Hivi ni kwanini ina kuwa hivyo?

Nesindiso Sir

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
379
21
Jiulize haya yanatutokea kila siku.....

LAW OF QUEUE:
Ukibadilisha mstari unapopanga foleni ule uliouacha unakwenda mbio zaidi.

LAW OF TELEPHONE:
Namba unayopiga kwa makosa daima haipo bize (busy)

LAW OF MECHANICAL REPAIR:
Mikono yako inapokuwa michafu pua inaanza kuwasha ili uikune

LAW OF THE ALIBI:
Ukimdanganya bosi kuwa umechelewa kwa sababu gari lako limepata pancha kesho yake utapata pancha kweli

BATH THEOREM:
Ukishajitia maji tu simu itaanza kuita

LAW OF ENCOUNTERS:
Uwezekano wa kuonekana na watu unaongezeka unapokuwa na mtu unayetaka usionekane ukiwa nae

LAW OF THE RESULT:
Unapojaribu kumueleza mtu kwamba mashine yako imeharibika ukiwasha itafanya kazi

LAW OF BIOMECHANICS:
Sehemu inayowasha mwilini huwasha zaidi pale ambapo huwezi kujikuna

THEATRE RULE:
Watu wanaokalia viti vizuri ndio wanaochelewa kufika

LAW OF COFFEE:
Ukikaa tu ofisini na kuanza kunywa kahawa yako bosi atakuita na kukuchelewesha mpaka kahawa yako ipoe.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom