Hivi ndugu zangu CHADEMA mnafikiri CCM na wabunge wake watakubali Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi kwa maneno yenu matupu?

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
376
1,000
Kama hizo ndizo fikra zenu/zetu ni wazi tunajidanganya.

CCM ni mchwa uliozoea kula vinono kupitia mapungufu ya Taasisi tajwa hapo juu.CCM na watu wake kamwe hawawezi kakubali kuanzishwa kwa Taasisi huru ambazo kwayo itapelekea hata wao kuchunguzwa na hata kushtakiwa kwa makosa waliyopata kuyafanya huko nyuma.

Nini kifanyike;

Kwanza lazima wachache waliojitoa mhanga kupigania haki waungwe mkono na wasibezwe.

Pili Watanzania sote hasa vijana ni muda sahihi kujitoa mhanga kuitetea kesho yetu kutoka mkononi mwa hao mchwa wala keki ya Taifa.

Tatu si wakati wa hayo mapambano kuwaachia Chadema pekee bali tutambue kila awaye inampasa kuingia mzima mzima pasi na kujali changamoto zilizo mbele yetu.

Ni wakati sahihi kwa vijana kufanya lolote alipo litalokuwa chanya kwenye mapambano ya kuidai haki.

Ni wakati sahihi wa mbwai isiyo na majeraha kwa Nchi yetu.

Ni wakati sahihi kabisa wa kuipambania kesho yetu.

Tutambue,kumuua mwizi ama kibaha mwenye dhamira ya kukudhulumu wala si kosa kisheria.

Vilevile kufa ukiutetea uhuru wako napo si kosa kisheria.
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,766
2,000
Wanataka katiba mpya kwa maslaji yao binafsi
Kikwete aliwapa nafasi katiba mpya iandaliwe, sijui hata walifanyaje mchakato ukapotea
Kaja Magufuli kawasmbia sio kipaumbele changu,wameufyata
Kuja Mama Samia kawaambia subirini kwanza nijenge nchi, hawataki wanataka sasa hivi
Ukiwatafakari hao jamaa wapo kwa maslahi yao tu
Wangeenda vizuri na huyu mama mbona katiba ingepatikana
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,766
2,000
Hii kauli bila timeframe ni bure,anaweza kuwa anamaanisha sibirini siku ya kiama ndio tutaanza mchakato wa Katiba mpya.

Asitufanye Watoto wa wakwea minazi.
Sasa si bora huyo kasema subirini
Yule mwingine kawaambia sio kipaumbele changu wakaufyata kimya
Huyu wangeenda nae taratibu hilo jambo lingewezekana kabisa
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,735
2,000
Katiba mpya aipigi kura,jitokezeeni kwa wingi kuikataa ccm lzm ilale hata kama kingai atakuwa igp plus kigogo kuunga juhudi bado haitoboi 2025.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
26,016
2,000
CCM kukubali katiba mpya ni sawa na kuyarudisha madaraka yao kwa wananchi - si jambo dogo hili.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,441
2,000
Katiba mpya aipigi kura,jitokezeeni kwa wingi kuikataa ccm lzm ilale hata kama kingai atakuwa igp plus kigogo kuunga juhudi bado haitoboi 2025.

Huko kwenye kura ndio zinahesabiwa kihalali? Njia sahihi kwa sasa ya kuipata katiba mpya ni machafuko tu.
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,735
2,000
Huko kwenye kura ndio zinahesabiwa kihalali? Njia sahihi kwa sasa ya kuipata katiba mpya ni machafuko tu.
Machafuko ya nn CCM ilishakufa kitambo inapumulia police tu,wanachama wake wazee na vikongwe idadi yao inapungua KILA siku.

Wanasema Wana wanachama milioni 9 mbona bado wanaiba kura na Kupita bila kupingwa.
 
igogondwa

JF-Expert Member
Aug 1, 2021
1,784
2,000
Wanataka katiba mpya kwa maslaji yao binafsi
Kikwete aliwapa nafasi katiba mpya iandaliwe, sijui hata walifanyaje mchakato ukapotea
Kaja Magufuli kawasmbia sio kipaumbele changu,wameufyata
Kuja Mama Samia kawaambia subirini kwanza nijenge nchi, hawataki wanataka sasa hivi
Ukiwatafakari hao jamaa wapo kwa maslahi yao tu
Wangeenda vizuri na huyu mama mbona katiba ingepatikana
Kama ambavyo wewe uko na maslahi ya mbogamboga...
 
igogondwa

JF-Expert Member
Aug 1, 2021
1,784
2,000
Sasa si bora huyo kasema subirini
Yule mwingine kawaambia sio kipaumbele changu wakaufyata kimya
Huyu wangeenda nae taratibu hilo jambo lingewezekana kabisa
Huyo wa 'siyo kipaumbele changu' yuko wapi sasa? Karma is a....
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,441
2,000
Machafuko ya nn ccm ilishakufa kitambo inapumulia police tu,wanachama wake wazee na vikongwe idadi yao inapungua KILA siku.
Wanasema Wana wanachama milioni 9 mbona bado wanaiba kura na Kupita bila kupingwa.

Wanaowaweka ccm madarakani ni vyombo vya dola, sasa hapo bila machafuko unategemea nini?
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,766
2,000
Kama ambavyo wewe uko na maslahi ya mbogamboga...
Mimi sio mboga mboga
Na aio kila anaekinzana na ninyi kimawazo ni ccm, kama hampendi kukosolewa msiwe mnakosoa na wengine ninyi sio malaika kwamba hamkosei
 
nautaka tena

Senior Member
Jun 29, 2021
184
250
Hivi ni kwanini hili suala linakua la chadema nafikiri kila mtanzania angeunga mkono kinachitokea mahakamani kwa kweli ni maumivu makubwa kwa mtu mwenye kufikiri tuna Hali mbaya Kama nchi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom