Hivi ndoa za Roman Catholic ukiingia kunakutoka kweli?

Tumia akili basi. Kanisani ni utaratibu lakini uhalisia wa maisha kuna ambayo huwezi vumilia, kwa nini mahakama inavunja ndoa, kwa nii talaka inaruhusiwa. Ni haya haya. Mfumo uliopo ni mbovuuuuuuu
Kama huo utaratibu unautambua na unaona una nafasi yake kwanini u "underestimate" au ulazimike kufanya hivyo? Kila mahala pana utaratibu wake.Lakini pia hata hayo ambayo huwezi kuvumilia nadhani kuna taratibu zake za kubatilisha ndoa,Sio kwamba haiwezekani kabisa.Lakini kimsingi kiapo,tena mbele ya madhabahu na mbele ya mashahidi ni very Serious.Pale hauli kiapo mbele ya hakimu kiongozi! Pale unakula kiapo mbele ya Mungu! Sasa Mahakama na Mungu nani zaidi?
 
Alichokiunganisha Mungu..... (malizia)
Huo ni msemo tu. Nadharia. Kiuhalisia sio Mungu ameunganisha. Ni nyie wawili mmeungana na ndio maana hata askofu anaweza kuvunja ndoa. Mahakama wakati wote inavunja. Padri au mchungaji ni Mungu?
Huyu huyi anasema msizini alafu anakuja kula mke wangu ndio Mungu. Ebu acha bwana. Mke anadanganya anaenda maombi kumbe anapigwa na aliyetufungisha ndoa. Hadi anamzalisha. Ebu acha bwana
 
Huo ni msemo tu. Nadharia. Kiuhalisia sio Mungu ameunganisha. Ni nyie wawili mmeungana na ndio maana hata askofu anaweza kuvunja ndoa. Mahakama wakati wote inavunja. Padri au mchungaji ni Mungu?
Mkuu nina wasiwasi na imani yako.Neno la Mungu unawezaje kuita msemo tu?

Marko 10:9
Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

Kanisa pekee ndilo lenye mamlaka hayo ya kubatilisha ndoa,Wala si Mahakama wala Hakimu.

Mathayo 16:19
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

Ndoa halali ikishafungwa,Si Askofu wala Padre anayeweza kutenganisha/kuvunja.Bali wanachoweza kufanya ni kubatilisha ndoa iliyobainika kuwa na dosari kwa maana nyingine ndoa hiyo haikuwepo!
 
Uwoya hadi alifunga ndoa na dogo janja ya kiislam lakini bado kanisa linamtambua hakuna cha kutengwa wala kunyimwa sakramenti.
Kama unalishuhudia hili kuwa una uhakika nalo, na kwamba unalisema hadharani mbele ya Mungu, basi kuna uwajibikaji haujafanyika katika Parokia husika
 
Kuvunja ndoa kupo, Ila kuwe na sababu kubwa kabisa, tena inayojirudia zaidi ya Mara 2 ndio unaruhusiwa kuivunja iyo ndoa.
 
Ona unavyoweka vitisho na hukumu. Binadamu acheni hukumu. Hata Yesu hakumhukumu yule mwanamke kahaba
Kama unalishuhudia hili kuwa una uhakika nalo, na kwamba unalisema hadharani mbele ya Mungu, basi kuna uwajibikaji haujafanyika katika Parokia husika
 
Mie sio mkatoliki mkuu so dont panic
Usichokielewa ni kipi kiongozi? Hautaki sheria za katoliki basi nenda kafunge ndoa makanisa au dini zingine.Ila ukishafunga ndoa Mbele ya madhabahu ya Kanisa Katoliki na padre akishasema "Alichokiunganisha Mungu,Mwanadamu asikitenganishe" basi ndoa hiyo itabaki siku zote! Kwingineko ni kujidanganya tu.
 
Sio ya kikatoliki. Christian marrige hakuna kuachana mpaka kifo kiwatenganishe. Kile kiapo mnachoapa m ele ya madhabahu na mbele ya waamini wenzako ndio shida.

Hii kitu Joti ilimshinda kabisa.😁😁😁
Mkuu nii mapokeo tu ya kanisa. Ila ukweli ni kwamba kwenye biblia kutoka mwanzo Hadi ufunuo, hutakuta hicho kiapo cha "nitakuwa na wewe katika shida na raha Hadi kifo kitutenge". Hakuna..

Ata uwe umesoma theolojia ya wapi still msingi mkubwa utakuwa ni bible yenyewe ambayo Haina kiapo hicho.

Kuna misimamo mitatu kwa wakristu ambapo ndo tunajikuta wengine tumekuwa kwenye viapo Kama hivyo.

Kwanza msimamo wa Biblia unasemaje yenyewe. Pili msimamo wa kanisa na mapokeo ya kanisa, na mwisho msimamo wa Wakristo wote. Ambao kwa lugha ya theology wanaita.. "Christian or apostalical Creed. (Statement of the shared beliefs)

Jamaniii
Mtu anakuzingua arafu eti unakuwa nae katika shida na rahaa... Thubutu...

Kuna ndoa zina mizengwe bna, Yesu alibebeshwa msalaba wa mbao, lakin kuna ndoa zingine watu wanabebesha wenzi wao misalaba ya chuma si mbao Tena...
 
Naomba niwasahihishe wachangiaji wote.

ni KUBATILISHA ndoa sio KUVUNJA ndoa.

Hakuna mwenye mamlaka ya kuvunja ndoa isipokuwa yule aliyeifungisha (MUNGU)

Marko 19:16
Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

Kinachofanyika ni kubatilisha.Kwa maana nyingine ndoa hiyo ni batili yaani haikuwepo tokea mwanzo.Lakini kama ilishakuwepo basi itabaki hivyo hivyo.
 
