Hivi ni jini gani anapitia huko kwa wabunge na baadhi ya viongozi wa Chama Tawala (CCM)

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,927
6,465
Ndugu wana jamvi Nawasalimu kwa mujibu wa imani zetu.

Katika pitapita zangu mitandaoni na kwenye vyombo vya habari nimekutana na mambo yaajabu sana yanayofanywa na wabunge pomoja na baadhi ya viongozi wa Chama chetuTawala.
Mambo haya ambayo yanaenda kinyume kabisa na Katiba ya nchi yetu sio kwamba yanasikitisha tu bali yanadhalilisha hata viongozi wetu wakuu.

Hivi ni nani hajui kuwa CAG anaafanya kazi kwa mujibu wa katiba halali ya nchi na bunge halitakiwi kumuingilia au kutojaribu hata kuhoji utendaji wake? Tangu lini Bunge linalotakiwa kuisimamia serikali likang'oa macho yake yanayolipa uwezo wa kuona baadhi ya matumizi yasiyofaa ya fedha inazopitisha?

Nani huko chamani asiyejua kuwa uchaguzi uko kwa mujibu wa Sheria na hata kama hakuna mgombea mwingine kinawekwa kivuli?

Nani huko chamani asiyejua kuwa kipindi cha Urais kwa Tanzania ni miaka 5 na mwisho ni vipindi viwili vya miaka tajwa?

Jamani naomba sana kama wabunge hawajui wajibu na majikumu yao waje huku mtaani pamoja na spika wao tuwaambie wanatakiwa kufanya nini.
Inaumiza sana kusema kuwa unataka kufanya kazi na kuongea na rais halali wa Tanzania ila himtambui John Pombe Joseph Magufuli
Shame on us!!!!!!
 
Kuna huyu aliyemtaka Mungu amshukuru magu, dah yaani amejitoa ufahamu
 
Ndugu, CCM imechoka na imechakaa, kwa sasa hawajui tena hata maana ya kuwa mbunge ni nini. Inasikitisha sana.
Cha msingi 2020 tushikamane tuwatose maccm wote wasiendelee kulinajisi taifa
 
Ndugai alidhani na yeye ataitwa na CAG akahojiwe kama yeye alivyomwita. Professionals doesn't panic any time. Ndugai na wabunge wasiomtaka CAG ndo wamevuja mabilion ya wananchi kwenye (matibabu hewa) nje ya nchi sasa wanataka kuizuia report. Makonda na makontena yake walivutana na waziri wa fedha ila baadae Kila kitu kikajulikana . Time will tell.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana jamvi Nawasalimu kwa mujibu wa imani zetu.

Katika pitapita zangu mitandaoni na kwenye vyombo vya habari nimekutana na mambo yaajabu sana yanayofanywa na wabunge pomoja na baadhi ya viongozi wa Chama chetuTawala.
Mambo haya ambayo yanaenda kinyume kabisa na Katiba ya nchi yetu sio kwamba yanasikitisha tu bali yanadhalilisha hata viongozi wetu wakuu.

Hivi ni nani hajui kuwa CAG anaafanya kazi kwa mujibu wa katiba halali ya nchi na bunge halitakiwi kumuingilia au kutojaribu hata kuhoji utendaji wake? Tangu lini Bunge linalotakiwa kuisimamia serikali likang'oa macho yake yanayolipa uwezo wa kuona baadhi ya matumizi yasiyofaa ya fedha inazopitisha?

Nani huko chamani asiyejua kuwa uchaguzi uko kwa mujibu wa Sheria na hata kama hakuna mgombea mwingine kinawekwa kivuli?

Nani huko chamani asiyejua kuwa kipindi cha Urais kwa Tanzania ni miaka 5 na mwisho ni vipindi viwili vya miaka tajwa?

Jamani naomba sana kama wabunge hawajui wajibu na majikumu yao waje huku mtaani pamoja na spika wao tuwaambie wanatakiwa kufanya nini.
Inaumiza sana kusema kuwa unataka kufanya kazi na kuongea na rais halali wa Tanzania ila himtambui John Pombe Joseph Magufuli
Shame on us!!!!!!
Inapofikia hatua chama kinakuwa muhimu kuliko watu wanaowachagua haya ndiyo yanawezekana kutokea.
Lakini kwa serikali iliyoundwa na watu huu ujinga hutauona.

Kuna haja ya kuunda "serikali ya Jamhuri ya watu wa Tanzania"
Na sio "serikali ya chama cha Mapinduzi"

Kwa maana ukiita serikali ya chama viongozi watawajibika katika chama ambacho ni kikundi cha watu wachache ktk Jamuhuri ya Tz.

Lakini ikiwa serikali ya watu wa Jamuhuri ya Tz viongozi lazima watawajibika kwa Raia.

Jina serikali ya chama naona linawapa viburi sana na kujiamulia mambo kichamachama na kuwapuuza sauti watz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom