Hivi ni kwanini Gharama za Wakili ni kubwa hapa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kwanini Gharama za Wakili ni kubwa hapa Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Jun 29, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa sasa hapa Tanzania Uwakili ni dili,ukiwa na Kesi inayohitaji Wakili unafikiria mara mbili maana gharama za Wakili ni kubwa sana.Na hata hali ya kifedha ya Mawakili ni si haba hapa Tanzania.Vilevile kuna tetesi kuwa Mawakili wa pande mbili hukubaliana na hivyo kula fedha pande mbili.Sasa si ni wakati wa kuweka mazingira mazuri ili msaada wa Wakili katika kesi iwe na gharama nafuu ili wananchi waweze kusaidiwa kisheria.Wana JF wanasheria kwanini Gharama za mawakili hapa Tanzania ni za gharama kubwa?
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  DEMAND and SUPPLY fix the price
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jun 29, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Unaposema kubwa unalinganisha na nini? Unamaanisha kazi wanayofanya haiendani na malipo au kwa kuwa simply wananchi hawana kipato cha kutosha? Kama wananchi walio wengi hawana kipato cha kutosha basi hilo sio kosa la wakili ni la wananchi wenyewe na serikali yao. Hilo suala la kula dili la mtu mmoja moja kama lipo na ni utovu mkubwa wa kiapo cha utumishi katika uwakili!
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  gharama za wakili tanzania ni za kawaida sana, Anyway hujasema ni ghali kwa vipi, kuliganisha na nchi gani kwa aina gani ya kesi labda ufafanue.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,174
  Trophy Points: 280
  Gharama za wakili bongo bado ni za kawaida tuu, nchi zilizoendelea hata kupangisha nyumba tuu lazima wakili fungu nene.
  Gharama za wakili Tanzania zinadhibitiwa na sheria ya mawakili, hawalipwi zaidi ya asilimia 4 ya gharama halisi.
  Kuna vituo kibao vya misaada ya kisheria kwa wasio na fedha, hivyo unapatiwa wakili bure.
  Kesi zote za capital punishment, ambazo hukumu zake ni kifo, kama kesi za mauaji na uhaini, serikali inakuwekea wakili wa kukutetea ambaye analipwa na serikali yenyewe.
  Mambo ya mawakili ndio kwanza wameongezewa ulaji tangu leo, Waziri wa Katiba na Sheria ameliambia Bunge, mahakimu wote wa mahakama za mwanzo sasa ni wahitimu wa degree ya sheria, hivyo mambo ya mawakili sasa ni toka mahakama ya mwanzo!.
   
 6. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  "Gharama halisi" za nini, una maana damages zitakazo kuwa awarded kwenye kesi ya madai?

  Mkuu, Pasco, tutajie, tafadhali, kipengele cha hiyo sheria inayosema mawakili wasilipwe zaidi ya "asilimia 4 ..."
   
  Last edited: Jun 30, 2009
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jun 30, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kweli! Ukitaka mjadala unoge ni kuleta data toka reliable sources. Ukileta hisia hutaeleweka!
   
Loading...