Hivi ni kwanini Cocacola inaendelea kutangazwa wakati hakuna wanachoongeza wala kupunguza kwenye soda hiyo?

Wanawekeza sana kwenye matangazo wakati ilihali wanaotengeneza na kusambaza soda wana hali ngumu kweli na pia hata magari yao ni mabovu,iyo hela wanayoitoa kwa ajili ya matangazo basi kidogo wawafikirie wafanyakazi wao
 
Jina la 'COCACOLA' limetokana na ingredients kuu za soda hiyo, nazo ni 'COCA' leafs na 'KOLA' nuts, hizo 'COCA' leafs ndio hutumika kutengeneza madawa makali ya kulevya aina ya 'COCAINE' ambayo ni very addictive. Anyway, utamu wa aina hii ya 'COCAINE' (Cola cocaine a.k.a cocacola) ni ule ule kote duniani.
Usibishe, kuna utofauti. Maji ya Moshi ni mazuri zaidi, yanafanya Coca Cola ya Moshi iwe tamu zaidi. Pili, Coca Cola does not contain cocaine, it contains caffein, sawa na chai na kahawa.
 
Ni zaidi ya miaka 100 sasa cocacola imekuwa ikitangazwa kwa nguvu sana duniani kote. Lakini kwa miaka yote hiyo, hakuna chochote kilichoongezwa wala kupunguzwa kwenye soda hiyo, ladha ni ile ile duniani kote kwa miaka yote. Sasa wanachotangaza kila siku tena kwa nguvu as if ndio wana launch kinywaji kipya ni nini? Kuna nini kilichojificha kwenye aina hii ya sumu?
Atleast kampuni kama za simu utasema wame launch kifurushi kipya hivyo wana kitangaza, lakini soda hii haina whatsapp wala facebook bure useme eti wanakitangaza..
Soda hii imeua watu wengi sana kwa kemikali ya cafein....
 
Matangazo ni lazima ili waendelee kuwa juu kibiashara.

Pia Coke wametoa Coke zero, na coke za aina nyingine sio kweli hamna aina nyingine , na mbona umesema coke tuu ... pepsi vipi?
 
Biashara ni matangazo mkuu,, pamoja na ukongwe walionao ktk biashara lakini wanafahamu kuwa wana washindani wengi duniani kote kwahiyo lazima waendelee kujitangaza ili kulinda soko la bidhaa zao na hata kuliongeza..
 
Jibu ni very simple...Watu waliokuwepo miaka 100 bado wapo leo hii? Je unajua Coca cola anawashindani kwenye soko. Biashara ambayo huitaji matangazo ni ile ya monopoly, mfano Tanesco, DAWASCO . Lakini wakitokea washindani tu itabidi wabadili mbinu. Jaribu pia kusoma vitabu vya entrepreneuship na marketing in general unaweza pata mwanga zaidi.
 
Jibu ni very simple...Watu waliokuwepo miaka 100 bado wapo leo hii? Je unajua Coca cola anawashindani kwenye soko. Biashara ambayo huitaji matangazo ni ile ya monopoly, mfano Tanesco, DAWASCO . Lakini wakitokea washindani tu itabidi wabadili mbinu. Jaribu pia kusoma vitabu vya entrepreneuship na marketing in general unaweza pata mwanga zaidi.
Kama hawana mshindani mbona wanapata hasara na kudai ruzuku kila mwaka?
 
Kama hawana mshindani mbona wanapata hasara na kudai ruzuku kila mwaka?
hayo ni mengine sasa. Kama hujui sababu ya wao kupata hasara then it is not even worth discussing here. Yaani unahama kwenye hoja yako mwenyewe. Hebu rudia kusoma nilichoandika uelewe vizuri. Be a good listener...
 
Back
Top Bottom