Hivi ndiyo vipindi 5 vyenye ushawishi mkubwa kwenye Media za Bongo

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Wakuu habari zenu..

Huu ni wakati ambao Watanzania wengi wapo macho sana kusikiliza taarifa kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania hasa zinazohusu uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu 2020. Kuna wale wenzangu na mimi ambao siasa kidogo na mambo mengine zaidi.

Leo ningependa nikupe mtazamo wangu wa vipindi vitano vya Radio na Tv vyenye ushawishi mkubwa sana wa kusikilizwa au kutazamwa kwenye media za hapa Bongo.

1. Friday Night Live (FNL)
Hiki ni kipindi ambacho huruka kila siku za Ijumaa kuanzia majira ya saa 3:00 usiku hadi saa 5:00 usiku. Kipindi hiki ambacho hurushwa na kituo cha televisheni cha EATV ni kipindi ambacho kinaonekana kuwa na mvuto sana. Ukubwa wa kipindi hiki unatokana na ukweli kwamba wasanii wengi wa Afrika Mashariki wanapohitaji kutambulisha video zao mpya basi hufika hapo kuzitambulisha na hii huvutia watazamaji wengi hasa vijana kukitazama ili waone video mpya iliyotoka/zilizotoka.

2. XXL ya Clouds Fm:
Unaweza kukataa au kukubali lakini mnyonge mnyongeni isipokuwa msimdhulumu haki yake. XXL ni moja kati ya show kali sana ambayo huruka kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 7:00 mchana hadi saa 10:00 alasiri.

Hiki ni kipindi ambacho kimekuwa kivutio sana kwa vijana ambao wanapenda kupata habari za muziki wa ndani na nje ya Tanzania huku ma-dj wakali wakipamba kipindi.

3. Sitasahau:
Hiki ni kipindi ambacho mwanzoni kilikuwa kikiendeshwa na mtangazaji Roi Maganga ambaye kwa sasa hayupo tena pale RFA. Kipindi hiki kimekuwa kivutio cha wengi sio watoto, wazee na hata vijana na hualika wageni kutoa simulizi za mambo magumu waliyoyapitia kwenye maisha yao. Kipindi hiki huruka kila siku za Jumapili kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 5:00 pale Radio Free Africa.

Clouds Fm walikuja na kipindi cha kufanana na"Sitasahau" na wakakipa jina la "Njia panda" lakini bado ile ladha ya kipekee ya Sitasahau bado ipo juu.

4. Papaso ya TBC Fm:
Kuna watu wanadai kuwa kipindi hiki kimepoteza mvuto lakini nikwambie kitu kimoja kuwa hakuna kipindi chenye wasikilizaji wengi hasa vijijini kama PAPASO. Mtangazaji wa kipindi hiki D'jaro Arungu mbali na kujizolea umaarufu mkubwa lakini ameshinda tunzo kadhaa za kuwa Mtangazaji bora kupitia kipindi chake.

Papaso huruka kila siku za juma isipokuwa Jumamosi na Jumapili kuanzia 19:00 hadi 22:00 Maudhui ya kipindi hiki yapo kwenye burudani, habari, simulizi n.k.

5. ITV Habari:
Japo karibia vituo vyote vya televisheni vinasoma habari lakini bado ITV Habari kinakuwa na kipindi ambacho kina watazamaji wengi sana. Kipindi hiki huruka kila siku saa 2:00 usiku hadi saa 3:00 usiku. Ubora wa kipindi hiki unatokana na kuenea kwa reporters wake wengi nchi nzima na nje ya Tanzania na hutoa habari zenye uhakika na zilizohaririwa kwa kiwango cha juu.

HITIMISHO
Vipindi hivyo hapo juu ni kwa mujibu wa utafiti wangu nilioufanya kwa miaka kadhaa. Mpangilio huu pia hauhusiki na ni media gani yenye wasikilizaji wengi ila nimeegemea kwenye kipindi kama kipindi. Unaweza kuja na maoni yako pia ambayo yanaweza kuwa kinyume na mimi au ukaongeza list.

Naomba kuwasilisha....
 
KWENYE FRIDAY NIGHT LIVE YA EATV NAKUBALI NA KWENYE XXL NAKUBALI PIA, KWENYE HABARI YA ITV ILIKUA NI KWELI ILA KWASASA BAADA YA MEDIA NYINGI KUBANWA NA UTAWALA KIDOGO ITV WAMESHUKA NA KWASASA AZAM HABARI HAWANA MPINZANI.
HIVYO VIPINDI VINGINE SINA UHAKIKA SANA NA UTAFITI WAKO.
 
Ahsante kwa maoni yako
 
Naikubali mno ITV habari UTV ndio siwaelewi kabisa muda mwingi habari ni moja tu na mahojiano marefu juu ya swala moja mf kipindi cha Corona mwanzo mwisho na sasa hivi Uchguzi mwanzo mwisho as if hamna incidents zozote nchini
 
Wao hutaka kuongelea kwa undani zile habari kubwa na kuacha zingine
 
Kwenye habari ni vipindi viwili tu vyenye mvuto, hapa Tanzania kwa sasa.
-BBC-swahilli (Star Tv, saa tatu usiku)
-UTV(Azam) (saa 2usiku)

Tatizo la UTV ipo kwenye king'amuzi cha Azam pekee, huwezi kuipata kwenye Startimes, DSTV, Continental, Satelite dish(FTA), Ting, Zuku nk.
Binafsi nilikuwa siifahamu UTV habari mpaka siku nilipo miliki king'amuzi cha Azam, na toka nianze kuiangalia sijajuta na wala sijarudia tena kutazama ule uchafu wa ITV-habari niliokuwa nimeuzoea.
 
Tunayaheshimu mawazo yako
 
Yaani mzee wangu bila kuangalia habari ITV hiyo haijawa habari..

Japo habari kibongobongo now ni UTV na BBC Swahili saa tatu kupitia StarTv
 
Yaani mzee wangu bila kuangalia habari ITV hiyo haijawa habari..

Japo habari kibongobongo now ni UTV na BBC Swahili saa tatu kupitia StarTv

Ni kweli kabisa ila kama umesoma maelezo ya mchangiaji hapo juu amesema udhaifu wa UTV ni kwamba ili uipate ni hadi uwe na king'amuzi cha Azam tu. Pia UTV huwa wanajikita sana kuongelea habari moja ambayo wataona ina mashiko sana mfano, kipindi cha vuguvugu la Corona wao waliegemea sana kutoa taarifa za Corona tu kama ilivyo kwa sasa walivyojikita kwenye uchaguzi.

Kuhusu BBC ya Star Tv ni kweli ipo vizuri lakini tatizo mfumo wa vipindi vya star Tv siku hizi umekuwa sio mzuri sana kiasi cha watu kuipuuza kwa namna moja au nyingine.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom