Hivi Ngombale Mwiru alikuwa ni mjamaa kweli au ilikuwa ni geresha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Ngombale Mwiru alikuwa ni mjamaa kweli au ilikuwa ni geresha?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Mar 15, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika makada wote wa chama, waliokuwa karibu na Baba wataifa, kuanzi enzi za TANU hata CCM, mzee Ngombale Mwiru ndiye alikuwa akionekana machoni mwa watu wengi, kuwa ni mjamaa wa kweli kwa kauli na vitendo. Wakati lilipotolewa Azinio la Arusha alikuwa ni msomi pekee aliyeliona azimio hilo kuwa na mapungufu, kwa kutofafanua wazi, ni aina gani ya demokrasia iliyokuwa ikizungumzwa kwenye azimio hilo. Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 1970, wanafunzi wa UDSM walipanga kufanya maandamano kwenda ikulu kwaajili ya kumshitaki makamu wa cuo hicho wa wakati huo Pius Msekwa kwa kuendekeza ubepali. mzee Ngombale wakati huo akiwa mkuu wa mkoa wa DSM alitumia fursa hiyo kuandaa matawi ya wafanyakazi wa sehemu mbali mbali, ili yajumuike katika maandamano hayo, kwa lengo la kwenda kuwaumbua kwa rais, viongozi wa mashirika hayo alioamini walikuwa wanaendekeza vitendo vya ubepari. Kwa bahati mbaya maandamano hayo yalisambaratishwa na askari kabla hayajafika kokote. Baadaye wanafunzi walituma wawakilishi wao, waliokutana na Mwalimu huko Chamwino; baada ya maelezo marefu yenye lengo la kuonyesha ni kwa namna gani Msekwa alikuwa anasaliti siasa ya ujamaa na kujitegemea, Mwalimu aliwajibu kwa sentensi moja; "Msekwa ni TANU na TANU ni Msekwa, haya kwaheri." Kwa watu wanaomjua mzee Ngombale, wanasema imani yake katika siasa ya ujamaa ilipata pigo kubwa wakati alipolazishwa kujiuzuru ukuu wa mkoa kwa kushindwa kuunga mkono hoja ya serikali bungeni; watu hao wanaelezea kwamba kwa siku alizokaa benchi yeye na familia yake walipata hadha kubwa kwakuwa hawakuwa hata na nyumba ya kuishi. wanasema aliporejeshwa kwenye utumishi wa serikali ilimlazimu atazame kando wakati mke wake akitumia mgongo wa mme wake kuendesha biashara ya ulanguzi wa bidhaa adimu ili kugharimia ujenzi wa nyumba yao; baada ya kuvunja mwiko huo inasekana mama huyo hakurudi nyuma hadi sasa.
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama walipewa majibu ya aina hiyo na mimi kuhusu swala hili la Kingunge nasema ''' KINGUNGE NI CCM NA CCM NI KINGUNGE!''
   
Loading...