Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Najaribu kujiuliza swali hilo kwa kutafakari sana hivi sababu zipi zinazofanya hao watendaji wakuu hawajajiuzulu hadi hivi sasa nafssi zao licha ya Wizara ya Mambo ya Ndani kuwa ndiyo Wizara inayonyooshewa vidole na Umma wa watanzania kwa hivi sasa kutokana na vitendo vya kuuawa watu bila watuhumiwa kukamatwa, vitendo vya utekaji wa watu bila hao watu kuonekana tena, vitendo vya kuokota miili ya watu kwenye viroba, ni baadhi ya visa ambavyo vinatokea nchi hii bila Watuhumiwa kufikishwa mahakamani.
Hebu tujikumbushe nyuma kidogo mnamo mwaka 1977, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu uwazili wake wa mambo ya ndani kutokana na mauaji yaliyotokea kule Shinyanga.
Ninajiuliza mbona Rais mstaafu alijiuzulu uwaziri kwa tukio moja tu la mauaji, mbona hivi sasa matukio ni mengi sana, hususani yanayohusu kuonewa kwa chama kikuu cha upinzani cha Chadema, mbona watendaji hao wakuu wa Mambo ya ndani wamegoma kabisa kujiuzulu??
Najiuliza swali lingine la pili, ni kwanini basi watendaji hao wakuu baada ya kugoma kuwajibika kwa kujiuzulu, Rais naye anasita kuwatumbua??
Ifahamike pia kuwa haya mauaji yenye mlengo wa kisiasa hapa nchini yeshapata coverage kubwa kwenye vyombo mbalimbali vikubwa vya nje ya nchi
Kwa jinsi tunavyomfahamu Rais wetu ambavyo hana mchezo hata kidogo kwa kutengua wateule wake hata kwa vijikosa vidogo, iweje kwa Jeshi la Polisi ukiwa wajibu wao no 1 ni kuwalinda raia na Mali zao, iweje sasa kwa hawa watendaji wakuu wa Jeshi la Polisi, wanaonekana wazi kuwa wajibu huo wa kuwalinda raia na mali zao "wamefeli" kabisa, ni kwanini Rais anaonekana anashikwa na "kigugumizi" kuwafukuza kazi??
Iwapo yeye Rais aliweza kutengua mara moja uteuzi wa Waziri wa Habari wa wakati ule, Nape Nnauye kwa "kosa" la kuunda Tume ya kuchunguza tukio ls Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa kuvamia studio za Clouds akiwa na askari wenye silaha za moto, tunashangaa hii huruma ya wakati huu ya "kulinda" ajira za watu hao wawili inatoka wapi??
Tungependa Rais wetu achukue hatua za haraka za kuwafukuza kazi Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba na IGP Simon Sirro ili sisi wananchi turejeshe Imani na serilali yake.
Mungu ibariki Tanzsnia