Ova.
 
Naandika Kama katekista tuelewane.
Kanisa katoliki halivunji ndoa kwasababu yoyote ile msidanganyane ati ukimfumania na mashahidi itavunjwa.

Ipo mahakama ya kanisa na hapo zinatumika sheria za kanisa pamoja na biblia."samehe mara saba sabini "pamoja na kile kisa cha mwanamke mzinzi aliyetakiwa kupigwa mawe afe yesu akamuokoa Kwa kuwaambia asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga mawe, huwa ni Mistari inayopangua hoja ya kutaka kuvunja ndoa Kwa uzinzi.

Ni kweli kwamba kuna ndoa ambazo hutangazwa batili au kutenguliwa Yani haisemwi kwamba ndoa imevunjwa bali inatangazwa kwamba Ilikuwa batili Yani haikuwapo kwasababu haikufuata misingi ya sheria za kanisa au ilikosa sifa kabla na baada ya Kufunga.
Kwa mfano waliofunga kubainika ni ndugu, mmojawapo wa wanandoa kubainika alikuwa na ndoa nyingine ya kanisa,mwanandoa kukosa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa tangu mwanzo na kwamba alimficha mwenzake.
Lakini ugumba hauvunji ndoa.
Ugumba unavunja Kama muhusika aliingia akijua Ana tatizo hilo
 
Marko 10:9

Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

Ova.
Ndugu yangu.
Marko 10:9

Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

Ova.
Mkuu unapo itafisiri Biblia jitahidi Sana kutafuta maana halisi ya mwandishi alitaka wewe msomaji uelewe nini, alikuwa ana waambia watu gan? kwa wakati gani? hao watu walikuwa na tamaduni zipi? Kwann aliwaambia hiv na sis tunajifunza nini? N.k

usiweke tena mawazo yako tofauti na canon ya mwandishi mwenyewe. Nadhani utakuwa unaelewa kanuni hiz ( exegesis and Eisegesis) ni muhim sana kuwa nazo makini kwenye kusoma neno la Mungu.

Unasoma neno, unalitoa kulingana na matakwa ya mwandishi, si kusoma neno ukaliongezea bias flan flan.

Sasa apa umesema Mark 10:9 "Alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe" it's ok. Swali kwa hiyo wewe ndo ukatafisiri kwamba ndo kiapo cha nitakuwa na wewe katika shida na raha?

Ndo tafisiri sahihi ya andiko Hilo kweli? Ndo msingi wa kiapo cha ndoa?........ Au kuna mstari mwingine wa hicho kiapo?

Mungu Kama ameunganisha Jenifa na Paulo kuwa mwili mmoja. Hatakiwi kutokea rafik, wifi, Kaka, au mtu yeyote kuwatenganisha. Lakin pia mkuu, kumbuka huo mstari hausemi chochote kuhusu wao wasipoelewana. Yaan Jenifa na Paulo wasipo endana wao kwa wao wafanyeje,

Biblia iko kimia. So ukiona kimia Jibu linaweza kuwa Yes or No! So wakizinguana ikitokea Yes powa ikitokea No still Powa. Sema tu hapa tunakuja kubanwa na neno la Mungu la kusamehe 7x70. Na kuchukuliana + Upendo Kama tunavyo ambiwa na Biblia kuwapenda wanao tukwaza.. otherwise tuna shida hapa.

Mkuu, ata kwa mujibu wa kile kiapo na Biblia, kwamba hatuachani mpaka kifo kitutenganishe, fine. Lakin je umewahi kujiuliza kuna vifo vya aina ngapi? Hukawai kusikia mtu amekufa kifo Cha kiroho? Au unajua kifo Cha kimwilili tu?

Je kifo Cha kiroho na Cha kimwili, ni kipi kibaya sana mbele za Mungu? Adam na Eva walikufa vifo vingapi? Na kati ya vifo vyao ni kifo kipi mpaka leo kimetuletea laana?

Yaaani kwenye ndoa niwe na lijitu linasheratika haswaaa ,maadili yote ya kiubinadamu linayaacha, halina hata 0.0001 ya hofu ya Mungu ndani yake, si limekufa kiroho Hilo? mpaka mbele za Mungu si linanuka japo linatembea, arafu eti ni subiri afe kifo Cha mwili ndo tuachane hakuuuu!!!!

So msiachane Hadi kifo kiwatenganishe ni farisafa kubwa...

Ngoja nipause kidogo.
 
Naomba niwasahihishe wachangiaji wote.

ni KUBATILISHA ndoa sio KUVUNJA ndoa.

Hakuna mwenye mamlaka ya kuvunja ndoa isipokuwa yule aliyeifungisha (MUNGU)

Marko 19:16
Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

Kinachofanyika ni kubatilisha.Kwa maana nyingine ndoa hiyo ni batili yaani haikuwepo tokea mwanzo.Lakini kama ilishakuwepo basi itabaki hivyo hivyo.
Yote yalikwisha msarabani, unaita damu ya Yesu na unafuta viapo na laana zote kwa Mamlaka Jina na Damu ya Yesu. Hakuna kisichofutika
 
Halafu watu wanachanganya swala la kusamehe.

Unaweza ukamsamehe mtu lakini haina maana ulokosewa una utayari wa kurudiana na mwenzi wako wa ndoa.

Unaweza ukamsamehe mtu lakini ukajiweka mbali naye ili msije mkaumizana mioyo tena.
 
Back
Top Bottom