Hivi ni kwa nini wafanya kazi wanaolipa kodi hawapewi namba za tin ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kwa nini wafanya kazi wanaolipa kodi hawapewi namba za tin ?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kaangwa, Jun 24, 2012.

 1. kaangwa

  kaangwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ninawasalimu wanajamii forum wote mnaosoma na kujadili mambo muhimu sehemu hii
  Nitangulie kuomba samahani huenda issue hii ilishajadiliwa humu lakini mimi kwa kiasi fulani bado ni mgeni,hivyo sijaiona lakini inanitatiza naomba kwa wenye ujuzi na ufahamu ktk nyanja hii wanielimishe.
  Mimi ni mfanya kazi ninayekatwa kitu inaitwa(PAYE) na kwa mwaka nalipa si chini ya 3,600,000/= ,sijawahi kusikia mtu ananiulizia TIN,lakini ninapoenda kure-new,leseni ya gari ambapo fedha ninayolipa haifikii hata 50000/= baada ya miaka 3 au ninapolipia road licence ya gari kiasi cha 100000/= kwa mwaka nadaiwa TIN,hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa kanuni inayotumika hapa.
  Niliambiwa maana ya TIN ni ''tax payer identification number'' nilidhani ukishakuwa na hii number kila kodi unayolipa inaingizwa kwenye number hiyo,lakini nimekuta ninakokatwa fedha nyingi namba hii haitumiki,ninakolipa fedha kidogo inatumika,jambo hili linanichanganya.Mwenye utaalam na mambo haya naomba aniondolee ujinga huu.
  Naomaba kuwakilisha
   
 2. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kuwa TRA hawatupi wafanyakazi tunaolipa PAYE, TIN (namba ya mlipa kodi. Mfanyakazi analipa kiasi kikubwa kuliko wafanyabiashara lakini hatupewi TIN nadhani hili ni kosa.
   
 3. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  TIN unayo sema wewe huifahamu namba yako, ila wao kule wanayo ukiomba wanakupa.
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapana.

  Unapolipa PAYE ni mwajiri ndiye anayeonekana kana kwamba kalipa na sio mfanyakazi binafsi. Fomu za PAYE wanazohaza waajiri hazioneshi majina wala idadi ya walipa kodi hiyo bali huonesha tu kiasi kilicholipwa.

  Nakubaliana na mleta mada, tunahitaji kupewa TIN. Majirani zetu Kenya nadhani wameanza hii kitu
   
 5. GP

  GP JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  daaah, asee mleta mada kaona mbali, kweli wewe ni great thinker!,
  ni kweli nafikiri serikali iliangalie hili jambo kwa jicho la tatu, watu tunalipa PAYE why hatuna TIN?.
   
 6. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  wadau mwajiri ndo anatakiwa kupeleka hayo makato ya kodi (paye) yeye anakuwa "withholding agent" kwa tafsiri isiyo rasmi wakala wa kodi ya zuio,katika form anazojaza ili kuwasilisha hayo malipo yake TRA kuna sehemu anajaza tin namba yake hata kwa malipo ya kielektroniki (electronic fund transfers/TISS etc) mara malipo yanapohamishwa kwenda kwenye account ya TRA unatakiwa upeleke nakala ya malipo yako kwa ajili ya kumbukumbu zao.

  Ingawa kwa kiasi kikubwa mfumo huu unategemea kwa kiwango kikubwa sana uaminifu wa mwajiri kwani anaweza akapeleka malipo pungufu au akawa na payrolls mbili na kwakweli ni mara chache sana maofisa wa TRA wakapita kila ofisi kukagua hizo payrolls na kubaini madudu hayo hivyo tunasafari ndefu sana huko tuendako mpaka kufikia nchi ya ahadi.
   
 7. mito

  mito JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,607
  Likes Received: 1,979
  Trophy Points: 280
  kaangwa asante sana kwa kuliona hili, nadhani ni muda muafaka wa kulipigania. Wakati new financial year inapoanza, wangeangalia na hii kitu, tena na hivi bunge linaendelea nadhani ndo penyewe.
   
 8. kaangwa

  kaangwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu,ila nadhani sina sababu ya kuomba kujua hiyo namba tofauti na ninapoenda kulipia kitu kingine ilitakiwa wao(TRA) waibaini namba yangu na kuniingizia malipo yangu.kwa sasa ukienda kulipia kitu kingine pamoja na kwamba unalipia PAYE kwa muda mrefu unaulizwa namba yako ta TIN na ukisema sina wanakwambia ufungue na kweli unafungua,je unataka kuniambia wanapokusajili unakuwa nazo 2? yaani ya PAYE na hiyo unayosajiliwa kulipia hilo jambo lingine? Na kama ndivyo basi mfumo wanaoutumia ni mbovu kama unaweza kuwa na utambulisho wa mlipa kodi zaiodi ya 1na majina yako ni yaleyale.
   
 9. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2013
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kaangwa,

  Unachosema ni sahihi, na hili ni pungufu moja kubwa la mfumo wetu wa kodi. Mchango wako kama mfanyakazi hauonekani, badala yake ni mwajiri ndiye anayeonekana kalipa kodi.

  Halafu baadae ukienda kusajili TIN ya biashara (hususani biashara ndogondogo ambayo hutunzi mahesabu kitaalam) wanakuuliza eti mtaji umetoa wapi na usipojitetea vizuri utatozwa kodi mara mbili kwa kipato kile kile (yaani cha mshahara wako).
   
Loading...