RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 4,330
- 10,537
Ii serikali ijaribu kutafakali kwa kina.Alama za mwaka huu zimebanwa sana.
2016/2017
A.80_100
B.70_79
C.60_69
D.50_59
E.40_49
Hapa ukiwa na CEE huendi chuo kikuu eti mpaka uwe na D mbili.
2014.
A.75_100.
B+.60_74
B.50_59
C.40_49
D.35_39
E.sikumbuki.
Hapa ukiwa na D mbili ulikuwa unaenda chuo kikuu
Before 2014
A.75_100
B.65_74
C.55_64
D.45_54
E.35_44
hapa ukiwa na E mbili ulikuwa unaenda chuo kikuu
Bora serikali ingeweka kuja chuo uwe na div 2 kama zamani 2007 huko,lakini kuliko sasa sasa ivi wamewabana sanawanafunzi.
Mwanafunzi wa sasa akipata 45 tatu,hana uwezo wakujiunga chuo.Lakini before 2014 angejiunga chuo chochote na course nyingi angechagua akakubaliwa.
Mwanafunzi wa sasa akipata 55 tatu anakuwa na div 2 ya point 12,wakati before 2014 angekuwa na div 1 ya 9.
Mimi nimuhanga wa hili mdogo wangu was kike ana div 3 ya point 13 combination PCM-ECE before 2014 angejiunga chuo Ila kwa mwaka huu sijui labda mbadili mawazo yenu.
Mh.Magufuli,Mama ndalichako nyie mlisoma kwa madaraja gani ya ufaulu?.Tunaomba muwaangalie ndugu zetu

Habari JF,
Nimekuwa nikijaribu kutoa mawazo yangu hasa katika mfumo wa elimu wetu kwa sababu ninayo kiu kubwa ya kuona elimu anayoipata Mtanzania inamkomboa kutoka katika dimbwi la umaskini. Ardhi tunayo tena iliyojaa rasilimali mbalimbali, watu tupo labda tunakosa tu maarifa ya jinsi ya kutumia rasilimali tulizojaliwa na Mungu. Maarifa haya yanakosekana kwa ngazi ya taifa hadi kwa mtu mmoja mmoja.
Hakuna kitu kingine ambacho kinaweza kutupatia maarifa hayo isipokuwa ni ELIMU. Sasa kama uboreshaji wa elimu yetu utategemea mawazo ya mtu mmoja au wawili, watatu sidhani kama tutafikia malengo ya kutoa elimu bora itakayowapa vijana ujuzi na maarifa ya kutosha ili kutumia rasilimali tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu kwa maendeleo ya Taifa letu.
Hofu yangu ni pale sasa maboresho yanakuwa ni mawazo ya mtu leo akiamka hivi anabadili kwa mujibu wa akili yake ilivyomtuma, akigundua amekosea kesho anabadilisha tena. Haya ninayasema kutokana na kile kinachofanywa na NECTA na TCU, sijui nini kinawasibu.
Nianze na NECTA; Mwaka 2014 NECTA walikuja na taarifa kuwa wamekusanya maoni ya wadau wa elimu kuwa wabadili mfumo wa upangaji matokeo. Hivyo wakaja division iliyo na A,B+,B,C,D,E na F. Mwaka 2015 hatujui tena kama wadau ndiyo walibadili mawazo au ni mawazo ya mtu mmoja. NECTA wakabadilishia gia angani na kuja na GPA. Je, nini kilichotokea kwenye upangaji matokeo wa 2014? Mwaka 2016 baada ya Ndalichako kuchukua ofisi ya wizara ya elimu, aliwataka watoe maelezo kwa nini GPA ni bora kuliko division.
Walikosa maelezo na hivyo kurudisha mfumo wa division lakini ikiwa hivi; A 80-100, B+ 70-79, B 60-69, C 50-59, D 40-49, S 35-39, F 0-34. Vijana wa kidato cha sita wamefanya mtihani wakijua huo ndiyo mfumo wao. Tar 11/07/2016 TCU wakatoa sifa zitakazotumika kudahili wanafunzi elimu ya juu. TCU wao wakadai zitatumika A,B,C,D,E na S. Hivyo B+ ikaondolewa na kuwekwa E. NECTA bila kutoa tena mwongozo, tar 15/07/2016 wakatoa matokeo ambayo yana mfumo uliotolewa na TCU.
TCU katika viwango walivyotoa kwenye muongozo wao, kwa wale waliomaliza kabla ya 2014 na waliomaliza 2016 walitakiwa kuwa na angalau D mbili ili kuapply chuo kikuu. Kwa kuwa D ina weight ya mbili hivyo katika masomo mawili lazima mwanafunzi awe na pointi 4 lakini D ndiyo ikiwa ni principal pass. Wamegundua kuwa wamekosea, kwa sababu kuna mtu atakuwa na BEE, hapo kwenye masomo mawili anakuwa na pointi 5. Imewalazimu jana tar 16/07/2016 wabadili msimamo wao kwa kuedit sharti la kuwa na D mbili ndipo uapply, sasa wametoa tena muongozo ambao unamtaka mwanafunzi awe na pointi 4 regardless ni DD, CE au BE. Je, hawakujua nini kitatokea? Je, ni halali kusema walikurupuka, au kuna kosa critical thinking?
Je, elimu itakuwa ya majaribio mpaka lini? Kwa nini watu wanafanya uamuzi bila kushirikisha mawazo ya watu wengine ambao ni wadau wa elimu? Natoa rai kwa wizara ya elimu, kama inataka kuboresha elimu basi ifanye mchakato wa kukusanya maoni ya wadau wa elimu. Tuachane na ukigeugeu wa kila kukicha kwa sababu tutajikuta kila mwaka tunatoa vyeti kwa wahitimu wa elimu ya sekondari hasa kidato cha sita vyenye sura tofauti tofauti katika ufaulu.