Hivi ni kwanini Dr. Slaa na Mbowe huwa hawatoi matamko ya kufariji waathirika kunapotokea majanga?

Status
Not open for further replies.
Lukosi,
Unataka Tamko gani zaidi ya wawakilishi wetu waliokuwa kwenye eneo la tukio na kuwaomba wananchi wachangie Damu. Au unatafuta tu maneno. Wananchi Jana hawakuchangia damu, uliwaomba wewe, au ile Damu iliteremka kutoka angani? Tatizo ni nMna yako/yenu ya kufikiri na kuona mambo.

Lukosi ni Mkosi, hana fikra...
 
Wao wanachojua ni maandamano tu,
Mimi nina uhakika chadema hufurahia wanapoona majanga yanaikumba nchi yetu ili wapate cha kuongea majukwaani.
Wanatumia maisha ya watu kama mtaji wa kisiasa

24/7 unawaza CHADEMA, Dr Slaa na Mbowe, pole sana ndg na hao ulionao huko naamini wanapata taabu isiyo kifani.
 
naamini siku mkipata madaraka pia mtakula komaeni na maandamano milipuko n kusingizia watu mauaji sijapata adala ya ccm jamaniiiiiiiiiii :help:

umebanwa na mkojo. nenda kasusu halafu ukalale mtoto. hiyo alfu saba unanunulia nini yote? pipi kijiti?
 
Lukosi,
Unataka Tamko gani zaidi ya wawakilishi wetu waliokuwa kwenye eneo la tukio na kuwaomba wananchi wachangie Damu. Au unatafuta tu maneno. Wananchi Jana hawakuchangia damu, uliwaomba wewe, au ile Damu iliteremka kutoka angani? Tatizo ni nMna yako/yenu ya kufikiri na kuona mambo.
Dr Shikamoo,

Nashukuru kwa kuja kunijibu.

Mimi nakuomba wewe kama kiongozi wa wananchi na wanachama wengi wa chadema ambao wengi wanaamini utakuwa Rais wao. Ujitokeze kwenye vyombo vya habari kama vile magazeti na television kutoa tamko la chama kama sio lako binafsi ili kuwapa faraja waathirika ambao naamini wengine ni wafuasi wako.
Ninasema hivi kwa sababu jana mlimuachia Lema akashindwa kutoa tamko lenye kujenga bali alianza kubomoa mpaka redio maria wakamkatiza.

Kama ujuavyo mimi ni mkatoliki kama wewe na ninasali Rozari walau mara mbili kwa wiki, na tunajifunza katika dini yetu kusamehe na kudumisha upendo
Kama ujuavyo katika ile sala aliyotufundisha baba yetu huwa tunasema hivi

"TUSAMEHE MAKOSA YETU, KAMA TUNAVYOWASAMEHE NA SISI WALIOTUKOSEA"

Lema alikosea na nilitegemea wewe ambaye ndio political power ya Chadema ujitokeze kwenye vyombo vya habari kutoa
tamko lenye weledi.

Samahani kama nimekukwaza lakini nadhani wewe mwenyewe hukupendezwa na tamko la kijana wako jana.

Wewe umesomea upadri na unajua kabisa kanisa katoliki linafundisha nini.

Nimeona ujumbe wako kwenye facebook page yako lakini face book haiwafikii wengi na sio kila mtu anaingia facebook.

Nakuomba kwa manufaa ya taifa letu na vizazi vijavyo, ujitokeze ukemee uchochezi wa aina yoyote na uwaombe watanzania watulie waisaidie polisi kwenye upelelezi wa tukio hili hatari kwa taifa letu.

Mimi mkatoliki, na nimeumizwa sana kuona wakatoliki wenzangu wanauawa wakati wa ibada, lakini nisingependa kuona wakatoliki nao wanaingia mitaani kuanza kulipiza visasi baada ya kusikia kauli ya kiogozi kama Lema
 
Ndugu zanguni,

Nchi yetu imekumbwa na mlolongo wa matukio ya maafa siku za karibuni suala ambalo tunahitaji watanzania wote tuungane kuombeana amani na upendo na pia kuwaombea waliathirika na kuwapa faraja.

Cha kushangaza viongozi wa chama kikuu cha upinzani chadema wamekuwa kimya kila yatokeapo haya na matokeo yake ndio wanawaachia waropokaji watoe matamko kama alivyofanya Lema jana.

Mimi nataka niwaulize Dr Slaa na Mh Mbowe. Jee ,mnafurahia yanayotokea mkitegemea wananchi kuichukia serikali? au ndio tuseme hamna uchungu na waathirika?

Lilianguka ghorofa Dar lakini hatukuona hata mmoja wao akienda kwenye tukio au kutoa tamko zaidi ya Mh Mbowe kutoa comments kwenye facebook

Leo bomu limelipuka na watu wamepoteza maisha Arusha lakini kimya mpaka sasa.
Naomba ufafanuzi hapa.

