Hivi ni kwa nini Israel ni mwanachama wa UEFA?

geometry

JF-Expert Member
Oct 30, 2014
466
356
Nimekuwa nikijiuliza hili swali,inajulikana kijiografia israel je kwa nin ni mwanachama wa uefa?
kwa yoyote anaejua anijuze
 
Wapo huko kisiasa na kiusalama.kumbuka miaka ya nyuma south Africa walikuwa hawashiriki michezo barani Africa kwa sababu ya siasa zao.
 
Ni kwa sababu za kideplomasia. Israel hawaelewani na mataifa ya asia kama iran, iraq
 
Yes, Israel is in the middle east but they joined UEFA so in football they are a European team. Countries can sign up with whatever confederation they like.
Australia is another example. They joined the Asian Federation so they could avoid play offs with South American teams and have an easier route in qualifying for the world cup.
 
"Between 1954 and 1974 Israel took part in the Asian Games, but political pressure exerted by Arab countries led to Israel's exclusion from the re-organized Olympic Council of Asia in 1981.[1] In the early 1990s Israel was admitted into European sports organizations, and became full member ofEuropean Olympic Committees in 1994. Israel has participated in the biannual European Youth Olympic Festival, since 1995, and the European Gamessince 2015".

Kwa mujibu wa Wikipedia Israel ilitimuliwa na waarabu ambao hawapatani kulikopelekea wao kujiunga UEFA. Kwahiyo sio kwa kupenda kwao bali walitimuliwa. Na sio kwenye michezo tu bali hata katika nyanja zingine Israel inajihusisha zaidi na Europe.
 
Tunasema kila siku wale ni wazungu,pale palestina walihamia tu toka europe na wakajiita eti wayahudi wakati si kweli.

Russia ipo europe pia
 
iliwahi kutokea miaka ya 50 kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia. isreal ilipangiwa icheze na Turkey, Turkey wakakataa so kisheria isreal ilichukua point 3 automatically. mech iliofata ilikua indonesea nao walikataa, misri ivo ivo.....karibu nchi 5 kutoka asia na africa zilikataa kucheza na isreal kwa sababu za kusiasa....mwisho wa siku isreal ilifuzu kuingia world cup bila ya kucheza mech hata moja ya kufuzu..... ila FIFA wakaona sio fair tim ingie world cup kirahisi hivi. wakasema basi isreal icheze na tim moja kutoka ulaya, ikapangwa mechi kati ya Belgium vs isreal mshindi ataingia world cup Belgium nao wakakataa kucheza. ikapangwa wales vs isreal wakakubali wales alishinda 2-0 na kuingia world cup....kiufupi isreal haina mahusiano mazuri na nchi za africa na asia ndo mana wako UEFA
 
Back
Top Bottom