Elections 2010 Hivi NEC ndio imeanza kubadilishwa?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,467
Kwenye magazeti ya leo Dr. Shein kamteua Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Makungu kuwa mwanasheria mkuu wa Z'bar. Hivi atafanya kazi zote mbili? Au hii nafasi ya huku NEC ndio iko wazi? Ndio janja ya kuwanusuru hawa mabosi wa NEC?
 
Ya umenena vyema its obvious kama kamfanya kazi nzuri ya kkukiweka chama(ccm) madarakani ndio muda muafaka wa fadhila
 
Kwenye magazeti ya leo Dr. Shein kamteua Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Makungu kuwa mwanasheria mkuu wa Z'bar. Hivi atafanya kazi zote mbili? Au hii nafasi ya huku NEC ndio iko wazi? Ndio janja ya kuwanusuru hawa mabosi wa NEC?

hapa ndo tunapotaka mabadiliko ya katiba, ivi ulimtegemea jamaa kama huyu atende haki na je kama alishaambiwa kwamba nikishinda tuu unakuwa mwanasheria mkuu hata ungekuwa wewe ungechakachua to the maximum, naam naona kazi alotumwa kaifanya ipasavyo..kama uanasheria mkuu mwanangu, umefanya kazi nzito..wehu wengine hawa..
 
Si NEC wala ZEC inayobadilishwa ni watu. Mabadiliko ya NEC na ZEC ni ya kimfumo zaidi kuliko watu. Endaikawa mabadiliko aliyoyafanya shein zanzibar ni takrima kwa kazi nzuri alioifanya ya kumwibia kura za ushindi. CCM hata siku moja hawana mawazo ya kutengeneza mifumo ya taasisi za kuongoza nchi kwa haki, kwa lengo la kuhakikisha wizi na ufisadi unaendelea kuwa utamaduni wa taifa hili.
 
Kwenye magazeti ya leo Dr. Shein kamteua Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Makungu kuwa mwanasheria mkuu wa Z'bar. Hivi atafanya kazi zote mbili? Au hii nafasi ya huku NEC ndio iko wazi? Ndio janja ya kuwanusuru hawa mabosi wa NEC?
Kubadilisha sura siyo mageuzi tunayoyataka.......................tunachotaka ni NEC ambayo inateuliwa na wadau wa asasi mbalimbali na wala siyo kuteuliwa na mdau mmoja tu ambaye ana masilahi mazito ya kuyachakachua matokeo aendelee kutawala isivyo halali na kinyume cha sheria...........................
 
Tumsubiri JK naye kwa fadhila zake kwa watu mbalimbali, waliompiga TAFU ktk uchakachuaji
 
Back
Top Bottom