Hivi ni kwanini Baraza Kuu la CCM liliwaita na kutaka kuwahoji akina Membe na kumwacha Musiba?

Kwenye sheria ni lazima unapohitaji haki itendeke uhusishe pande zote ili uujue ukweli na ufanye uamuzi usiopendelea upande mmoja

Nimesikia kwenye kikao cha baraza kuu la CCM kilichomalizika siku chache zilizopita, huko Mwanza, kuwa kimeamua kuwaita akina Bernard Membe, Abdurahman Kinana na Yusufu Makamba kuwahoji kuhusu tuhuma zinazowakabili za kuvuja kwa sauti zao kwenye audio clips

Nina maswali machache ninataka kuwauliza hao wajumbe wa NEC walioazimia azimio hilo

1. Ni kwanini muwaite akina Membe na kutaka kuwahoji wakati mmeacha kumuita Musiba, ambaye ndiye "root cause" ya haya yote yanayotokea ikiwa mnatafuta haki itendeke kwa kusikiliza pande zote za mgogoro huo?

2. Hivi "privacy policy" haipo tena nchini Tanzania, ambapo mtu analindwa kisheria katika maongezi yake ya faragha??

3. Mnawezaje kuwa nyinyi baraza la CCM kuwa ndiyo waamuzi wa kesi hiyo, wakati mnajua kabisa kuwa mnakiuka "principle" kuu ya "natural justice" inayosema "You can't be a judge in your own case"

4. Hivi kwa kitendo kilichofanywa na baraza la CCM, siyo kinazidi kuthibitisha shutuma za wananchi walio wengi kuwa huyo Musiba anakingiwa kifua na anatumwa na mtu mzito sana ndani ya nchi hii kutoa hizo shutuma zake zisizokuwa na ushahidi??

Hili Taifa kama linafanya maamuzi yake kwa ubaguzi wa waziwazi kabisa, katika kuwashughulikia wahusika wake linalowatuhumu, kama huu tunaouona sasa tujue kama Taifa tupo hatarini kusambaratika

Naomba nijibiwe kwa hoja, wala si kwa kutoa povu
Mkiitwa muwe makini@malima@arsenic
 
Mimi siko CCM wala Chadema

Kuuliza kwangu ni kwanini NEC ya CCM inawaita akina Membe na kunwacha Musiba, ni kwa kuwa nataka haki itendeke na naamini kuwa huyo Musiba ndiyo "root cause" wa haya yote yanayotokea

Kitendo cha CCM kufanya ubaguzi na kuwaonea baadhi ya watu, kitasababisha Taifa hil lisambaratike. OVA
Swali la ovyo

Musiba aitwe kwa kosa gani?

Kwenye zile audio hatujamsikia musiba ,akimtukana Jpm , sasa aitwe kwa kosa gani?

Mm nikajua kwann asipongezwe kwa kufichua wanaomuhujumu RAIS
 
Wahojiwe leo kesho utahojiwa wewe unayewahoji - tusiendekeze viongozi wetu kutukanwa, kudharauriwa na kufanywa daraja

Haitatokea tukapata kiongozi asiyekuwa na udhaifu hivyo kukosoana sana tukuache na kuijenga CCM yetu
 
Kwani Musiba amekuwa kigogo wa CCM?na je aitwe na CCM kwa kosa gani na akiwa kama nani?
Kwani mmewaita akina Membe kama vigogo wa CCM au kutokana na tuhuma zao wanazikabiliana nazo?

Wewe unadai kuwa Musiba ni mtu mdogo, lakini unajua kuwa yeye ndiye "root cause" wa yote haya yanayotokea?
 
Back
Top Bottom