Hivi ni kipi hasa kinachoifanya TFF ishindwe kumiliki media zake?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Tangu ilipokuwa inaitwa FAT chini ya mzee Ndolanga na bwana Rage mpaka leo hii kuwa TFF ya Jamal Malinzi, mimi kama mdau wa michezo hususani mchezo wa mpira wa miguu sijaona juhudi zozote za viongozi wa juu wa taasisi hii muhimu kuwezesha umiliki wa vyombo vyake vya habari.

1. Kwanza hizo media zingekuwa ni vitega uchumi vizuri na vya uhakika kwa chama na kuwapunguzia adha ya kuombaomba fedha.

2.matukio makubwa ya kimichezo ya ndani na nje ya nchi kama michuano ya UEFA au ligi kuu za ulaya na hapa nyumbani mngekuwa mna- dominate na taasisi ingepiga hela nyingi sana aisee.

Lakini mpaka sasa hakuna kitu!

Tatizo ni nini hasa jamani?

Naombeni mawazo yenu wadau wenzangu...!

==== Majibu ya Jamal Malinzi====

Si vyema Football Federation kumiliki vituo vya habari.Duniani kote vyama vya mpira vinamiliki habari (content) na vituo vya redio/TV vinanunua hii content.Content ni kama mpira wa ligi,mechi za kimataifa,kombe la FA n.k.Haya ni mahusiano ya kibiashara ambayo yana guarantee a win win situation.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Last edited by a moderator:
t.f.f inamilikiwa na c.c.m wapo kwa maslahi yao sio ya wananchi wote poleni mpira wa tanganyika.
 
Tangu ilipokuwa inaitwa f.a.t chini ya mzee ndolanga na bwana rage mpaka leo hii kuwa t.f.f ya jamal malinzi, mimi kama mdau wa michezo hususani mchezo wa mpira wa miguu sijaona juhudi zozote za viongozi wa juu wa taasii hii muhimu kuwezesha umiliki wa vyombo vyake vya habari. (1)kwanza hizo media zingekuwa ni vitega uchumi vizuri na vya uhakika kwa chama na kuwapunguzia adha ya kuombaomba fedha. (2)matukio makubwa ya kimichezo ya ndani na nje ya nchi kama michuano ya uefa au ligi kuu za ulaya na hapa nyumbani mngekuwa mna- dominate na taasii ingepiga hela nyingi sana aisee. Lakini mpaka sasa hakuna kitu! Tatizo ni nini hasa jamani, naombeni mwawazo yenu wadau wenzangu...!

Tunahitaji ligi imara, sio kituo cha tv.
 
Shutzstaffel si vyema Football Federation kumiliki vituo vya habari.Duniani kote vyama vya mpira vinamiliki habari (content) na vituo vya redio/TV vinanunua hii content.Content ni kama mpira wa ligi,mechi za kimataifa,kombe la FA n.k.Haya ni mahusiano ya kibiashara ambayo yana guarantee a win win situation.
 
Mkuu hujalala...
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi kwanini unasema si vyema kwa TFF kumiliki media? kwani kuna sheria ya kimataifa ama ya ndani inayowabana kutofanya hivyo au ni bendera kufuata upepo tu? na mbona FIFA inamiliki tv station yake? how do you justify this?
 
t.f.f inamilikiwa na c.c.m wapo kwa maslahi yao sio ya wananchi wote poleni mpira wa tanganyika.
Mkuu upo sahihi maana kwenye CECAFA timu ya Tanganyika inatumia kila kitu cha muungano mpaka kocha!!!!!! Aibu.
 
Jamal Malinzi kwanini unasema si vyema kwa TFF kumiliki media? kwani kuna sheria ya kimataifa ama ya ndani inayowabana kutofanya hivyo au ni bendera kufuata upepo tu? na mbona FIFA inamiliki tv station yake? how do you justify this?
Mkuu mbona umeenda mbali mno? Timu au vilabu vinamiliki TV na radio zao kama BarcaTV, ManuTV na hata hapa nchini sasa tuna AzamTV! Ukweli ni kuwa taasisi kama hii hutumiwa kwa masilahi binafsi mno kuliko dhamira iliyokusudiwa. Pesa nyingi mno inapotelea mifukoni mwa wajanja kwenye mechi za ligi kwa kuendeleza utamaduni wetu wa ukataji wa tiketi kwenye milango ya viwanja tena siku hiyo hiyo ya mechi kuanzia pengine mchana.
 
Kweli hakuna mwenye nia ya kuendeleza soccer hapa nchini!
 
TFF wanatumia media-mtandao wa Issa Michuzi www.issamichuzi.blogspot.com kama chombo chao cha media maana kila siku taarifa za TFF tunazipata huko.

Itakuwa vizuri Malinzi akafungua official TFF thread hapa Jamiiforumsports kufuatilia mambo maana Jamiiforums ni Media-Kiongozi wa habari Tanzania.
 
Kumiliki kituo cha televisheni mathalani kunahitaji pesa nyingi, mwaka jana TFF iliahirisha uchaguzi wake kwa kisingizio cha kukosa fedha. Unaweza kukisia suala la kumiliki vyombo vya habari liko mbaloi kiasi gani...
 
...operating a media business inalipa saanaa na sidhani kama ni kweli hawa jamaa hawana uwezo wa kuinvest kwenye hili kama kweli wana nia..waachane na mazoea ya kuombaomba au kwao ni sifa na kuona wanashirikiana na wadau?
 
Ingawa huwa napata tabu kuelewa lugha za namna hii (za maigizo) acha nikujibu tu. Umesema 'operating a media business inalipa' na bado ukagusia uwezo wa 'kuinvest', ambao ni uwekezaji na sote twajua kuwa uwekezaji unataka mtaji, ambao ni pesa. Kila mtu anajua kuwa biashara ya mafuta inalipa, na bado hawaendi huko, nimekupa mfano mmoja wa matatizo ya kiuchumi ya TFF kuonesha ni kwanini ni vigumu kwao kuwekeza.
 
Wazo lako nimelielewa sana ya kwamba pesa nyingi za TFF huliwa na wajanja kwa utaratibu wa kukata tiketi mlangoni!
 
Back
Top Bottom