa watanzania ni sababu zipi zilizowafanya Jeshi hilo kuwakamata na kuwafungulia mashitaka, karibu viongozi wote wakuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema??

Hivi hao Polisi huwa hawaangalii chanzo cha tukio lenyewe??

Kwa mujibu wao wenyewe viongozi wa Chadema, walilazimika kuandamana kuelekea kwa Mkurugenzi, Aron Kagurumjuli, wa wilaya hiyo ili awaeleze ni kwanini amevizuia viapo vya mawakala wao, zikiwa zimebaki chini ya Massa 12 hadi kesho yake, ambayo ndiyo siku ya uchaguzi wenyewe??

Tukumbuke kuwa hata kule Afrika Kusini enzi zile za utawala wa kibaguzi, Polisi wa kule walikuwa wakitumia mbinnu hizi hizi za kuwabambikia kesi waafrika weusi na kuiaminisha dunia kuwa hao waafrika weusi ni wachochezi na wasaliti wa maendeleo ya watu wa Afrika Kusini na ndiyo sababu iliyowafanya wamfungulie mashitaka ya kughushi, shujaa wetu wa ukombozi wa Bara hili, Mzee wetu Nelson Mandela na kumhukumu kifungo cha maisha jela kwa makosa ya uhaini!

Ikiwa Jeshi letu la Polisi lingependa kufanya uchunguzi wa tukio zima,ni lazima wangegundua kuwa huyo Mkurugenzi wa Kinondoni ndiye chanzo cha tukio hilo.

Ndipo hapo ninapouliza ni kwanini Jeshi letu la Polisi halijamkamata Mkurugenzi wa wilaya ya Kinondoni na kumuhoji kuhusiana na kitendo chake cha kuhatarisha amani ya nchi kwa kuwapa viapo mawakala wa CCM na kuwanyima wale wenzao wa Chadema??

Maendeleo ya nchi hayana Chama!
 
Subiri awamu fulani ambayo itachemsha viporo vyote na kuliwa...kuwa na subira!
Hakika haya ni maonezi ya hali ya juu kwa viongozi kina Mbowe kuendelea "kuozea" jela wakati Mkurugenzi wa wilaya ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli, ambaye ndiyo chimbuko la tatizo hili akiendelea kula raha uraiani!
 
kuna tatizo Jiwe analitengeneza bila kujua... wanadamu si wajinga kiasi hiko tena waafrika hahahah. Samuel Doe, aliuawa kikatili kutokana na hayahaya, Gadaff, Sankara na wengine walijinasibu kuleta maendeleo ila wakasahau kuwa mwanadamu siyo pet...Now naiona Tanzania yangu ikikosa umoja kisa fikra za mtu na kikundi chake kidogo.. vipi hawa watu hawasomi hata historia?
 
kuna tatizo Jiwe analitengeneza bila kujua... wanadamu si wajinga kiasi hiko tena waafrika hahahah. Samuel Doe, aliuawa kikatili kutokana na hayahaya, Gadaff, Sankara na wengine walijinasibu kuleta maendeleo ila wakasahau kuwa mwanadamu siyo pet...Now naiona Tanzania yangu ikikosa umoja kisa fikra za mtu na kikundi chake kidogo.. vipi hawa watu hawasomi hata historia?
Very true

Hoja hujibiwa kwa hoja majukwaani na sivyo kama anavyofanya huyu jamaa, kwa yeyote anayemkosoa kuwa amekosa uzalendo au ni msaliti anayetumiwa na mabeberu!
 
Kwani mkurugenzi ndo alihamasisha maandamano,akili za nyumbu ziko makalioni daima

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kada wa Lumumba hebu soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 20(1) uone namna maandamano ya amani yanavyoruhusiwa na wao Polisi wanachotakiwa ni kuyapa ulinzi

Hebu nieleze ni sababu zipi ziliwafanya Jeshi la Polisi kuyavunja maandamano yale ya amani, tena kwa kutumia risasi za moto zilizosababisha kuuawa kwa mwanafunzi Akwilina Akwiline??
 
Back
Top Bottom