Nakushukuru sana! Environmental Impact Assessment nani alifanya? Je, waliruhusiwa na NEMC?Hizo porojo za kajima tunazifahamu. Ila kabla ya ujenzi huu wa BRT maji yalikuwa hayapandi juu ya daraja. Maji yameanza kupanda juu ya daraja baada ya huu ujenzi kwa kuwa wameyang'anya maji sehemu ya kutulia bahari inapokuwa imejaa.
Kumbuka wakati huu ujenzi unaanza vifusi vyote walivyokuwa wanafukua barabara ya zamani walikuwa wanavileta hapa jangwani wakawa wanasawazisha mpaka wakapa_level na kujenga karakana moja iliyokuwa na mabomba mengi sana pale nje. Ile karakana baadae walikuja kuiondoa lakini damage ilikuwa imeshafanyika kwani lile bonde lilikuwa limesaminywa na kupunguza uwezo wake wa kuhifadhi maji. Ndio maana tangu hapo hili tatizoo limeanza.
hakuna daraja linalounganisha Salender na Coco Beach... daraja linaanzia Sea View linakuja sambamba na Salender, linaishia Ubalozi wa UK ambao uko karibu na mataa ya Salender njia panda ya Kinondoni, ambapo ndio Oysterbay inapoanzia. Coco Beach ipo kwenye edge ya Masaki, Oysterbay inapoishia. Kwa hiyo hili daraja litakuwa linachukua traffic ya Kinondoni na Mwenge pia.
hakuna njia ya jangwani inayounganisha Magomeni na jijini D'Salaam kwa sababu Magomeni ipo jijini D'Salaam...
tuuelewe kwanza mji na mabarabara kabla ya kupendekeza na kukosoa madaraja na mafuriko.....
Baada ya kuona haya mateso makubwa wanayopata wanabchi kwa kufunga barabara inayounganisha jijini Dar na Magomeni ikijirudia Mara kwa Mara kutokana na mvua kunyesha, nimekuwa nikijiuliza hivi hawa watawala wetu walitumia busara kweli kuamua kujenga daraja la kuunganisha coco beach na selander, badala ya kutoa kipaumbele cha kuliinua daraja la Jangwani?
Imekuwa ni kawaida sana kwa siku za karibuni kila mvua inaponyesha, hata kama ni ndogo, tunaambiwa kuwa barabara ya Morogoro, inayounganisha Magomeni na jijini Dar imefungwa
Hebu tujaribu ku-imagine ni madhara kiasi gani yanayopatikana kiuchumi kila barabara hiyo inapofungwa?
Hebu pia tujaribu ku-imagine ni wakazi wangapi wanapata usumbufu wa kutokwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Muhimbili au kwenda waona wapendwa wao waliolazwa katika hospitali hiyo kubwa hapa nchini kutokana na kadhia hiyo?
Lakini kwa kuwa nchi hii hivi sasa tunajua kuwa inaendeshwa kwa "misifa" ya ONE MAN SHOW, kila alitakalo bwana yule ni lazima litekelezwe, bila kwanza kuangalia ni kitu gani cha kutoa kipaumbele kwa muda tulionao
Nina hakika watu maelfu kwa maelfu, wanaathirika sana na hii barabara ya Morogoro ya kipande cha daraja la Jangwani kinachounganisha Magomeni na jijini Dar
Pia soma:
1). Magufuli: Tutajenga flyover Salender Bridge
2). Yaliyojiri Uwekaji wa jiwe la msingi Daraja la Selander
3). Wabunge pingeni na kataeni kujengwa kwa Daraja la Juu ya Bahari kutoka Coco Beach to Agakhan
Baada ya kuona haya mateso makubwa wanayopata wanabchi kwa kufunga barabara inayounganisha jijini Dar na Magomeni ikijirudia Mara kwa Mara kutokana na mvua kunyesha, nimekuwa nikijiuliza hivi hawa watawala wetu walitumia busara kweli kuamua kujenga daraja la kuunganisha Coco beach na Salenda, badala ya kutoa kipaumbele cha kuliinua daraja la Jangwani?
Imekuwa ni kawaida sana kwa siku za karibuni kila mvua inaponyesha, hata kama ni ndogo, tunaambiwa kuwa barabara ya Morogoro, inayounganisha Magomeni na jijini Dar imefungwa
Hebu tujaribu ku-imagine ni madhara kiasi gani yanayopatikana kiuchumi kila barabara hiyo inapofungwa?
Hebu pia tujaribu ku-imagine ni wakazi wangapi wanapata usumbufu wa kutokwenda kutibiwa kwenye hospitali ya Muhimbili au kwenda waona wapendwa wao waliolazwa katika hospitali hiyo kubwa hapa nchini kutokana na kadhia hiyo?
Lakini kwa kuwa nchi hii hivi sasa tunajua kuwa inaendeshwa kwa "misifa" ya ONE MAN SHOW, kila alitakalo bwana yule ni lazima litekelezwe, bila kwanza kuangalia ni kitu gani cha kutoa kipaumbele kwa muda tulionao
Nina hakika watu maelfu kwa maelfu wanaathirika sana na hii barabara ya Morogoro ya kipande cha daraja la Jangwani kinachounganisha Magomeni na jijini Dar
Pia soma:
1). Magufuli: Tutajenga flyover Salender Bridge
2). Yaliyojiri Uwekaji wa jiwe la msingi Daraja la Selander
3). Wabunge pingeni na kataeni kujengwa kwa Daraja la Juu ya Bahari kutoka Coco Beach to Agakhan
Hili jambo nimekuwa nikifikiria toka siku nyingi sana, hii stratergically ingepunguza msongomano na pia kufupisha safari.Nilisema ingekuwa busara hata kama kungejengwa daraja lingine Hananasif mpaka Upanga/ Muhimbili.
Na bado, sasa hivi wanataka kujenga daraja kwenda Zanzibar!