Au Chadema inafurahia pale tunapopatwa na majanga ili waje pata cha kuongea kwenye majukwaa ya siasa?

Mkae mkijua kuwa hao magaidi wataendelea kuwepo hata kama mtachukua nchi. Ssiku zote serikali yoyote duniani hukumbwa na matatizo ya namna moja au nyingine kwani binadamu wote hawako sawa na kuna wengine maisha yao wanawaza kuua tu. Pia mkumbuke kuwa maghorofa hayatawaogopa mkiwa watawala kama yalijengwa vibaya yatabomoka tu

Chadema mnatutia mashaka watanzania

JITAMBUE!
Mkuu hao jamaa ni kizazi cha nyoka, wao ni sumu tu!!!!!
 
Tanzania bila matamko kwenye majanga inawezekana, chukua hatua ya kupambana haya yasitokee badala ya kutoa matamko yasiyotibu majanga.
 
Kuna mtu mmoja tu Kwenye safu nzima ya Chadema ambaye anapiga Siasa kwa maendeleo ya taifa na sio sifa wala njaa.

Mheshimiiwa Philemon Ndesamburo,

Huyu kwangu mimi he is an iconic figure na ningependa niwe Kama yeye in politics and business wise in general
Dr Slaa napenda harakati zake alipokuwa Mbunge lakini kwa SASA Ni Kama vile inabidi afuate Siasa za Mbowe hata Kama hazipendi kwa sababu Mbowe Ndio Chadema,
Money talks!

Aliyewahi kusema akili yaknj "inaugua" alisema kweli , judging from your comments unaonekana unaripuka tu bila kujua ulipoanzia na unaenda kuishia wapi, mara kuna mtu mmoja tu CHADEMA Ndesamburo, mara namu admire Dr. Slaa, una shida gani Lukosi!!?
 
..........wakijitokeza kusema munasema wanatafuta umaarufu wa kisiasa, wakinyamaza munawashangaa......na ukumbuke ndugu Lukosi ukilia sana msibani haina maana wewe ndio una uchungu sana la hasha!

Serikali ya CCM imeshasema sana yanapotokea majanga lakini hakuna kinachobadilika, kule zanzibar wametoka mate na mapovu mdomoni....tunakemea, lazima wakamatwe,tutaita fbi na maneno chungu mbovu werevu tukajua hapa tunazugwa, sasa tena limetokea hili ona wanavyopishana huko Arusha na matamko lukuki, werevu wamenyamaza wana uchungu ila ndio wafanye nini SERIKALI imetia magunzi masikioni na bongo zinawawaza Dr Slaa na Mbowe, lini chadema itakufa....upuuzi.

Jengo limeporomoka Mheshimiwa Rais akiambatana na wife wake wameenda kutoa pole, tunashukuru kwa hilo, Mheshimiwa akatoa agizo waliohusika na uzembe wote wawajibishwe, kilichotokea mpaka mara ya mwisho nasoma kwenye vyombo vya habari kuna mtendaji mmoja wa Serikali anahusika na huo uzembe lakini bado yupo ofisini na gari letu la ofisi anatumia.

Si hayo tu tayari pameshasemwa majengo yaliyo chini ya viwango yapo mengi na yanajulikana, wataalamu wamesema yavunjwe.....hembu niambie ndugu Lukosi lipi mpaka sasa limevunjwa? wanasubiri yaanguke watoe matamko na Pole......upuuzi.
 
Lukosi,
Unataka Tamko gani zaidi ya wawakilishi wetu waliokuwa kwenye eneo la tukio na kuwaomba wananchi wachangie Damu. Au unatafuta tu maneno. Wananchi Jana hawakuchangia damu, uliwaomba wewe, au ile Damu iliteremka kutoka angani? Tatizo ni nMna yako/yenu ya kufikiri na kuona mambo.

Dr. Umejibu kwa upole kana kwamba wewe ndio ulierusha bomu.

Mungu akujalie hekima na unyenyejevu.
!!
 
Dr. Umejibu kwa upole kana kwamba wewe ndio ulierusha bomu.

Mungu akujalie hekima na unyenyejevu.
!!
Mkubwa mimi sio Chadema lakini naamini Dr sio Llema na ndio maana nikamuambia mtu hapa awe na adabu pale alipomfananisha Dr na Lema.

