Hivi ni kwanini bodi ya mikopo mnamchonganisha mtukufu Rais na wapigakura wake ?

Mwemary

JF-Expert Member
May 25, 2016
330
340
Wanajamvi napenda kuliezea hili kwa masikitiko makubwa kuhusiana na BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU (HESLB) jinsi gani inavyopingana na sera ya Rais wetu kipenzi ya Hapa kazi tuuuu. Haya ni maneno ambaya Rais wakati anahutubia bunge alisisitiza mambo ma2 ambayo hatayavumilia kuyasikia katika awamu yake. laKwanza tupo kwenye upembuzi, la pili tupo kwenye mchakato mhe Rais alisema hapendi kuyasikia maneno haya.

Hebu turudi nyuma kidogo bodi ya mikopo ilianza kupokeaa maombi tarehe 23 may na kusitisha tarehe 30 July. Na wakasisitiza mambo yote yafanyike online kisha kutumiwa form for further certification of addition details. Wakati huo huo TCU wenyewe walifungua maombi yao tarehe 15 July mpka 30 August. Ilipofika tarehe 9 septemba wakatoa waliofanikiwa awamu yakwanza nakurushu awamu ya pili waanze kuomba.

Nawaliopata awamu ya pili majina yameshatoka sasa hivi wameruhusu awamu ya tatu na muda sipunde watatoa majina ya waliopata. Sasa turudi bodi ya mikopo sijui kunanatatizo gani mpaka sasa inaonekana hawa watu wa bodi walianza kufanyia kazi form za waombaji baada ya kusikia vyuo vinafunguliwa.

Muda wote walikuwa wapi wanatuambia majina elfu 7 ndo yamekamilika hv hawa watu wanastahili kubaki katika ofisi hiyo mhe Rais.Tumbua kuna vijana wengi wa IT tuko mtaani tunatafuta kazi. Hao watu wa bodi walishazoea kufanya kazi kwa mazoea. Hebu mtukufu Raisi wetu liangalie kwani unachonganishwa na wapiga kura wako.

Hebu tujiulize hv hao designer wa website LOAN BOARD Waliwatoa wapi? Mara unaambiwa haujaomba, mara form haijafika kwahiyo website ni magumashi? Walioomba mkopo ni karibia wanafunzi 60000 halafu kila bechi mnatoa wanafunzi 4000 je situtafika mwezi 6 mwakani ndo mnamaliza?

Hebu waoneni huruma watoto wa wakulima jamani? Vyuo vya UDSM, SUA , MUM, SAUTI, Jamani mbona wameshafungua?
 
Wewe mchakato kati ya TCU na BODI panatofauti kubwa sana,HESLB fomu moja inafanyiwa mambo mengi kuliko TCU na baadhi ya vipengele heslb hawawezi kuvifanyia kazi mpaka TCU wamalize na watume majina HESLB hivyo usilinganishe kazi za TCU na HESLB,Kwa mfano hawawezi kufanya allocations bila TCU Kupeleka majina ya wanafunzi walio pangiwa vyuo Heslb, cha msingi tusubri na serikali yenyewe hii imekua kigeugeu,mwakajana walimwaga mikopo ili wapate kura mwaka huu mmmmh! tutalia
 
Daaa
Wewe mchakato kati ya TCU na BODI panatofauti kubwa sana,HESLB fomu moja inafanyiwa mambo mengi kuliko TCU na baadhi ya vipengele heslb hawawezi kuvifanyia kazi mpaka TCU wamalize na watume majina HESLB hivyo usilinganishe kazi za TCU na HESLB,Kwa mfano hawawezi kufanya allocations bila TCU Kupeleka majina ya wanafunzi walio pangiwa vyuo Heslb, cha msingi tusubri na serikali yenyewe hii imekua kigeugeu,mwakajana walimwaga mikopo ili wapate kura mwaka huu mmmmh! tutalia
Daaaaah nimesikia UDSM wamesitisha Udahili mpk loan board wapeleke majina hao ndo wanaume sio wakuu wa vyuo vingine full kujipendekeza na unafiki daaaahhhh huyo Razak sijui wamemugotea wapi anakwambia kila serikali ina kipaumbele chake serikali kipaumbele chake ni viwanda haya mmejenga viwanda vingapi mapunguani nyinyi?
 
Back
Top Bottom