Hivi ni kwa nini wasomi wenye background ya sayansi na engineering ndio wanaofanikiwa sana kibiashara?

Ni kweli kuwa Engineer au mwanasayansi kuna vitu vingi unajua. ila kikubwa nachojua mimi ni watu hawa wengi wanajua kutafiti vizuri na reasoning ya kwanini nifanye hivi au kwanini nafanya hii biashara au kwanini nisiongeze na kupunguza hiki na sababu yake ni nini

Tuchukulie mfano engineer wa majengo anapojenga jengo ikitokea ameweka nguzo ya zege katika eneo fulani kwenye nyumba inatakiwa awe na sababu ya msingi ambayo inamfanya aweke hio nguzo na sababu hiyo inatakiwa kutetewa na hoja ya kimahesabu ya kuthibitisha mafanikio ya ubora katika hio nguzo kwamba itastahimili au itafeli

Sasa basi tukiludi kwenye uhalisia wa maisha upande wa mafanikio na biashara kwa reasoning ya mtindo huo inamfanya kila analofanya lazima ahoji na kujipa majibu ya maelezo na kimahesabu yaliyo sahihi kabla hata ya biashara au project kuanza. hivyo kupelekea kufanikiwa kwa kipindi kirefu

Sasa ukija kwa watu nje ya fani hiyo sio kwamba hawafanikiwa hapana. Mafanikio yako popote sayansi ni njia tuu. Huku unakuta mtu anafanya biashara kwa kufuata trending business (biashara zilizoshika kasi kwa kipindi fulani) hivyo kumfanya kuwa mtu anayefanya biashara pasipo tafiti. Na ukifanya biashara kwa mtindo huu inakuhitaji uwe na uwezo wa kubadilika kwa muda mfupi kama trendline itabadilika kuelekea uelekeo tofauti

Hivyo unamkuta mtu ni mfanya biashara mzuri anafilisika ndani ya mda mfupi sababu ya kukosa tafiti. Na uwezo wa kubadilika pamoja na teknolojia ya kumuwezesha kubadilika mapema.

Thanks
 
sababu wote tuliosoma science wale PCM wenzangu huwa tunakua na IQ kubwa kwenye uelewa wa mambo mbalimbali hata uwezo wa kufikiria na kutatua changamoto za maisha
 
Back
Top Bottom