Ukiacha siasa, Dr ni mtu makini lakini mazingira ndiyo yanayomfanya sometimes aonekane kama wao
 
Hawa akina Slaa na Mbowe ndiyo tunasema waje kuchukua nchi, naona tayari wameshaanza kuchelewa kutoa kauli na maamuzi kwenye issue nyeti kama hii. Eti wanawaza long term solution! Mpaka ikifika 2015 watamtawala nani kama nchi ishavurugika? Mimi nashangaa watu wanatoa kauli za kufananisha utawala wa Mwinyi, Mkapa, na Mwalimu hakukua na kauli za udini!
Rudia press conference ya Mwalimu pale Kilimanjaro Hotel "Nyufa nne" RUSHWA, UDINI, MUUNGANO, UKABILA. Hata wakati wake Mwalimu alishutumiwa kwamba amechagua mawaziri wengi wakatoliki, aliyazungumzia yote haya mwenyewe. Mnataka kutuambia anayeshutumiwa ndiyo anakuwa M-DINI?
 
Aliyewahi kusema akili yaknj "inaugua" alisema kweli , judging from your comments unaonekana unaripuka tu bila kujua ulipoanzia na unaenda kuishia wapi, mara kuna mtu mmoja tu CHADEMA Ndesamburo, mara namu admire Dr. Slaa, una shida gani Lukosi!!?
Na ndiyo utashangaa leo MwanaCCM kutomsifia Zitto Kabwe, anyway kwa sababu bado yuko chini ya uangalizi wa Dr Pauline basi tumvumilie huyu mgonjwa wetu.
 
Ila we jamaa ni mav. kweli kwani wakitoa matamko ndio majanga yataisha. suala ni kufikiria ni jinsi gani ya kuyaondoa hayo majanga. na njia mojawapo ni kuiondoa ccm madaraka kwani majanga mengi ni kwa sababu ccm ipo madarakani. . Yana sababishwa directly or indirect na ccm.
Soma vizuri uelewe,

Chadema ndio Chama kikuu cha upinzani nchini, hivyo ni kawaida kwa nchi yenye demokrasia viongozi wakuu wa upinzani kujitokeza na kuungana na taifa zima kwa kutoa tamko maalum kuwafariji na kuwapa moyo waathirika.

Huwezi kujiita kiongozi wa wananchi halafu kunapotokea majanga unakula kona, huo ni unafiki mbaya sana
 
Aliyewahi kusema akili yaknj "inaugua" alisema kweli , judging from your comments unaonekana unaripuka tu bila kujua ulipoanzia na unaenda kuishia wapi, mara kuna mtu mmoja tu CHADEMA Ndesamburo, mara namu admire Dr. Slaa, una shida gani Lukosi!!?

Unahangaika na mgonjwa wa akili,
yeye akiongea neno anasahau ndio maana haeleweki,mpuuze tu.
 
Hivi nyie watu kwanini mnakuwa mamburura hivyo matamko yanasaidia nini kwani jk anavyotoa matamko majanga ndio yameisha/ Muwe watu wnye kufikiri.
Hawa akina Slaa na Mbowe ndiyo tunasema waje kuchukua nchi, naona tayari wameshaanza kuchelewa kutoa kauli na maamuzi kwenye issue nyeti kama hii. Eti wanawaza long term solution! Mpaka ikifika 2015 watamtawala nani kama nchi ishavurugika? Mimi nashangaa watu wanatoa kauli za kufananisha utawala wa Mwinyi, Mkapa, na Mwalimu hakukua na kauli za udini!
Rudia press conference ya Mwalimu pale Kilimanjaro Hotel "Nyufa nne" RUSHWA, UDINI, MUUNGANO, UKABILA. Hata wakati wake Mwalimu alishutumiwa kwamba amechagua mawaziri wengi wakatoliki, aliyazungumzia yote haya mwenyewe. Mnataka kutuambia anayeshutumiwa ndiyo anakuwa M-DINI?
 
Wako na pressure kuwa issue inaweza kubumburuka ndo maana wanakuaga kimya.
Wao wanachojua ni kuwataka watu wajiuzuru ,ndo zao.

ukitoa tamko ndio kumaliza tatizo, hujajiuliza mbona miskiti hailipuliwi na mabomu, hau unawadhihaki wahanga? dont be silly for real issue..**¤§
 
Ila we jamaa ni mav. kweli kwani wakitoa matamko ndio majanga yataisha. suala ni kufikiria ni jinsi gani ya kuyaondoa hayo majanga. na njia mojawapo ni kuiondoa ccm madaraka kwani majanga mengi ni kwa sababu ccm ipo madarakani. . Yana sababishwa directly or indirect na ccm.
Sasa matusi ya nini?
Viongozi wako wapo hapa na hadi muasisi wa Chadema anasoma unayoandika, je unadhani anafurahia lugha yako?
JITAMBUE
 
mimi najitolea mifuko hamsini ya sabuni...umeambiwa wao ni wachafu!? CCM endeleeni kutoa misaada na pole wakati wa matukio badala ya kudhibiti vyanzo vya matukio ipo cku tutawafukuza na rais wenu kwenu misiba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom